Ni kweli kabisa, na mimi hutembelea Kenya mara nyingi. Wabongo wengi hapa watasoma hii mada kuwa Wakenya wana viwanda vingi, majumba makubwa na barabara nzuri. Hivyo wanavyo. Lakini maendeleo hasa ya Kenya ni juu ya watu wake. Wakenya wako mbali sana kifikra na kielimu, kiasi ambacho Mkenya hu fit popote ulimwenguni. Maelfu ya Wakenya wafanya kazi Ghuba, tena siyo kazi za kufagia tu...kuendesha ndege, mabenki, polisi, jeshini... (kazi ambazo Mtanzania hata kuziomba hawezi!) Na hivyo hivyo Ulaya na Marekani.
Watanzania ni wafinyu wa upeo wa ulimwengu, waoga, wachache wa elimu....kwa ujumla 'binadamu Mtanzania amejawa na shida, hofu na mashaka'. Ikitokea kwamba amekwenda nje, aghalabu ni hizo kazi za maboksii, kuosha wazee....ndiyo, pengine wawili watatu watakuwa tofauti.
Nitasema tena: hii inatokana na utawala wa muda mrefu wa vitisho na ukandamizaji- police state, unaoendelea hadi leo. Aidha elimu ya kujua kusoma na kuandika tu (hata hiyo siku hizi ni mbinde). Nakubali maneno ya mchangiaji hapo juu 'Tanzania is doomed to be poor.
Watasema tuko uchumi wa kati, hahahahaa! Ni nani huyo? Sijakutana na Mtanzania wa uchumi wa kati miye!
Nini kifanyike?
Si vyema kulaumu tu bila kutoa ufumbuzi.
1- Tupambane kuleta katiba mpya. Bila ya hii hatutoki. Maana tatizo kubwa la Tanzania ni siasa na uongozi. Viongozi mbumbumbu wenye madaraka makubwa ya kupita kiasi, huchagua mbumbumbu wenzao katika sehemu nyeti. Tukiliondoa hili, tukapata viongozi weledi wenye madaraka yatokayo kwa umma, tutakuwa tumepiga hatua ya mwanzo.
2- Kubadilisha kabisa mfumo wa elimu. Ikibidi tu copy and paste mfumo wa jirani zetu uliofanikiwa. Tulete walimu kutoka Kenya, Uganda, Zimbabwe, nk kwa miaka mitano. Wakati huo tunarudia kuwa train walimu wtu na hatimaye tuchague wenye sifa tu. (Ndiyo, tutumie matrilioni, hata ikibidi tukope).
3- Kuvunjwa kabisa kwa jeshi la polisi na kurudia kulisuka upya, kupata polisi wenye elimu ya kiraia na wenye maadili.
4- Kupambana na rushwa ikiwezekana adhabu ya kifo kwa atakayeiba, kula rushwa ya sh. milioni 20 na kuendelea. Hawa ni wauaji kama wauaji wengine, isipokuwa madhara ya mauaji yao hayajulikani (can't be quantified)
Utaona hapo nimejikita kwenye kumtengeneza mtu kwanza, kabla ya vitu.
Sasa endelea......kuleta mapendekezo ya kilimo, biashara, viwanda nk.
Tukiweza, hayo yatakuwa maendeleo ya kweli.