Kama rasilmali zilizosheheni humu nchini na kwingineko Afrika zengelitumika kwa ustawi wa wananchi, huduma zote muhimu za kijami viz. elimu, afya, maji, nishati nk zingepatikana kama sio bure, kwa gharama nafuu sana ambapo kila mwananchi angemudu. Bali rasilmali hizo zinanufaisha mataifa ya nje kupitia uwakala wa watawala wetu, nao wakinufaika na ‘crumbs’ zinazodondoshwa na hao wakubwa.
Miaka ya 70 Walter Rodney aliandika kitabu, “How Europe underdeveloped Afrika” akitanabahisha mahusiano ya kinyonyaji kati mataifa ya magharibi (Center) na mataifa ya Africa (Periphery). Na mahusiano hayo yaliwezeshwa kwa ushirikiano kati ya watawala wa mataifa ya magharibi (Center of Center) na watawala wa mataifa ya Africa (Center of Periphery). Nadharia hii (Center-Periphery Theory) ya Rodney ilikuja kupewa nguvu na professor Chachage (Makuwadi wa Mabepari) na John Perkins (Confession of an Economic Hitman)
Leo wigo wa unyonyaji wa rasilmali za Afrika umetanuka zaidi ukihusisha Amerika na mataifa ya Asia yenye uchumi mkubwa kama Urusi na China. Walter Rodney alishatangulia lakini nadharia yake bado inaishi, sio tu kama nadharia bali hali halisi.