Wakuu twende mbele turudi nyuma, nchi ya Kenya imeitupa Tanzania mbali sana kimaendeleo. Nakiri sijawahi kufika Kenya, lakini nimekuwa mfuatiliaji sana wa mafanikio ya wenzetu kupitia kupitia Luninga na hasahasa Google Earth ambayo inaweza kukupeleka popote pale na kukuonesha mandhari mbalimbali duniani.
Nchi ya Kenya eneo lake kubwa ni Jangwa kama ionekavyo hapo chini ukifananisha na Tanzania. Pia eneo lake ni dogo ukilinganisha na Tanzania.
Sijaainisha ni maendeleo gani wametupita ila karibu nyanja zote utakazozifikiria wewe wao wapo mbele yetu.
Sisi Tz tunakwama wapi?
~ Je, ni historia ndio iliyoturudisha nyuma?
~ Je, ni mfumo wa Elimu?
~ Je, ni wanasiasa?
Shida ni nini hasa? Au sisi ni wavivu kufanya kazi? Nchi yetu imebarikiwa kila rasli mali, mito mingi, maziwa yametuzunguka, bahari, mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro, madini mbalimbali... Tufanye nini kuisaidia nchi yetu kusonga mbele?
Nimewiwa tu kuandika hivi nikiamini wapo wajuvi humu ndani na tunaweza kujadili pamoja.
Mungu ibariki Tanzania.