Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Hakuna kufungua mipaka,kwao hakuna fulsa,kwetu zipo kibao,tukifungua mipaka,wao ndio watafaidi zaidi.
Nairobi wasomi wamejaa halafu kazi ni chache sana. Sasa wanataka na sisi tuseme "Tunaruhusu Wakenya waje kufanya kazi Tanzania bila vibali vyovyote vile" hahahahaaaa itakula kwetu big time mzee baba.
 
Mkuu, kwani watanzania hakuna katika nchi zingine wanachama wa EAC?

..ninachoona mimi ni kwamba Watz wanatamani kuwa taifa " kilongola " ktk Afrika Mashariki.

..nisichokiona na viongozi wetu kufanyia kazi matamanio ya wananchi wa Tz.

..sioni mipango madhubuti ya kufanya Tz itoke kuwa mzalishaji mkuu wa raw materials za viwandani kwenda kuwa mzalishaji mkuu wa finished products za viwandani.

..sioni mikakati ya kuiboresha elimu ya Tz iwe the best in eac. Sidhani kama mitaala yetu ni ya kisasa kuliko majirani zetu. Sidhani kama tuna invest per student kuzidi majirani zetu.

..Je, majirani zetu wanaitamani elimu ya vyuo vya kati na vyuo vikuu vya Tz? Je, wahitimu wetu wanasakwa na nchi majirani wakawafanyie kazi?

..Naamini niliyaeleza hapo juu yalitakiwa yafanyiwe kazi na serikali za Mzee Mkapa, Mzee Kikwete, na Mzee Magufuli. Naamini viongozi hao, serikali zao, na chama chao, wanastahili lawama kwa yanayoendelea sasa hivi.

NB.

..malalamiko ya Rostam Aziz kule Nairobi yalinisikitisha. Alitakiwa alaumu serikali ya Tz kwa kutoweka mazingira yanayowezesha viwanda kushamiri huku kwetu.

Hakutakiwa alaumu serikali ya Kny. Hakuna Mtz aliipigia kura serikali ya Kny, why should the Kny govt be responsible with Tz industrialization?

Cc Nguruvi3
 
..sioni mipango madhubuti ya kufanya Tz itoke kuwa mzalishaji mkuu wa raw materials za viwandani kwenda kuwa mzalishaji mkuu wa finished products za viwandani.
Mbona viwanda vingi sana vimejengwa wakati wa uongozi wa awamu ya 5?
 
..sioni mikakati ya kuiboresha elimu ya Tz iwe the best in eac. Sidhani kama mitaala yetu ni ya kisasa kuliko majirani zetu. Sidhani kama tuna invest per student kuzidi majirani zetu.
Itapendeza sana kama utatona na mfano kidogo juu ya hili mkuu. Elimu bure ujue sasa hivi?
 
..malalamiko ya Rostam Aziz kule Nairobi yalinisikitisha. Alitakiwa alaumu serikali ya Tz kwa kutoweka mazingira yanayowezesha viwanda kushamiri huku kwetu.
Tayari Rostam alikwisha shamiri Tanzania hivyo akataka kwenda na Kenya akakutana na vizuizi kama vyote.
 
Hakutakiwa alaumu serikali ya Kny. Hakuna Mtz aliipigia kura serikali ya Kny, why should the Kny govt be responsible with Tz industrialization?
Eti unasema "why should the Kny govt be responsible with Tz industrialization" wakati mnapiga kelele kuwa hao ni so-called "ndugu zetu". Huu ndio unafiki ambao mimi siutaki mkuu.
 
..kama tunajiamini kwamba elimu yetu ni nzuri na wahitimu wetu wanaweza kushindana kwanini tunapiga mayowe kila kunapotokea pendekezo la kufungua milango ya ajira ktk EAC?
Kenya sio ndugu zetu. Sisi ndugu zetu ni Uganda
 
..kama tunajiamini kwamba elimu yetu ni nzuri na wahitimu wetu wanaweza kushindana kwanini tunapiga mayowe kila kunapotokea pendekezo la kufungua milango ya ajira ktk EAC?
Uimara wa soko la ajira la ndani na kudhibiti "employment rate" ndio moja ya viashiria kwamba uchumi wakua.

Hivyo wajenga viwanda na kuimarisha miundombinu ili kusaidia kukuza na kuboresha uchumi.

Hatua za kufungua milango ya ajira kwa wengine ilhali vijana wako wanahitimu vyuoni lakini hawana kazi hiyo si dalili nzuri.

Ndo maana nchi za Ulaya kama Uingereza waliona athari ya open door policy na free movements kwamba vilikuwa vikiwafaidisha zaidi raia wa kigeni na vijana wao wakiishi kwa "handouts".

Na tangu Brexit ifanyike Uingereza wameanza kukufaidika kiuchumi zaidi kwa kuwaingiza vijana wao kwenye schems kama apprenticenships ili kuwapatia ujuzi kabla ya hawajaajiriwa.

Sasa suali kwa sisi watanzania je tunazo apprenticeships za kutosha kuwasaidia vijana wanomaliza VETA na vyuo vingine?

Hivyo masuala haya si ya kuyaangalia kwa haraka bali yataka ujuzi wa kuchambua uchumi, sera na mipango ya kuliendeleza taifa lenye vijana na watu wenye welewa wa what is going on.
 
Kenya sio ndugu zetu. Sisi ndugu zetu ni Uganda

..sawa.

..ila usisahau kwamba Uganda hata muuza matembele anaongea Kiingereza.

..hapa Tz Jaji Mkuu analalamika kwamba mawakili wanaoomba usajili hawawezi kuzungumza Kiingereza.

..sasa tusije tukaanza kutafutana siku pendekezo la kufungua milango ya ajira linawekwa mezani.

..Kama kweli tunaipenda nchi yetu basi ni vizuri tukaambiana ukweli.

..Serikali imekuwa ikiwadanganya Watz tangu EAC ianzishwe miaka ya 90.
 
Hatua za kufungua milango ya ajira kwa wengine ilhali vijana wako wanahitimu vyuoni lakini hawana kazi hiyo si dalili nzuri.
Misconceptions! Kazi ya elimu si kuajiriwa bali kujiajiri. Hapa napo ndipo hoja ya JokaKuu inapoanza kupata 'miguu' kwamba, ikiwa tuna resources lakini vijana wa jirani wanaweza kuja na kushamiri , je elimu yetu ipo sawa ?
Ndo maana nchi za Ulaya kama Uingereza waliona athari ya open door policy na free movements kwamba vilikuwa vikiwafaidisha zaidi raia wa kigeni na vijana wao wakiishi kwa "handouts".
Hapana! kuna zaidi ya Employement katika Brexit. Unajua Pound Sterling iliendelea hata baada ya Euro
Uingereza ilipewa haki tofauti na za EU hata suala la ajira pia. Yaani UK ilikuwa 'special' katika EU
Wageni waliokwenda UK walitoka Poland. Walikwenda kuchuma matunda, si kazi za maofisini

Ironically, vijana wa UK walikwenda nchi nyingine kupata kazi na hiyo ilikuwa sababu ya upinzani wa Brexit
Walikuwa na advantage ya lugha kwasababu English ilikuwa ni '' Lingua franca''
Na tangu Brexit ifanyike Uingereza wameanza kukufaidika kiuchumi zaidi kwa kuwaingiza vijana wao kwenye schems kama apprenticenships ili kuwapatia ujuzi kabla ya hawajaajiriwa.
Hapana, bado wana tatizo hakuna wachuma matunda na mboga na wameanza kwa siri kampango ka kuwaingiza watu wa EU kwa muda na mkataba. Tatizo la ajira za UK lilikuwepo na hilo haliishi kwa Brexit
Kuna short and long-term effects za haya mambo
Sasa suali kwa sisi watanzania je tunazo apprenticeships za kutosha kuwasaidia vijana wanomaliza VETA na vyuo vingine?
Ndiyo maana JokaKuu anauliza mfumo wetu wa elimu upo sawa? Huwezi kuongelea apprentceships bila kuangalia mfumo mzima wa elimu. Kwahiyo unaungana na JokaKuu
Hivyo masuala haya si ya kuyaangalia kwa haraka bali yataka ujuzi wa kuchambua uchumi, sera na mipango ya kuliendeleza taifa lenye vijana na watu wenye welewa wa what is going on.
Nakubaliana nawe na hasa kuweka siasa nje ya utaalam
 
..sawa.

..ila usisahau kwamba Uganda hata muuza matembele anaongea Kiingereza

..hapa Tz Jaji Mkuu analalamika kwamba mawakili wanaoomba usajili hawawezi kuzungumza Kiingereza.
Halafu kuna amri ya kutafsiri na kutoa hukumu kwa Kiswahili. Hili nalo ni tatizo
Kiingereza si lugha bora kuliko kisukuma, lakini hatukwepi ukweli kuwa ni 'universal language ' and Lingua franca
Maarifa mengi na utaalam umefichwa katika lugha hiyo.

Wajanja kama India wana lugha zao lakini English ni mandatory. India siyo sisi lakini wamekubali
Kila mahali walipo wanapiga bao. Hivi kuna tatizo gani watu kujua lugha zaidi ya Kiswahili??
..sasa tusije tukaanza kutafutana siku pendekezo la kufungua milango ya ajira linawekwa mezani.
Natamani sana EAC iweke pendekezo hilo
..Kama kweli tunaipenda nchi yetu basi ni vizuri tukaambiana ukweli.
Watu hawataki kusikia ukweli wanataka hoja 'sugar coated'
..Serikali imekuwa ikiwadanganya Watz tangu EAC ianzishwe miaka ya 90.
Na hakuna strategy za kurekebisha hali. Kinachoendelea ni 'protections'
Lazima ifike mahali tuache wageni waje wachangamshe vijana wetu
 
Misconceptions! Kazi ya elimu si kuajiriwa bali kujiajiri. Hapa napo ndipo hoja ya JokaKuu inapoanza kupata 'miguu' kwamba, ikiwa tuna resources lakini vijana wa jirani wanaweza kuja na kushamiri , je elimu yetu ipo sawa ?

Hapana! kuna zaidi ya Employement katika Brexit. Unajua Pound Sterling iliendelea hata baada ya Euro
Uingereza ilipewa haki tofauti na za EU hata suala la ajira pia. Yaani UK ilikuwa 'special' katika EU
Wageni waliokwenda UK walitoka Poland. Walikwenda kuchuma matunda, si kazi za maofisini

Ironically, vijana wa UK walikwenda nchi nyingine kupata kazi na hiyo ilikuwa sababu ya upinzani wa Brexit
Walikuwa na advantage ya lugha kwasababu English ilikuwa ni '' Lingua franca''

Hapana, bado wana tatizo hakuna wachuma matunda na mboga na wameanza kwa siri kampango ka kuwaingiza watu wa EU kwa muda na mkataba. Tatizo la ajira za UK lilikuwepo na hilo haliishi kwa Brexit
Kuna short and long-term effects za haya mambo

Ndiyo maana JokaKuu anauliza mfumo wetu wa elimu upo sawa? Huwezi kuongelea apprentceships bila kuangalia mfumo mzima wa elimu. Kwahiyo unaungana na JokaKuu

Nakubaliana nawe na hasa kuweka siasa nje ya utaalam
1. Si misconceptions bali ni hali halisi. Vijana wanahitaji kuanza kujifanyia shughuli zao wenyewe baada ya kumaliza apprenciteships kinachohitajika ni uwezo wa kupata mitaji ya kuianzisha shughuli zao.

2. Ni kweli kwa Uingereza vijana wengi walikwenda nje lakini moja ya sababu kuu ya nchi hiyo ambayo napenda kuitolea mfano kuondoka kwenye EU ni kutaka kulinda soko lake la ndani la ajira.

Maoni ya wapiga kura wengi yalikuwa ni kukosekana kwa ajira kwa vijana wao ambao walikuwa "priced out" na vijana wa nchi kama Poland, Lithuania na Estonia ambao walikuwa wakilipwa ujira mdogo kulinganisha na ajira ambao wangelipwa vijana wa Uingereza.

Kwa mfano kazi ya kijana ambae ni fundi mchundo au fundi bomba atatoza kiasi kama pauni 120 hadi 150 kwa siku wakati kijana wa Ulaya akija na vifaa vyake atatoza nusu ya tozo hiyo.

Pia kwenye suala la fedha za kujikimu au "benefits" raia wengi wa nchi kama Poland waliweza kuishi hukohuko Poland na kuchukua hizo benefits ambazo zilikuwa processed Uingereza bila kufanyiwa checks na ilikuja kugundulika baadae kuwa waingereza walikuwa wakipigwa vibaya.

Hivyo Boris Johnson akabeba jukumu la kuitoa Uingereza kwenye EU kisha kuhakikisha analinda soko la ajira na kuboresha mishahara khasa ya kima cha chini na kisha kubana masuala ya benefits kwa kuweka restrictions na criterias kwa raia wa kigeni pamoja na kuziunga hizo benefits kuwa universial credits.

Hivyo raia wa kigeni hachukui benefits hadi awe amepiga boksi kama miaka miwili hivi kabla ya kuanza kuvuta mshiko.

Sasa nini kifanyike hatuoni, ndo ngoma za madogoli zilipo hapo watu wacheza tu usiku mchana siasa zapigwa hakuna kinachoonekana.

1. Apprenticeships zipewe kipaumbele na kuwepo ufuatialiaji wa skills muhimu kwa vijana ili waweze kujiajiri na kuanzisha vikampuni vyao wenyewe.

2. Bado hakuna mfumo mzuri wa mishahara ambapo kuna tofauti ya sekta binafsi na sekta ya umma. Kima cha chini cha mshahara chapaswa kuwa ni sheria na ni kwa nchi nzima.

Narudia tena uchumi hukua kwa kasi kutokana na kuwepo mazingira mazuri kama viwanda, miundombinu, teknolojia na mfumo mzuri wa VETA itoe vijana na wawezeshwe kujiajiri.

Mfumo wa elimu ni uleule ulotumiwa na wewe mkuu Nguruvi na mimi na hata Jokakuu, isipokuwa kwa sasa wahitaji uende sambamba na matumizi ya teknolojia.

Teknolojia nnayoizungumzia ni ile inayowawezesha walimu na wanafunzi kujifunza kwa kutumia mbinu na programs za kisasa katika masomo yao.

Tuje siku tuone kijana akimaliza VETA basi anaweza kutumia kompyuta kutengeneza samani za kisasa tangu kubuni kuchora hadi kuunda.

Tatizo ni kuona twaitumia vipi elimu tuipatayo katika mazingira yanayotuzunguka.

Leo hii tusikubali kuagiza samani kutoka China ambao nao hutumia teknolojia kutengeneza samani nzuri kwa ajili ya masoko ya nje.

Tuone viwanda vikitengeneza bidhaa ambazo zoezi zima la kuunda kwake limeanzia kwa kijana aliekaa ofisi kwake akibuni na kutuma tu mchoro kiwandani kwenda kuunda au kutengeneza bidhaa.

Hapo ndipo wenzetu waloendelea walipotushinda.

Nafikiri mtanifahamu hapo wakuu.
 
Kuwepo kwao na manufaa wanayopata ni vitu viwili tofauti...Compare makampuni zaidi ya 500 vs 30 equity ipo wapi hapo?
Alichokisema JokaKuu ni kuwa;

"miaka 25 ya kuwa wanachama wa eac ninaamini ilikuwa inatosha kabisa kuwaandaa wananchi wetu kuweza kuishi popote"

Kwa hiyo kinachojadiliwa hapa ni watu na sio makampuni.
 
..ila usisahau kwamba Uganda hata muuza matembele anaongea Kiingereza.

..hapa Tz Jaji Mkuu analalamika kwamba mawakili wanaoomba usajili hawawezi kuzungumza Kiingereza.
Hakuna graduate wa Tanzania asiyeweza kuzungumza kiingereza. Sema watu kama nyie mnaona mtu mwenye swagger za american english kuwa ndiye msomi na mbobezi wa lugha ya malkia.
 
..nadhani tunakosea sana kuwakweza TISS na kukabidhi maisha yetu mikononi mwao.

..suala la viwanda kufa au kustawi linategemeana na mazingira ya kibiashara yaliyoko Tz.

Unajua wewe jamaa kuna vitu vingi sana hujui ila unajikuta mjuaji sana. Suala la kufa na kustawi inategemea mazingira peke yake? You mean people can't influence things, you mean hata hizo hujuma za USA kwa China ni mazingira ya China ndio yanaua Huawei, hakuna external influences.
Mahn, shut your mouth sumtyms and learn
 
Back
Top Bottom