Kenya Huwa wanatuzidi vipi kwenye uchumi Tanzania?

Nchi ambayo ardhi inamilikiwa na matajiri ni lazima iwe na uchumi mkubwa kila siku ardhi inazalisha
 
thamani ya pesa kuwa kubwa haina uhusiano na kuendelea zaidi au kuwa na maisha mazuri zaidi, Pesa ya Oman ndio yenye thamani kubwa zaidi ukilinganisha na nchi nyengine 5 za kifalme ziloizunguka, Lakini wao ndio wenye standard ndogo ya maisha ukilinganisha na wenzao.
 
kuna sababu ya sis kuwa hapa hata hivo hiyo kenya n swala la muda tu akipatikana kiongoz shupavu tutakua juu
 
Inabidi ifanyike namna hii reply iwe pinned kwenye hii thread pale juu kabisa kila mmoja asome, umetisha b…
 
Kwenye uchumi kenya wametupita.

Acha niongelee masuala mengine.

1 Kwenye ishu ya maisha kuwa magumu
Nchi zilizo tawaliwa na British zina mfumo tofauti wa maisha.

Kenya wana mfumo tofauti wa maisha sio kama sisi TZ
Wao wana tofauti kubwa kwenye gap kati ya Tajiri na maskini. Ndo maana unasema maskin wa kenya ni fukara kupindukia na tajiri wa huko ana ukwasi kupindukia.

Hii imeletwa na mfumo wao wa maisha tangu enzi za ukoloni. Wale wa kenya waliokua wanafanya kazi kwa wazungu, wengi walipata elimu na pesa za kujikimu na kuanza maisha mapema tofauti na wale waliokuwa raia wa kawaida.
Tofauti na sisi mwalimu alituweka kwenye ujamaa ndo maana tabaka kati ya tajiri na maskini halionekani sana, ni kama wote tupo sawa.

Nazan umeona maisha yao yalivyo tofauti. Bidhaa zao nyiingi wanategemea kununua supermarket kuliko maduka ya mangi kama sisi. Wao hadi unga wa mahindi utaupata supermarket ndo maana utaskia kelele kua bei ya unga imepanda

2
. Ishu nyingine Raia wa kenya kulingana na katiba yao wanamiliki ardhi na serikali haina haki ya kumpangia au kuwanyang'anya ardhi. Tofauti na sisi ambao ardhi ni mali ya serikali na Rais akiamulisha uondeke kwenye ardhi yako basi huna la kusema

3 Wakenya wengi wapo nje ya nchi kwa sababu ya kiingereza wanatafta fursa nje ya mipaka na wanapa fedha huko na kutuma nchini kwao. Sisi walioko nje ya nchi ni wachache na ishu ya lugha inafanya watu wasitafte fursa nje ya mipaka, Tupo wote nchine tunategemea serikal itupe ajira au tujiajiri.

4 Ishu ya Vijana GenZ au wananchi kuishinikizas erikali kufanya wao wanachotaka ni jambo kubwa kwani serikali itakua inawaza mara mbilmbili kabla ya kufanya maamuzi yanayowahusu wananchi.
Ila kwetu TZ serikal ikisha amua hamna wa kuongea, hamna Freedom of speech ya kuzungumza mawazo yako. tena kama yatayolenga kuikosoa serikali ndo hautojulikana ulipo
👇👇👇

 
Hivyo viwanda vidogo vinatuzidi Nini sisi wenye dhahabu, Tanzanite, Mbuga, kilimo, biashara n.k
Kuwa na pua kubwa sio wingi wa kamasi. Swali ni kwamba wewe mwenye dhahabu au hizo tanzanite kwanini usimzidi huyo asiyekuwa nacho.
 
Fala ,huna akilli
 
waneexport sana bidhaa zao. Kuna zingine ni za kwetu kama maua vipepeo
 
Tz hatuna viwanda kuwazidi,mfano bidhaa za plastics,sufuria Kenya wametuacha mbali sana,tuna import toka huko.....hapa viwanda kama Maxima,Oceans au BGI kwa sufuria na Jambo,Seifi,cello bidhaa hazina ubora ukilinganisha na Kenya....kwahiyo tunawapelekea Dollars nyingi sana
 
Kusema kwl Individual level ya wakazi wa kenya na Tz Wabongo wako mbali sana kwa wakenya, mimi nimezaliwa Sirari Tanzania ambapo ni mpakani Mwa kenya na tz, Kwa bahati nzuri maeneo yote uliyotaja nayajua kwa uzuri na nilishaenda mara kibao, Migori nimeenda kupitia njia ya Isbania Kurya, Mabera, Migori kisii, Nakulu, kisumu na nairobi, kusema kwl wakazi wa kenya wanatia huruma sana ujuaji mwingi kizungu kingi ila njaa ni kubwa sana kwao
 
Kwenye upuuzi tumewazidi,ila kwenye mambo serious hatujawazidi
 
Kuna GDP na GDP per capital kwenye GDP KENYA wametupita ila kwenye GDP per capital Tumewapita na wametuzidi kwenye deni la taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…