Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Kijana 254 nakuona unatetea nchi yako
Haha, mkuu, ni kweli lakini nampa vitu real huyo, ka hela hana, alafu anatarajia mambo yanyooke, urongo huo. Sahi kisomo kinaambatana na hela + connection. Bila hivyo, atabaki kulia lia tu wakati ndugu zake wanapiga kazi za kishua huku.
 
Uo ujasusi kwani Tanzania imezuiwa kuwafanyia Kenya ?

Fanyeni kazi vijana mpate pesa tuache kulia lia


Mambo ya kufanyiwa ujasusi mbona ni ya kawaida tu hata sisi kwani hatufanyi ujasusi kwa Kenya?

Na nchi zote za maziwa makuu? Acheni utoto.
 
Uo ujasusi kwani Tanzania imezuiwa kuwafanyia Kenya ?

Fanyeni kazi vijana mpate pesa tuache kulia lia


Mambo ya kufanyiwa ujasusi mbona ni ya kawaida tu hata sisi kwani hatufanyi ujasusi kwa Kenya?

Na nchi zote za maziwa makuu? Acheni utoto.
Kwanza unatakiwa kujifunza kwa aliyekutangulia kuliko kung'ang'ana na Burundi
 
Huu ndio ukweli.
 
Tatizo watz maskini wa mawazo Fursa zimefunguliwa Kenya na tz utaona wenzetu watavyochangamkia Fursa sisi tutaanza kuvaa fulana za cccm nakuanza kulaumu wakenya wanachukua Fursa zetu ujinga.
 
Akikujibu nami niite nisome ccm imeharibu akili za matz mengi.
 
Mkwamo wetu hapa ndipo ulipo

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Sisi ni watu wa visingizio tu. Na tutabakia hapa hapa na umasikini wetu kama tukiendelea kudhania umasikini wetu unasababishwa na watu wengine na sio sisi wenyewe!

Yaani tunafikiri tukiwazuia Kenya kuendelea ndio sisi tutaendelea? Yaani tulikuwa tayari nafasi ya MD wa Voda apewe mmisri kuliko mkenya! Roho mbaya tu. Tumefaidikaje? Voda kampuni ya UK/SA.....Kenya haina incentive ya kuiua na kwa kweli haiwezi kuiua.....ni service industry..... ikifa Voda wateja hawahamii Safaricom.....sanasana watahamia Tigo, Airtel, TTCL nk. Stupidity at it's best!

Inanikumbusha ile stori ya jamaa aliyeambiwa na "mungu" aombe kitu kimoja kwa sharti kwamba chochote atakachoomba atapewa lakini nduguye atapewa mara mbili yake! Jamaa alivyo na roho mbaya akaomba atobolewe jicho moja.....! (Ili nduguye awe kipofu kabisa).
 
..nadhani tunakosea sana kuwakweza TISS na kukabidhi maisha yetu mikononi mwao.

..suala la viwanda kufa au kustawi linategemeana na mazingira ya kibiashara yaliyoko Tz.
Mkuu tatizo letu ni moja,sisi kazi ya usalama wa taifa ni kuwawinda wapinzani na kuwapoteza, imagine akina bashite ndio walikuwa viongozi wao wa kupanga misheni,
Wakati wenzetu wanaangalia fulsa na kuzinyakua ,
Usalama wanamlinda mtu kwa maslahi yake wanaacha nchi na uchumi unakimbiziwa nje ya nchi,
Na shida nyingine wakajigeuza wambea wa kuchunguza wananchi wenye hela na kuwanyang'anya, ili kunusuru mitaji watu wakaangalia wapi hakuna wanyang'anyi wakakimbilia huko,
Wakati huo huku tunaimbishwa wimbo wa wanyonge
 
sema huyo alikuwa mbongo tuu hahaha
 

..Looh!!

..Wafanyabiashara ndio hao wamenyang'a nywa fedha.

..Maana yake hawana mitaji ya kushindana na Wakenya.

..Vijana nao wanaambiwa wasijifunze Kiingereza watakuwa watumwa na ni kukosa uzalendo.

..Maana yake huyu kijana akienda kwenye usaili wa kampuni ya wawekezaji wanaotoka nje atashindwa kupata kazi.

..Tunalalamika elimu yetu ni ya nadharia. Na juu ya hilo tunawalemaza vijana kwa kuwanyima communication skills.

..Tunawafanya vijana wetu wasiweze kushindana ktk soko la ajira la Afrika Mashariki. Tumesalimu amri kabla hata mchezo haujaanza.
 
Mazingira mkuu yanachangia sn
Kwani huyu mama umemuona na kasoro gani....ndo nyie muliokua mnamshabikia mwendazake kwasabb anatesa nakufunga matajiri wakati anaua uchumi....huyu mama ameanza kurekebisha mmeanza dharau zenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…