Hapa Jf kuna macomedian wengi. Kuna mtu anasema eti ndani ya bunge la Kenya kuna pro CCM na pro Magufuli. Hawa watu huwa wanaona tukijibizana nao humu alafu wanadhani eti wakenya wote wanajua kuhusu chuki zao dhidi ya Kenya. Watu hawana hiyo time na hata bunge letu halijakaa hata siku moja kwenye kikao likajadili kuhusu masuala ya Tz isipokuwa kupeana rambi rambi zao wakati wa misiba. Kenya haina bifu na nchi yeyote E.Africa, huu msimamo umetusaidia sana kwasababu tumeweza kuwa na muda wa kutosha wa kushughulikia masuala yetu ya ndani kwa ndani. Ila imetukosti kwasababu jirani zetu wenye nia mbaya wameona ni kama udhaifu na heshima haipo tena. Sidhani kuna mbunge yeyote awe wa Jubilee au NASA ambaye anaweza akasimama mbele ya wabunge wenzake alafu aanze kuendeleza agenda za nchi yeyote ile nyingine huku akitegemea kuungwa mkono. Hapo ndipo napowapendea wakenya wenzangu, iwe ni viongozi au wananchi mwendo huwa ni ule ule , Kenya mbele shetani nyuma.