Kenya Huwa wanatuzidi vipi kwenye uchumi Tanzania?

Kenya Huwa wanatuzidi vipi kwenye uchumi Tanzania?

Kwa uelewa wangu; Kenya kiiuchumi wako Juu yetu Tz kwa Sasa lakini speed ya ukuaji na ujenzi wa nchi 🇹🇿 mbeleni hawatatuweza.Kenya Uchumi unamilikiwa na matajili wachachee mf.aridhi, viwanda nk.Raia wengi ni choka mbaya kuliko maskini wa Tz.

Tatizo sisi kua nyuma limetengenezwa pindi Nyerere alipoleta Socialism ambapo private ownership of major means of production was banned 🚫 hivyo viwanda vikawa ni miliki ya serikali system hii ilikuja kufa 1990s ndipo tukarudi mfumo wa capitalism tena,wakati huo Kenya wao hawakutanga Tanga capitalism mwanzo mwishooo.

Hivyo basi Kenya wako Juu lakini ni swalaa la Mdaa tu hope mpaka 2050,Tz itakua mbele ya Kenya kivyovyote i.e Kiiuchumi,miundimbinu. Ni rahisi kutoboa maisha kwa Maskini wa Tz kuliko maskini wa Kenyaaaa.
Nchi ambayo ardhi inamilikiwa na matajiri ni lazima iwe na uchumi mkubwa kila siku ardhi inazalisha
 
thamani ya pesa kuwa kubwa haina uhusiano na kuendelea zaidi au kuwa na maisha mazuri zaidi, Pesa ya Oman ndio yenye thamani kubwa zaidi ukilinganisha na nchi nyengine 5 za kifalme ziloizunguka, Lakini wao ndio wenye standard ndogo ya maisha ukilinganisha na wenzao.
 
kuna sababu ya sis kuwa hapa hata hivo hiyo kenya n swala la muda tu akipatikana kiongoz shupavu tutakua juu
 
Umeuliza swali zuri sana, kwa nia ya kujifunza. Tofauti za Kimsingi za Kiuchumi kati ya Kenya na Tanzania ni njia za mapato yao ya taifa kwa mifumo.

1. Ukubwa wa Pato la Taifa (GDP) kwa Mtu
Pato la Taifa kwa kila mtu ni kiashiria kinachoonesha wastani wa kipato cha raia Kwa siku.

- Kenya: Kufikia mwaka 2023, GDP kwa kila mtu ni karibu $2,200, kutokana na sekta za huduma na biashara zilizokomaa.

- Tanzania: GDP kwa kila mtu ni takriban $1,200, ikiakisi uchumi unaotegemea kilimo cha kujikimu na uzalishaji mdogo wa viwandani.

Uchambuzi: Kenya ina wastani wa pato la juu kwa mtu kwa sababu sekta ya huduma (ambayo huchangia 50% ya GDP) imekua kwa kasi.
Tanzania bado inaelekeza rasilimali zaidi katika kilimo ambacho kinachangia 25% ya GDP lakini kinahusisha 65% ya nguvu kazi.

2. Sekta ya Huduma
- Kenya: Sekta ya huduma inachangia asilimia kubwa ya GDP, hasa kutokana na,
- Huduma za kifedha: Kenya imeanzisha mfumo wa malipo wa M-Pesa, unaowakilisha zaidi ya 40% ya miamala ya kifedha nchini.
- Elimu na Teknolojia: Kuna viwango vya juu vya ufahamu wa TEHAMA na uwekezaji katika elimu ya juu.
- Utalii: Utalii nchini Kenya unachangia karibu 10% ya GDP, huku nchi ikipokea zaidi ya watalii milioni 2 kila mwaka.

- Tanzania: Sekta ya huduma bado inakua, ikiwa na mchango wa karibu 40% ya GDP, hasa kupitia utalii na huduma za biashara. Hata hivyo, changamoto zipo:
- Miundombinu duni ya utalii na ukosefu wa masoko ya kimataifa.
- Usimamizi mdogo wa sekta za kifedha.

Uchambuzi: Uwekezaji wa Kenya katika huduma za kifedha na masoko ya kimataifa umeimarisha sekta hii. Tanzania inahitaji kuimarisha miundombinu na kuongeza uzalishaji wa bidhaa za thamani kubwa.

3. Sekta ya Kilimo
- Kenya: Kilimo kinachangia takriban 23% ya GDP, huku Kenya ikiwa moja ya wazalishaji wakubwa wa chai na maua ulimwenguni.
- Bidhaa za kilimo zinaongezwa thamani (value addition) kabla ya kusafirishwa.

- Tanzania: Kilimo kinachangia karibu 25% ya GDP, lakini zaidi ya 65% ya Watanzania wanategemea kilimo cha kujikimu.
- Mazao kama kahawa na korosho yanauzwa yakiwa ghafi, bila kuongezwa thamani.

Uchambuzi: Kenya inazalisha kwa ufanisi zaidi kupitia teknolojia ya kilimo, usimamizi wa maji, na mazao yenye faida kubwa kama maua. Tanzania inapaswa kuwekeza zaidi katika teknolojia za kilimo na usindikaji wa mazao.

4. Biashara ya Kimataifa
- Kenya: Inaongoza katika biashara ya kikanda kutokana na,
- Bandari ya Mombasa, ambayo ni kitovu cha usafirishaji kwa nchi zisizo na bahari kama Uganda na Rwanda.
- Viwanda vikubwa vya bidhaa za kielektroniki, chakula, na plastiki.

- Tanzania: Bandari ya Dar es Salaam inakua kwa kasi, lakini bado inashughulikia shehena ndogo ukilinganisha na Mombasa.
- Tanzania pia inauza nje madini ghafi, jambo linalopunguza thamani ya mauzo yake ya nje.

Uchambuzi: Kenya imejikita katika usafirishaji wa bidhaa zilizo na thamani ya juu, wakati Tanzania bado inategemea bidhaa ghafi.

5. Miundombinu na Nishati
- Kenya:
- Reli ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) imeongeza kasi ya usafirishaji wa bidhaa na watu.
- Uwekezaji mkubwa katika nishati ya upepo na jua umeongeza uzalishaji wa umeme.
- Tanzania:
- Mradi wa Stiegler's Gorge (bwawa la kuzalisha umeme) unatarajiwa kuongeza nishati ya bei nafuu kwa viwanda.
- Hata hivyo, miundombinu ya usafiri wa reli na barabara bado inahitajika kuimarishwa.

Uchambuzi: Kenya imefanikiwa kuunganisha miundombinu na sekta ya biashara, wakati Tanzania bado inasimamia miradi mikubwa inayoweza kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi baadaye.

6. Mazingira ya Uwekezaji
- Kenya: Inaonekana kama kitovu cha uwekezaji Afrika Mashariki kutokana na,
- Soko huria lenye urahisi wa kufanya biashara.
- Makampuni ya kimataifa kama Google, IBM, na Visa yamefungua ofisi zao Nairobi.

- Tanzania:
- Ingawa ina rasilimali nyingi, mabadiliko ya sera za uwekezaji yamekuwa changamoto kwa wawekezaji wa kigeni.

Uchambuzi: Kenya imekuwa mstari wa mbele katika sera rafiki za uwekezaji, wakati Tanzania inahitaji uthabiti wa sera zake ili kuwavutia wawekezaji zaidi.

Ova
Inabidi ifanyike namna hii reply iwe pinned kwenye hii thread pale juu kabisa kila mmoja asome, umetisha b…
 
Me sio mtaalam wa masuala ya uchumi.

Nimetembea baadhi ya maeneo Kenya kwenye harakati za kuusaka mkate maeneo kama Kisii, Migori Mombasa na Nairobi na maeneo mengine kadhaa

Lakini nmegundua Kenya Kuna taabu sana, yaani maisha ni magumu, Wakenya wananuka shida

Miundo mbinu mibovu, Tanzania Lami hadi huko Tandahimba

Kenya Kuna njaa, Wakenya wanaokula sukuma wiki
Kenya Kuna ukame, Tanzania tuna mvua na vyakula bwerere.

Mahitaji muhimu kama chakula, malazi na mavazi Wakenya vinawasumbua

Kwenye kiwanda cha burundani, tumewapiga gap sana
Juzi walikuwa wanalia Kwa Diamond

Tanzania Kwa Sasa wasanii wanafanya vyema kwenye sinema wakenya hata sijui movie zao

CAF wamewanganya uenyeji wa CHAN mwakani, wamewapa Rwanda kwakuwa Kenya hawakuwa na viwanja vyenye viwango, lakini Tanzania viwanja vipo

Harakati za biashara Tanzania ni nyingi mfano tu pale Kariakoo ila Kenya pamepoa mno

Tanzania yenye kila kitu madini, mbuga, Kilimo nk

Utashangaa ukivuka border pale Sirari au Namanga kubadilisha pesa ndo utashangaa
Tunawapa Elfu 1 ya Kenya wanakupa 25,000 ya Tanzania

Yaani pesa kidogo ya Kenya huku unapewa burungutu
Kwenye uchumi kenya wametupita.

Acha niongelee masuala mengine.

1 Kwenye ishu ya maisha kuwa magumu
Nchi zilizo tawaliwa na British zina mfumo tofauti wa maisha.

Kenya wana mfumo tofauti wa maisha sio kama sisi TZ
Wao wana tofauti kubwa kwenye gap kati ya Tajiri na maskini. Ndo maana unasema maskin wa kenya ni fukara kupindukia na tajiri wa huko ana ukwasi kupindukia.

Hii imeletwa na mfumo wao wa maisha tangu enzi za ukoloni. Wale wa kenya waliokua wanafanya kazi kwa wazungu, wengi walipata elimu na pesa za kujikimu na kuanza maisha mapema tofauti na wale waliokuwa raia wa kawaida.
Tofauti na sisi mwalimu alituweka kwenye ujamaa ndo maana tabaka kati ya tajiri na maskini halionekani sana, ni kama wote tupo sawa.

Nazan umeona maisha yao yalivyo tofauti. Bidhaa zao nyiingi wanategemea kununua supermarket kuliko maduka ya mangi kama sisi. Wao hadi unga wa mahindi utaupata supermarket ndo maana utaskia kelele kua bei ya unga imepanda

2
. Ishu nyingine Raia wa kenya kulingana na katiba yao wanamiliki ardhi na serikali haina haki ya kumpangia au kuwanyang'anya ardhi. Tofauti na sisi ambao ardhi ni mali ya serikali na Rais akiamulisha uondeke kwenye ardhi yako basi huna la kusema

3 Wakenya wengi wapo nje ya nchi kwa sababu ya kiingereza wanatafta fursa nje ya mipaka na wanapa fedha huko na kutuma nchini kwao. Sisi walioko nje ya nchi ni wachache na ishu ya lugha inafanya watu wasitafte fursa nje ya mipaka, Tupo wote nchine tunategemea serikal itupe ajira au tujiajiri.

4 Ishu ya Vijana GenZ au wananchi kuishinikizas erikali kufanya wao wanachotaka ni jambo kubwa kwani serikali itakua inawaza mara mbilmbili kabla ya kufanya maamuzi yanayowahusu wananchi.
Ila kwetu TZ serikal ikisha amua hamna wa kuongea, hamna Freedom of speech ya kuzungumza mawazo yako. tena kama yatayolenga kuikosoa serikali ndo hautojulikana ulipo
👇👇👇

Hivyo viwanda vidogo vinatuzidi Nini sisi wenye dhahabu, Tanzanite, Mbuga, kilimo, biashara n.k
Kuwa na pua kubwa sio wingi wa kamasi. Swali ni kwamba wewe mwenye dhahabu au hizo tanzanite kwanini usimzidi huyo asiyekuwa nacho.
 
Me sio mtaalam wa masuala ya uchumi.

Nimetembea baadhi ya maeneo Kenya kwenye harakati za kuusaka mkate maeneo kama Kisii, Migori Mombasa na Nairobi na maeneo mengine kadhaa

Lakini nmegundua Kenya Kuna taabu sana, yaani maisha ni magumu, Wakenya wananuka shida

Miundo mbinu mibovu, Tanzania Lami hadi huko Tandahimba

Kenya Kuna njaa, Wakenya wanaokula sukuma wiki
Kenya Kuna ukame, Tanzania tuna mvua na vyakula bwerere.

Mahitaji muhimu kama chakula, malazi na mavazi Wakenya vinawasumbua

Kwenye kiwanda cha burundani, tumewapiga gap sana
Juzi walikuwa wanalia Kwa Diamond

Tanzania Kwa Sasa wasanii wanafanya vyema kwenye sinema wakenya hata sijui movie zao

CAF wamewanganya uenyeji wa CHAN mwakani, wamewapa Rwanda kwakuwa Kenya hawakuwa na viwanja vyenye viwango, lakini Tanzania viwanja vipo

Harakati za biashara Tanzania ni nyingi mfano tu pale Kariakoo ila Kenya pamepoa mno

Tanzania yenye kila kitu madini, mbuga, Kilimo nk

Utashangaa ukivuka border pale Sirari au Namanga kubadilisha pesa ndo utashangaa
Tunawapa Elfu 1 ya Kenya wanakupa 25,000 ya Tanzania

Yaani pesa kidogo ya Kenya huku unapewa burungutu
Fala ,huna akilli
 
Tz hatuna viwanda kuwazidi,mfano bidhaa za plastics,sufuria Kenya wametuacha mbali sana,tuna import toka huko.....hapa viwanda kama Maxima,Oceans au BGI kwa sufuria na Jambo,Seifi,cello bidhaa hazina ubora ukilinganisha na Kenya....kwahiyo tunawapelekea Dollars nyingi sana
 
Kusema kwl Individual level ya wakazi wa kenya na Tz Wabongo wako mbali sana kwa wakenya, mimi nimezaliwa Sirari Tanzania ambapo ni mpakani Mwa kenya na tz, Kwa bahati nzuri maeneo yote uliyotaja nayajua kwa uzuri na nilishaenda mara kibao, Migori nimeenda kupitia njia ya Isbania Kurya, Mabera, Migori kisii, Nakulu, kisumu na nairobi, kusema kwl wakazi wa kenya wanatia huruma sana ujuaji mwingi kizungu kingi ila njaa ni kubwa sana kwao
 
Kwenye upuuzi tumewazidi,ila kwenye mambo serious hatujawazidi
 
Me sio mtaalam wa masuala ya uchumi.

Nimetembea baadhi ya maeneo Kenya kwenye harakati za kuusaka mkate maeneo kama Kisii, Migori Mombasa na Nairobi na maeneo mengine kadhaa

Lakini nmegundua Kenya Kuna taabu sana, yaani maisha ni magumu, Wakenya wananuka shida

Miundo mbinu mibovu, Tanzania Lami hadi huko Tandahimba

Kenya Kuna njaa, Wakenya wanaokula sukuma wiki
Kenya Kuna ukame, Tanzania tuna mvua na vyakula bwerere.

Mahitaji muhimu kama chakula, malazi na mavazi Wakenya vinawasumbua

Kwenye kiwanda cha burundani, tumewapiga gap sana
Juzi walikuwa wanalia Kwa Diamond

Tanzania Kwa Sasa wasanii wanafanya vyema kwenye sinema wakenya hata sijui movie zao

CAF wamewanganya uenyeji wa CHAN mwakani, wamewapa Rwanda kwakuwa Kenya hawakuwa na viwanja vyenye viwango, lakini Tanzania viwanja vipo

Harakati za biashara Tanzania ni nyingi mfano tu pale Kariakoo ila Kenya pamepoa mno

Tanzania yenye kila kitu madini, mbuga, Kilimo nk

Utashangaa ukivuka border pale Sirari au Namanga kubadilisha pesa ndo utashangaa
Tunawapa Elfu 1 ya Kenya wanakupa 25,000 ya Tanzania

Yaani pesa kidogo ya Kenya huku unapewa burungutu
Kuna GDP na GDP per capital kwenye GDP KENYA wametupita ila kwenye GDP per capital Tumewapita na wametuzidi kwenye deni la taifa.
 
Back
Top Bottom