Kenya imeiacha Tanzania parefu sana kimaendeleo, shida ni nini?

Wakuu twende mbele turudi nyuma, nchi ya Kenya imeitupa Tanzania mbali sana kimaendeleo. Nakiri sijawahi kufika Kenya, lakini nimekuwa mfuatiliaji sana wa mafanikio ya wenzetu kupitia kupitia Luninga na hasahasa Google Earth ambayo inaweza kukupeleka popote pale na kukuonesha mandhari mbalimbali duniani.

Nchi ya Kenya eneo lake kubwa ni Jangwa kama ionekavyo hapo chini ukifananisha na Tanzania. Pia eneo lake ni dogo ukilinganisha na Tanzania.

Sijaainisha ni maendeleo gani wametupita ila karibu nyanja zote utakazozifikiria wewe wao wapo mbele yetu.
Sisi Tz tunakwama wapi?
~ Je, ni historia ndio iliyoturudisha nyuma?
~ Je, ni mfumo wa Elimu?
~ Je, ni wanasiasa?

Shida ni nini hasa? Au sisi ni wavivu kufanya kazi? Nchi yetu imebarikiwa kila rasli mali, mito mingi, maziwa yametuzunguka, bahari, mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro, madini mbalimbali... Tufanye nini kuisaidia nchi yetu kusonga mbele?

Nimewiwa tu kuandika hivi nikiamini wapo wajuvi humu ndani na tunaweza kujadili pamoja.

Mungu ibariki Tanzania.

View attachment 2456941
Ukubwa tuu wa eneo la Tzn tayari Ni changamoto tosha
 
Wakenya ni wapambanaji wakubwa (Hustlers) wametapakaa kila pembe ya dunia kusaka fursa pia wanapeana sapoti wao kwa wao kwenda ughaibuni kusaka fursa na demokrasia yao ipo vizuri hasa sera ya kuruhusu Uraia pacha kwa raia wake.

Hii inawasaidia watu kwenda nje kutafuta ujuzi, Ajira na "in return" fedha wanazopata kama Diaspora zinachangia ukuaji wa uchumi

Pia Kenya wana mfumo mzuri wa Elimu na katiba yao pia ni nzuri.

Njoo bongo sasa Kupata pasipoti ya kusafiria tu hadi uzungushwe weeeehh!!! Utoe Rushwa weeeh! Uhojiwe maswali ya kijinga! Uambiwe mara leta barua ya uthibitisho uendako,mara barua ya Afisa mtendaji, Mara wakwambie majina yako kwenye vyeti hayafanani!!???? Process kibao!

Tz bado ina wajinga wengi sana na sera za kijinga na kipumbavu za Uchawa na kusifia ujinga wa viongozi wao.

Tanzania is doomed to remain poor!!!
Lugha imechangia
 
Uchumi wa Tz upo Top ten ila uchumi wa Kenya ni mkubwa karibia mara 2 ya wa Tanzania. Uchumi wa Kenya ni mkubwa sawa ukilinganisha na nchi za zamani za Africa Mashariki kwa pamoja (Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi).
Usijisifie umekuwa wa pili darasani ukiwa na D wakati aliyekutangulia ana B+
Hilo haliondoi ukweli kuwa Tanzania nado inafanya vizuri sana hasa tukiangalia background za nchi zote toka uhuru
Screenshot_20221225-082356_Chrome.jpg
 
Kagera War (1978-1979)

Waakanzia kutupiga gape hapo.
Kisa vita ya kidini (Mkatoliki Nyerere vs Muislamu Amin)
Kenya ilikuwa mbele kimaendeleo kwasababu wakoloni UK walijenga viwanda wakati huku Tanganyika hapakuwa na viwanda ukilinganisha na Kenya.

Sababu ya Vita ya Kagera haikuwa dini hata kidogo hizo zilikuwa siasa za misikitini zilizoasisiwa na Masheikh nja.

Sababu kubwa ni urafiki baina ya Mwl Nyerere na rafiki yake Milton Obote.Kwakuwa katiba yetu ilimpatia madaraka makubwa sana Rais ilikuwa ni rahisi Mwl Nyerere kutuingiza katika Vita isiyokuwa na faida yoyote.

Ni Mwl Nyerere huyo huyo aliyetumia fedha zetu nyingi kukomboa nchi za kusini dhidi ya ukoloni na ubaghuzi wa rangi.Hili nalo utasema ni udini ?.

Mwl Nyerere alitukomboa kutoka ukoloni wa Mwingereza akatunia katiba ile ile kujigeuza mkoloni mweusi mpaka leo katiba aliyoshiriki kuitengeneza inatutesa.
 
Wakenya ni wapambanaji wakubwa (Hustlers) wametapakaa kila pembe ya dunia kusaka fursa pia wanapeana sapoti wao kwa wao kwenda ughaibuni kusaka fursa na demokrasia yao ipo vizuri hasa sera ya kuruhusu Uraia pacha kwa raia wake.

Hii inawasaidia watu kwenda nje kutafuta ujuzi, Ajira na "in return" fedha wanazopata kama Diaspora zinachangia ukuaji wa uchumi

Pia Kenya wana mfumo mzuri wa Elimu na katiba yao pia ni nzuri.

Njoo bongo sasa Kupata pasipoti ya kusafiria tu hadi uzungushwe weeeehh!!! Utoe Rushwa weeeh! Uhojiwe maswali ya kijinga! Uambiwe mara leta barua ya uthibitisho uendako,mara barua ya Afisa mtendaji, Mara wakwambie majina yako kwenye vyeti hayafanani!!???? Process kibao!

Tz bado ina wajinga wengi sana na sera za kijinga na kipumbavu za Uchawa na kusifia ujinga wa viongozi wao.

Tanzania is doomed to remain poor!!!
Ni kweli remmitance zinasaidia sana kukuza uchumi wa Kenya....

Sisi huku hata mfumo wa Paypal hauruhusiwi...

Sisi wenyew ndo tunajifanya maskini....ukipata fursa ya kwenda nje hasa kama una professional nenda aisee...vinginevyo utakufa maskin
 
Tusidanganyane, Kunyaland Kuna maisha magumu na ya hovyo Sana na tatizo kubwa Ni income disparity baina ya wenye nacho na mafukara..

Kenyans wengi Wana survive Ila hawaishi
 
Sijaainisha ni maendeleo gani wametupita ila karibu nyanja zote utakazozifikiria wewe wao wapo mbele yetu.
Sisi Tz tunakwama wapi?
~ Je, ni historia ndio iliyoturudisha nyuma?
~ Je, ni mfumo wa Elimu?
~ Je, ni wanasiasa?

Shida ni nini hasa? Au sisi ni wavivu kufanya kazi? Nchi yetu imebarikiwa kila rasli mali, mito mingi, maziwa yametuzunguka, bahari, mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro, madini mbalimbali... Tufanye nini kuisaidia nchi yetu kusonga mbele?
Walitupiga wakati wa kuvunja EAC mwaka 1977
 
Mtoa mada nahisi uwenda huijui Kenya kwa marefu na mapana,sijajua labda unazungumzia kenya inatuzidi nini sisi Tanzania,nafikiri kama ungekuwa specific ingekuwa bora sana lakini ngoja nikutoe tongotongo mkuu…….

Mimi ni mjaluo au mluo,ninaenda sana kenya kuliko maelezo ata sasa nipo kenya kula x-mass..

Kenya ni nchi ya kibepari tena ule ulio kolea ukimkuta tajiri kenya jua ni tajiri kweli lakni pia ukimkuta maskini kenya jua ni maskini kweli,kiufupi Kenya wana maskini wengi sana kuliko Tanzania kwa kipato cha mmoja mmoja ata ukienda kwenye levels za matajiri,kenya hawana Billionaires kama wabongo TZ tuna billionaires wengi sana kuliko kenya (kama huamini nitakuelewesha kwa ushahidi)

Kwenye miundombinu wenzetu walianza kujenga flyovers,barabara ata njia za ndege toka kitambo sana tena nyingi vimefanywa na Wazungu sio wakenya ndio maana kuna barabara nyingi za kulipia lakini kitu ambacho huwez kukikuta TZ…Kiufupi Kenya uchumi unajengwa na wazungu na watu wa Asia sio wakenya,mfano mzuri ni Kenya airways juzi imefilisika na serikali ameuza hisa zake zote kwa mzungu

Kenya ni taifa linalo mtegemea sana mzungu kuliko chochote na wanakopa kweli kweli lakini wana ufisadi wa kutisha huku ata choo cha shule kinatafutiwa pesa za mkopo ili waweze kupga pesa

Ata hii GDP yao ya 100+B$ ni ya kutengenezwa kumbuka hii nchi ni kibaraka mkubwa wa mzungu(nikipata muda nitakuelezea vizuri kabisa)

Kiufupi,Kenya na Tanzania hakuna tofauti kubwa yoyote na bora Tanzania kuliko Kenya ndio maana ata wakenya wenyewe hawapendi nchi Yao wanaikubali Bongo kuliko maelezo na ndoto ya vijana wengi wa huku Nyanza na Mombasa wanapenda sana kuja bongo(kama ambavyo vijana wetu wanavyo penda kwenda SAUZI)

Kuna vingi nataman nikuweke sawa ila ngoja nikuachie hapa maana ninawahi Ibadani nikipata muda nitakuelezea Kinaga ubaga
 
1. Katiba yenu ni mbovu inakiuka sheria za natural justice mtu anaweza kaa jela without trial for a long time.
2. Mfumo wenu wa kibiashara to foreign investors kidogo unaweka vikwazo ambavyo nchi inayojaribu kuwa competitive haifai kuwa nazo. Mfano work permit ni ngumu kupata na tena very expensive. The world is now a global village wacheni kuji-isolate.

3. Foreigners can't own land unless for investments above $500,000. Land is a basic factor of production. Na hata ukiwa na iyo $500,000 lazima ungoje iyo process ikamiliki for more than 1 yr. Yaani mnataka investor angoje for that long?

4. Too many centers of power with unpredictable policies. Mara kwa mara huwa ninaona ma Regional commissioners in Tanzania wakiwaingilia investors hadharani ili kufurahisha wananchi na pia enforcing policies ambazo kana kwamba they are revenging against investors. Kutokuwa na katiba inayotoa ulinzi kwa investors haisaidii.

5. Kiswahili. Nyerere was very wise to teach you swahili ili kuunganisha makabila tofauti ya Tanzania but the effect of that too was to isolate you from mfumo wa globalisation ambao ndio ulikuwa unaenea kote duniani from the 1980's. Ukweli ni kwamba languages kama English ndio global languages, I can't imagine a Tanzanian youth trying to learning coding ili ajihusishe kwa hii dunia ya artificial intelligence yet their primary language ni kiswahili. Iyo inafanya mambo yake kuwa magumu sana.

6. Policy enforcers wenu are loyal to the president not constitution. Of course Kenya to some extent tuko hivyo but the amount of bootlicking in Tanzania is mind-boggling. Hii nafikiri explains ile point yangu ya policies kukuwa unpredictable.

7. Watanzania ni ngumu sana kukosa chakula kwa hivyo hamjihusishi sana na biashara kubwa kubwa. I cannot believe that kule mikoa ya Iringa mtu anaweza akanunua eka moja ya shamba na $100. Na hata sehemu za morogoro I saw sijui $400.
8. Remittances from Tanzanians living abroad ziko chini sana.

Bila hivyo vikwazo nimetaja hapo, Tanzania would be the largest economy in East Africa. Sioni vile Kenya tungewafikia. You guys can feed yourselves na bado mko na mashamba makubwa sana yako idle. Mko na natural resources ambazo sisi hatuna. Barabara na infrastructure mnazidi kujenga. Umeme mnazidi ku invest katika iyo sekta.

Having said that, Tanzania is the most beautiful country in East Africa. Mko na ecosystems mbalimbali na natural beauty mzuri sana. I still don't think you have explored your potential in Tourism that much.

One notable observation that I have made about TZ ni kuwa if a person is upper middle class na kuendelea in Tanzania then they are rich rich hakuna kubahatisha. While huku kenya mtu anaweza kuwa hivyo lakini kuna cycles ambazo anashukashuka na kupanda. But in Tanzania if you are rich, you are rich. It looks like upward mobility in Tanzania ni ngumu sana kwa wale wako chini.

Tanzania,kama una pesa is the best country to live in hapo hata mimi ninakubali. Middle class yenu niko sure they enjoy sana, kama vile middle class ya south africa does.
 
Kenya kuna maskini sana kiasi gani na Tanzania kuna maskini sana kiasi gani?
Weka idadi au aslimia badala ya maneno matupu.

Halafu China ina mabilonea wengi sana kuliko Marekani lakini inazidiwa sana kiuchumi na Marekani.
Mtoa mada nahisi uwenda huijui Kenya kwa marefu na mapana,sijajua labda unazungumzia kenya inatuzidi nini sisi Tanzania,nafikiri kama ungekuwa specific ingekuwa bora sana lakini ngoja nikutoe tongotongo mkuu…….

Mimi ni mjaluo au mluo,ninaenda sana kenya kuliko maelezo ata sasa nipo kenya kula x-mass..

Kenya ni nchi ya kibepari tena ule ulio kolea ukimkuta tajiri kenya jua ni tajiri kweli lakni pia ukimkuta maskini kenya jua ni maskini kweli,kiufupi Kenya wana maskini wengi sana kuliko Tanzania kwa kipato cha mmoja mmoja ata ukienda kwenye levels za matajiri,kenya hawana Billionaires kama wabongo TZ tuna billionaires wengi sana kuliko kenya (kama huamini nitakuelewesha kwa ushahidi)

Kwenye miundombinu wenzetu walianza kujenga flyovers,barabara ata njia za ndege toka kitambo sana tena nyingi vimefanywa na Wazungu sio wakenya ndio maana kuna barabara nyingi za kulipia lakini kitu ambacho huwez kukikuta TZ…Kiufupi Kenya uchumi unajengwa na wazungu na watu wa Asia sio wakenya,mfano mzuri ni Kenya airways juzi imefilisika na serikali ameuza hisa zake zote kwa mzungu

Kenya ni taifa linalo mtegemea sana mzungu kuliko chochote na wanakopa kweli kweli lakini wana ufisadi wa kutisha huku ata choo cha shule kinatafutiwa pesa za mkopo ili waweze kupga pesa

Ata hii GDP yao ya 100+B$ ni ya kutengenezwa kumbuka hii nchi ni kibaraka mkubwa wa mzungu(nikipata muda nitakuelezea vizuri kabisa)

Kiufupi,Kenya na Tanzania hakuna tofauti kubwa yoyote na bora Tanzania kuliko Kenya ndio maana ata wakenya wenyewe hawapendi nchi Yao wanaikubali Bongo kuliko maelezo na ndoto ya vijana wengi wa huku Nyanza na Mombasa wanapenda sana kuja bongo(kama ambavyo vijana wetu wanavyo penda kwenda SAUZI)

Kuna vingi nataman nikuweke sawa ila ngoja nikuachie hapa maana ninawahi Ibadani nikipata muda nitakuelezea Kinaga ubaga
 
Yote uliyoyaongea ni sahihi kasoro namba 3.
Ardhi yetu itabaki kwa Watanzania tu[emoji16]. Ardhi yetu inatakiwa ilindwe kwa nguvu zote kwa ajili ya wazawa tu wa nchi hii, hata Wakenya mnaojaribu kupata ardhi yetu kijanja kupitia migongo ya wazawa mnatakiwa mfurushwe.
1. Katiba yenu ni mbovu inakiuka sheria za natural justice mtu anaweza kaa jela without trial for a long time.
2. Mfumo wenu wa kibiashara to foreign investors kidogo unaweka vikwazo ambavyo nchi inayojaribu kuwa competitive haifai kuwa nazo. Mfano work permit ni ngumu kupata na tena very expensive. The world is now a global village wacheni kuji-isolate.

3. Foreigners can't own land unless for investments above $500,000. Land is a basic factor of production. Na hata ukiwa na iyo $500,000 lazima ungoje iyo process ikamiliki for more than 1 yr. Yaani mnataka investor angoje for that long?

4. Too many centers of power with unpredictable policies. Mara kwa mara huwa ninaona ma Regional commissioners in Tanzania wakiwaingilia investors hadharani ili kufurahisha wananchi na pia enforcing policies ambazo kana kwamba they are revenging against investors. Kutokuwa na katiba inayotoa ulinzi kwa investors haisaidii.

5. Kiswahili. Nyerere was very wise to teach you swahili ili kuunganisha makabila tofauti ya Tanzania but the effect of that too was to isolate you from mfumo wa globalisation ambao ndio ulikuwa unaenea kote duniani from the 1980's. Ukweli ni kwamba languages kama English ndio global languages, I can't imagine a Tanzanian youth trying to learning coding ili ajihusishe kwa hii dunia ya artificial intelligence yet their primary language ni kiswahili. Iyo inafanya mambo yake kuwa magumu sana.

6. Policy enforcers wenu are loyal to the president not constitution. Of course Kenya to some extent tuko hivyo but the amount of bootlicking in Tanzania is mind-boggling. Hii nafikiri explains ile point yangu ya policies kukuwa unpredictable.

7. Watanzania ni ngumu sana kukosa chakula kwa hivyo hamjihusishi sana na biashara kubwa kubwa. I cannot believe that kule mikoa ya Iringa mtu anaweza akanunua eka moja ya shamba na $100. Na hata sehemu za morogoro I saw sijui $400.
8. Remittances from Tanzanians living abroad ziko chini sana.

Bila hivyo vikwazo nimetaja hapo, Tanzania would be the largest economy in East Africa. Sioni vile Kenya tungewafikia. You guys can feed yourselves na bado mko na mashamba makubwa sana yako idle. Mko na natural resources ambazo sisi hatuna. Barabara na infrastructure mnazidi kujenga. Umeme mnazidi ku invest katika iyo sekta.

Having said that, Tanzania is the most beautiful country in East Africa. Mko na ecosystems mbalimbali na natural beauty mzuri sana. I still don't think you have explored your potential in Tourism that much.

One notable observation that I have made about TZ ni kuwa if a person is upper middle class na kuendelea in Tanzania then they are rich rich hakuna kubahatisha. While huku kenya mtu anaweza kuwa hivyo lakini kuna cycles ambazo anashukashuka na kupanda. But in Tanzania if you are rich, you are rich. It looks like upward mobility in Tanzania ni ngumu sana kwa wale wako chini.

Tanzania,kama una pesa is the best country to live in hapo hata mimi ninakubali. Middle class yenu niko sure they enjoy sana, kama vile middle class ya south africa does.
 
Sana tena sana!

Hata kidemokrasia wametuacha mbali sana.

Raila wakati ule kaenda kujiapisha na wafuasi wake waliandamana wakamaliza hatukuona askari yeyote alowapiga risasi wala mabomu ya machozi ya kuwatawanyisha.

Ingekuwa nchi yetu sipati picha !
 
Kama mtu wa kupiga soga kama hivi huwezi kuelewa Kenya walivyotuzidi.
Unaijua paypal? Kenya wanatuma na kupokea pesa kutoka paypal. Mtandaoni kuna fursa nyingi sana tunazikosa.
Kuna makampuni yanalipa kwa Paypal na Payoneer. Mfumo wa paypal ni rahisi unaingia kwenye simu moja kwa moja.
Wakati mwingine huwa natamani hata ningekuwa mkenya.
Yaan uwe mkenya kwa sababu ya paypal
 
Yote uliyoyaongea ni sahihi kasoro namba 3.
Ardhi yetu itabaki kwa Watanzania tu[emoji16]. Ardhi yetu inatakiwa ilindwe kwa nguvu zote kwa ajili ya wazawa tu wa nchi hii, hata Wakenya mnaojaribu kupata ardhi yetu kijanja kupitia migongo ya wazawa mnatakiwa mfurushwe.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwa kweli ardhi yenu inapendeza lakini kumbuka pia si wakenya tu. Any foreign investor akija kuwekeza, land will be a basic requirement. Sasa akishamaliza kudeal na vikwazo vya work permit anakutana na vikwazo vya ardhi. Kwa nini mnaogopa ku-compete?

Hili jambo nimelifuatilia sana kutoka enzi za kikweete and I think Tanzania will never change on issues of immigration and land ownership so usijali no one will take your land
 
Hata kwenye medical services wametuacha mbali sana.
Hiyo ni sababu za kihistoria, jiulize swali dogo kwanin Dar imeendelea kuliko miji mingine? Ukijua hilo jibu tayari unalo la kenya na Tz
 
..tatizo la Watanzanio sio kutokufanya kazi kwa bidii.

..we work as hard as Kenyans, if not harder.

..tofauti kati yetu, na haswa nikiangazia kilimo na ufugaji, ni kutokutumia maarifa na utaalamu wa kisasi.

..ukitaka kulitambua hilo angalia jinsi Wakenya wanavyolima na kufuga ulinganishe na Watanzania.

..Majirani na ndugu zetu wa Kenya wanatumia mbegu bora iwe kwenye kilimo au ufugaji, na mbinu zao ni za kisasa.
Hapo kwenye kilimo mbona umetupiga mkuu,60% ya chakula kenya wanategemea Tanzania,kilimo gani walichotupita wakenya!?
 
Back
Top Bottom