Misconceptions! Kazi ya elimu si kuajiriwa bali kujiajiri. Hapa napo ndipo hoja ya
JokaKuu inapoanza kupata 'miguu' kwamba, ikiwa tuna resources lakini vijana wa jirani wanaweza kuja na kushamiri , je elimu yetu ipo sawa ?
Hapana! kuna zaidi ya Employement katika Brexit. Unajua Pound Sterling iliendelea hata baada ya Euro
Uingereza ilipewa haki tofauti na za EU hata suala la ajira pia. Yaani UK ilikuwa 'special' katika EU
Wageni waliokwenda UK walitoka Poland. Walikwenda kuchuma matunda, si kazi za maofisini
Ironically, vijana wa UK walikwenda nchi nyingine kupata kazi na hiyo ilikuwa sababu ya upinzani wa Brexit
Walikuwa na advantage ya lugha kwasababu English ilikuwa ni '' Lingua franca''
Hapana, bado wana tatizo hakuna wachuma matunda na mboga na wameanza kwa siri kampango ka kuwaingiza watu wa EU kwa muda na mkataba. Tatizo la ajira za UK lilikuwepo na hilo haliishi kwa Brexit
Kuna short and long-term effects za haya mambo
Ndiyo maana
JokaKuu anauliza mfumo wetu wa elimu upo sawa? Huwezi kuongelea apprentceships bila kuangalia mfumo mzima wa elimu. Kwahiyo unaungana na JokaKuu
Nakubaliana nawe na hasa kuweka siasa nje ya utaalam
1. Si misconceptions bali ni hali halisi. Vijana wanahitaji kuanza kujifanyia shughuli zao wenyewe baada ya kumaliza apprenciteships kinachohitajika ni uwezo wa kupata mitaji ya kuianzisha shughuli zao.
2. Ni kweli kwa Uingereza vijana wengi walikwenda nje lakini moja ya sababu kuu ya nchi hiyo ambayo napenda kuitolea mfano kuondoka kwenye EU ni kutaka kulinda soko lake la ndani la ajira.
Maoni ya wapiga kura wengi yalikuwa ni kukosekana kwa ajira kwa vijana wao ambao walikuwa "priced out" na vijana wa nchi kama Poland, Lithuania na Estonia ambao walikuwa wakilipwa ujira mdogo kulinganisha na ajira ambao wangelipwa vijana wa Uingereza.
Kwa mfano kazi ya kijana ambae ni fundi mchundo au fundi bomba atatoza kiasi kama pauni 120 hadi 150 kwa siku wakati kijana wa Ulaya akija na vifaa vyake atatoza nusu ya tozo hiyo.
Pia kwenye suala la fedha za kujikimu au "benefits" raia wengi wa nchi kama Poland waliweza kuishi hukohuko Poland na kuchukua hizo benefits ambazo zilikuwa processed Uingereza bila kufanyiwa checks na ilikuja kugundulika baadae kuwa waingereza walikuwa wakipigwa vibaya.
Hivyo Boris Johnson akabeba jukumu la kuitoa Uingereza kwenye EU kisha kuhakikisha analinda soko la ajira na kuboresha mishahara khasa ya kima cha chini na kisha kubana masuala ya benefits kwa kuweka restrictions na criterias kwa raia wa kigeni pamoja na kuziunga hizo benefits kuwa universial credits.
Hivyo raia wa kigeni hachukui benefits hadi awe amepiga boksi kama miaka miwili hivi kabla ya kuanza kuvuta mshiko.
Sasa nini kifanyike hatuoni, ndo ngoma za madogoli zilipo hapo watu wacheza tu usiku mchana siasa zapigwa hakuna kinachoonekana.
1. Apprenticeships zipewe kipaumbele na kuwepo ufuatialiaji wa skills muhimu kwa vijana ili waweze kujiajiri na kuanzisha vikampuni vyao wenyewe.
2. Bado hakuna mfumo mzuri wa mishahara ambapo kuna tofauti ya sekta binafsi na sekta ya umma. Kima cha chini cha mshahara chapaswa kuwa ni sheria na ni kwa nchi nzima.
Narudia tena uchumi hukua kwa kasi kutokana na kuwepo mazingira mazuri kama viwanda, miundombinu, teknolojia na mfumo mzuri wa VETA itoe vijana na wawezeshwe kujiajiri.
Mfumo wa elimu ni uleule ulotumiwa na wewe mkuu Nguruvi na mimi na hata Jokakuu, isipokuwa kwa sasa wahitaji uende sambamba na matumizi ya teknolojia.
Teknolojia nnayoizungumzia ni ile inayowawezesha walimu na wanafunzi kujifunza kwa kutumia mbinu na programs za kisasa katika masomo yao.
Tuje siku tuone kijana akimaliza VETA basi anaweza kutumia kompyuta kutengeneza samani za kisasa tangu kubuni kuchora hadi kuunda.
Tatizo ni kuona twaitumia vipi elimu tuipatayo katika mazingira yanayotuzunguka.
Leo hii tusikubali kuagiza samani kutoka China ambao nao hutumia teknolojia kutengeneza samani nzuri kwa ajili ya masoko ya nje.
Tuone viwanda vikitengeneza bidhaa ambazo zoezi zima la kuunda kwake limeanzia kwa kijana aliekaa ofisi kwake akibuni na kutuma tu mchoro kiwandani kwenda kuunda au kutengeneza bidhaa.
Hapo ndipo wenzetu waloendelea walipotushinda.
Nafikiri mtanifahamu hapo wakuu.