Kenya imeiacha Tanzania parefu sana kimaendeleo, shida ni nini?

Njoo uwe mwenzetu huku Kenya
Kama mtu wa kupiga soga kama hivi huwezi kuelewa Kenya walivyotuzidi.
Unaijua paypal? Kenya wanatuma na kupokea pesa kutoka paypal. Mtandaoni kuna fursa nyingi sana tunazikosa.
Kuna makampuni yanalipa kwa Paypal na Payoneer. Mfumo wa paypal ni rahisi unaingia kwenye simu moja kwa moja.
Wakati mwingine huwa natamani hata ningekuwa mkenya.
 
..Kenya walikuwa wametuacha kimaendeleo hata kabla ya vita vya Kagera.

..kumbuka Tanzania tulivyohangaika kuanzisha viwanda mara baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika kwasababu tulikuwa tukitegemea bidhaa toka Kenya.
Mkapa alipiga kazi tukaiacha Kenya kwa GDP,akaingia kibaki kule,mchumi,akafanya alofanya tumeachwa mpaka kesho
 
..Tujitahidi kuboresha kilimo na ufugaji tutakuwa ktk nafasi nzuri ya ushindani.

..Kenya wanazalisha maziwa mengi kuliko Tanzania wakati sisi tuna ng'ombe wengi kuliko wao.
 
Nyerere alifukuza wazungu na kutuachia Kiswahili na kingereza chakuibia ibia kuanzia darasa la tatu- la saba, kisha form one tunaanza kuhangaika nacho kama mgawo wa umeme wa sasa pia tulibaki na wahindi pale kariakooni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tulikua na nafasi ya kuendelea kutumia English kama Lugha ya kufundishia. Leo hii kingekua kimetufungulia fursa nyingi sana nje. Wa Tz wapo wengi nje lakini wapo kimya sana tofauti na wenzetu wakenya au ugandans ambao wanaweza kujieleza vizuri kwa Lugha hiyo.
Watawala wameona Kiswahili kiendelee kutumika kufundishia mashuleni lakini watoto wao wanasoma English meadium schools na International schools
 
Yaani hapo kwakweli hata mie sitaacha kuwalaumu, nakumbuka tunaanza darasa la kwanza tuna rafudhi ya kiruga lakini tukafundishwa na kuelewa vizuri tena mwezi tu, kwanini asingekiacha tukaanza nacho tukiwa bado vichwa vinanasa vyema? Baba kwa hapo mmm hapana kwa watoto wamafukara inatesa sana. Wahindi wenyewe tupo nao humu halafu eti Kiswahili hawakijui ila mzungu au mchina akija siku 2 tu tunaongea naye kiswahili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi,unayegemea akili akili kama hizi zitaleta maendeleo Tanzania 🇹🇿?

20221217_102353.jpg
 
Wakuu twende mbele turudi nyuma, nchi ya Kenya imeitupa Tanzania mbali sana kimaendeleo. Nakiri sijawahi kufika Kenya, lakini nimekua mfuatiliaji sana wa mafanikio ya wenzetu kupitia kupitia Luninga na hasahasa Google Earth ambayo inaweza kukupeleka popote pale na kukuonesha mandhari mbalimbali duniani.
Nchi ya Kenya eneo lake kubwa ni Jangwa kama ionekavyo hapo chini ukifananisha na Tanzania. Pia eneo lake ni dogo ukilinganisha na Tanzania.
Sijaainisha ni maendeleo gani wametupita ila karibu nyanja zote utakazozifikiria wewe wao wapo mbele yetu.
Sisi Tz tunakwama wapi?
Je ni historia ndio iliyoturudisha nyuma?
Je ni mfumo wa Elimu?
Je ni wanasiasa?
Shida ni nini hasa? Au sisi ni wavivu kufanya kazi? Nchi yetu imebarikiwa kila rasli mali, mito mingi, maziwa yametuzunguka, bahari, mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro, madini mbalimbali....
Tufanye nini kuisaidia nchi yetu kusonga mbele?
Nimewiwa tu kuandika hivi nikiamini wapo wajuvi humu ndani na tunaweza kujadili pamoja.

Mungu ibariki Tanzania. View attachment 2456941

Swala la uchumi baina ya nchi za africa ya mashariki kwa kiasi kikubwa linamizizi ya ukoloni. Tutambue tu nchi yetu kwanza ilitawaliwa na mjerumani na baadae mwingereza km mwangalizi wa muda.

Kupitia wakoloni wa kiingereza kenya hasa nairobi ilijengwa sana na kufanywa km ndio makao makuu ya Africa mashariki huku tanganyika ikibaki km mashamba tu kwanza haikuwa mali ya mwingereza hivyo alijihusisha sehemu ndogo kwenye uchumi. (Gap la kwanza la uchumi likatokea hapo)

Maisha baada ya uhuru kwa nchi zote mbili pia yalikuwa na miundo tofauti sana hasa tanganyika tuliamua kufuata mfumo wa kijamaa na kenya wao waliendelea na ubepari. Mwanzoni ufumo wa kijamaa kwa tanganyika ulionekani mfumo sahihi sana maan uliweza kukuza uchumi kwa speed hadi miaka ya 77 nchi ilianza kujikuta kweny matatizo ya vita na kudondoka kwa ujamaa duniani hali hii ilipelekea nchi za kijamaa tulizokuwa tunazitegemea kusitisha misaada hali ikawa mbaya sana hivyo tukageukia ubepari kwa mashart magumu sana tukapewa mikopo.
(Gap la pili likatokea hapo)

Kufikia miaka ya 1995 nchi yetu ilikuwa hoi bin taaban kiuchumi inshort ilifilisika na ikaorodheshwa miongoni mwa nchi masikini zenye mzigo mkubwa wa madeni
Tukasamehewa na kuanza upya tena.

Baada ya kurudia ubepari tena toka uhuru jitihada mbalimbali zimefanywa na viongozi kwa kadri walivyoweza kuunyanyua uchumi tena ambao ulikuwa umeshakufaaa.

Hivi tunavyoongea tz ni miongoni mwa nchi 10 zenye uchumi mkubwa afrika kati ya nchi 54 sisi tukiwa namba 9 huku 8 akiwa Ethiopian na 7 kenya. U can imagine from down huko to top ten.

Maana yk ni kuwa tz inaendelea kwa speed sana kuliko kenya maan kenya hawajawahi kupata misukosuko ya kiuchumi km tz wala hawajawah kubadili mifumo ya uchumi ya nchi yao toka uhuru.
Achilia mbali wao walirithi nchi ikiwa na kila kitu teyar miundombinu ya kutosha, viwanda, man labour ya kutosha sisi hivyo vyote tulivisikia kwenye bomba na ilitubidi tuvijenge wenyewe maan tulichorithi ni reli na barabara ndogo ya rami.

Bongo kazi inapigwa sana ingawa pia baadhi ya viongozi wetu wanaturudisha nyuma ila kazi imepigwa haswa..
 
Umedadavua kisomi! Atleast naanza kuelewa wapi tulijikwaa
 
Wakenya ni wapambanaji wakubwa (Hustlers) wametapakaa kila pembe ya dunia kusaka fursa pia wanapeana sapoti wao kwa wao kwenda ughaibuni kusaka fursa na demokrasia yao ipo vizuri hasa sera ya kuruhusu Uraia pacha kwa raia wake.

Hii inawasaidia watu kwenda nje kutafuta ujuzi, Ajira na "in return" fedha wanazopata kama Diaspora zinachangia ukuaji wa uchumi

Pia Kenya wana mfumo mzuri wa Elimu na katiba yao pia ni nzuri.

Njoo bongo sasa Kupata pasipoti ya kusafiria tu hadi uzungushwe weeeehh!!! Utoe Rushwa weeeh! Uhojiwe maswali ya kijinga! Uambiwe mara leta barua ya uthibitisho uendako,mara barua ya Afisa mtendaji, Mara wakwambie majina yako kwenye vyeti hayafanani!!???? Process kibao!

Tz bado ina wajinga wengi sana na sera za kijinga na kipumbavu za Uchawa na kusifia ujinga wa viongozi wao.

Tanzania is doomed to remain poor!!!
Umerenga mkuki pahala pake. Kukazia ni uongozi bora au siasa safi imekosekana. Waliopo wanaimizana kula kwa urefu wa kamba zao huku wakiongeza kamba ziwe ndefu wale zaidi. Mfano halisi ni uongezaji idadi ya wajumbe kwenye Nec yao ccm, kuna ulazima gani!
 
..tatizo la Watanzanio sio kutokufanya kazi kwa bidii.

..we work as hard as Kenyans, if not harder.

..tofauti kati yetu, na haswa nikiangazia kilimo na ufugaji, ni kutokutumia maarifa na utaalamu wa kisasi.

..ukitaka kulitambua hilo angalia jinsi Wakenya wanavyolima na kufuga ulinganishe na Watanzania.

..Majirani na ndugu zetu wa Kenya wanatumia mbegu bora iwe kwenye kilimo au ufugaji, na mbinu zao ni za kisasa.
Still Kenya inategemea chakula kutoka tz kwa silimia nyingi sana
 
Kagera War (1978-1979)

Waakanzia kutupiga gape hapo.
Kisa vita ya kidini (Mkatoliki Nyerere vs Muislamu Amin)
Hapo umepuyanga yaani kabla ya vita gap lilikuwa kubwa sana kushinda sasa
 
..tatizo la Watanzanio sio kutokufanya kazi kwa bidii.

..we work as hard as Kenyans, if not harder.

..tofauti kati yetu, na haswa nikiangazia kilimo na ufugaji, ni kutokutumia maarifa na utaalamu wa kisasi.

..ukitaka kulitambua hilo angalia jinsi Wakenya wanavyolima na kufuga ulinganishe na Watanzania.

..Majirani na ndugu zetu wa Kenya wanatumia mbegu bora iwe kwenye kilimo au ufugaji, na mbinu zao ni za kisasa.
Halafu tunawalisha
 
Wakenya ni wapambanaji wakubwa (Hustlers) wametapakaa kila pembe ya dunia kusaka fursa pia wanapeana sapoti wao kwa wao kwenda ughaibuni kusaka fursa na demokrasia yao ipo vizuri hasa sera ya kuruhusu Uraia pacha kwa raia wake.

Hii inawasaidia watu kwenda nje kutafuta ujuzi, Ajira na "in return" fedha wanazopata kama Diaspora zinachangia ukuaji wa uchumi

Pia Kenya wana mfumo mzuri wa Elimu na katiba yao pia ni nzuri.

Njoo bongo sasa Kupata pasipoti ya kusafiria tu hadi uzungushwe weeeehh!!! Utoe Rushwa weeeh! Uhojiwe maswali ya kijinga! Uambiwe mara leta barua ya uthibitisho uendako,mara barua ya Afisa mtendaji, Mara wakwambie majina yako kwenye vyeti hayafanani!!???? Process kibao!

Tz bado ina wajinga wengi sana na sera za kijinga na kipumbavu za Uchawa na kusifia ujinga wa viongozi wao.

Tanzania is doomed to remain poor!!!
Umemaliza yote mkuu
 
..Tujitahidi kuboresha kilimo na ufugaji tutakuwa ktk nafasi nzuri ya ushindani.

..Kenya wanazalisha maziwa mengi kuliko Tanzania wakati sisi tuna ng'ombe wengi kuliko wao.
Siku hizi ndiyo tunarasimisha shughuli,huko nyuma palikua na wakulima na wafanyakazi,maana kilimo si kazi!
 
Back
Top Bottom