Kenya imeiacha Tanzania parefu sana kimaendeleo, shida ni nini?

Kenya imeiacha Tanzania parefu sana kimaendeleo, shida ni nini?

SGR na Nyerere Dam vikiisha Kenya watatafutana maana bandari ya Mombasa itakosa mizigo yote ya maziwa makuu!

Kenya elimu inafundishwa in English na kuiunga nchi na international transfer of capital , technology and international market maana Kenya wanauza nje bidhaa nyingi kuliko Tz sababu ya kuweza kuwasiliana in English

Kenya ni nchi masikini kuliko Tz ni suala la muda tu kuipita iwapo Rais atakomaa na miundombinu na kuzuia upigaji ambao tayari umeshamiri. Magufuli alishaipita Kenya katika ukuaji uchumi ila akafa kwasasa tumerudi nyuma!
subutu eti magufuli alikuwa ameshawapita aliwapita kwalipi labda kuminya democrasia unadhani kenya wao wamelala au wameridhika na hali yao lah sisi tumejenga bwawa la nyerere lenye 2100mgwatt wakati kenya wao wanaanda kinu cha kuzalisha umeme wa kutumia urenium itamalizika 2034 watazalisha mgwt 35,000sasa wewe utawapita wapi wanarusha chombo agani wana viuo vingi na sekondary nyingi kuliko sisi mtaala wao wa elimu uko juu wakulima na wafugaji wanafuga kisasa wanauza nyama nje na mazao mengi wana export shirika lao la kenya airways liko hai wanapokea watalii wengi kwakuwa na hotel zenye hadhi kenya wako juu ndugu hujatembea kenya vizuri gata mji wa turukana uko juu kuliko mji wa Tabora japo ni jangwa
 
Tanzania iko buzzy kupinga ushoga mtandaoni, na kuacha kushughurika na mambo ya msingi, huku kutwa kukicha kwenda kwa mashoga kupiga magoti na kuwalamba miguu wawape msaada na mikopoo.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada nahisi uwenda huijui Kenya kwa marefu na mapana,sijajua labda unazungumzia kenya inatuzidi nini sisi Tanzania,nafikiri kama ungekuwa specific ingekuwa bora sana lakini ngoja nikutoe tongotongo mkuu…….

Mimi ni mjaluo au mluo,ninaenda sana kenya kuliko maelezo ata sasa nipo kenya kula x-mass..

Kenya ni nchi ya kibepari tena ule ulio kolea ukimkuta tajiri kenya jua ni tajiri kweli lakni pia ukimkuta maskini kenya jua ni maskini kweli,kiufupi Kenya wana maskini wengi sana kuliko Tanzania kwa kipato cha mmoja mmoja ata ukienda kwenye levels za matajiri,kenya hawana Billionaires kama wabongo TZ tuna billionaires wengi sana kuliko kenya (kama huamini nitakuelewesha kwa ushahidi)

Kwenye miundombinu wenzetu walianza kujenga flyovers,barabara ata njia za ndege toka kitambo sana tena nyingi vimefanywa na Wazungu sio wakenya ndio maana kuna barabara nyingi za kulipia lakini kitu ambacho huwez kukikuta TZ…Kiufupi Kenya uchumi unajengwa na wazungu na watu wa Asia sio wakenya,mfano mzuri ni Kenya airways juzi imefilisika na serikali ameuza hisa zake zote kwa mzungu

Kenya ni taifa linalo mtegemea sana mzungu kuliko chochote na wanakopa kweli kweli lakini wana ufisadi wa kutisha huku ata choo cha shule kinatafutiwa pesa za mkopo ili waweze kupga pesa

Ata hii GDP yao ya 100+B$ ni ya kutengenezwa kumbuka hii nchi ni kibaraka mkubwa wa mzungu(nikipata muda nitakuelezea vizuri kabisa)

Kiufupi,Kenya na Tanzania hakuna tofauti kubwa yoyote na bora Tanzania kuliko Kenya ndio maana ata wakenya wenyewe hawapendi nchi Yao wanaikubali Bongo kuliko maelezo na ndoto ya vijana wengi wa huku Nyanza na Mombasa wanapenda sana kuja bongo(kama ambavyo vijana wetu wanavyo penda kwenda SAUZI)

Kuna vingi nataman nikuweke sawa ila ngoja nikuachie hapa maana ninawahi Ibadani nikipata muda nitakuelezea Kinaga ubaga
wakenya wanaotamani bongo ni wale wanaoona fursa nyingi huko kwakuwa wengi wamelala na duniani kote maskini wapo hata burney inayo masikini na matajiri tukubali kenya imetupita sana mkuu hujatembea bongo vijiji bora jehanamu
 
tatizo lenu wabogo hata ukilalia ngozi ukijisaidia vichakani mnajisifia acha wengine wakusifiye hayo ya magufuli ni siasa tu hakuna reality yoyote alikuwa anakopa anawadanganya tunajenga napesa zetu bwawa la nyerere alisema litamaliza tatizo na umeme juzi waziri kasema hata bwawa likiisha bado tutaendelea na mgawo tukubali tumepitwa siyo dhambi bali tupambane tutoke huku tulipo
Watu wenye kiwango chako cha akili ndio walioletewa yale mabehewa chakavu!!

Huwezi kutoboa kwa akili kama zako za kijamaa!

Kwasasa world economy is characterized by competition, lazima tuipite Kenya kiuchumi na sio mbali sana!! Soma data za WB nimeweka utaona foreign investors wanatua tz sio kenya tena!!
 
Miji mikubwa minne ya Kenya Nairobi, Mombasa, Nakuru na Kisumu imeendelea sana tu kama miji ya Africa Kusini na hiyo ina beba kama robo ya kenya. Robo nyingine imeendelea kawaida tu kama kanda ya ziwa hivi au niseme kanda ya kaskakazini huku Tanzania ILA nusu ya Nchi ya kenya ni masikini wa kutupwa, hawana hakika na mlo, hakuna shule, Hospitali , hakuna usalama nk wanaishi maisha ya taabu na wanakufa kwa njaa kila mwaka
Nahisi utafiti wako umeangukia kwenye hiyo miji minne ambayo inabeba kama robo tu ya Kenya.
Kwenye hiyo miji kuna viwanda vikubwa vya wazungu ambavyo vinafanya pato la Nchi liwe kubwa.

Wako mbele kiuchumi ila kwa pato la mtu mmoja mmoja hali si shwari!
Hapa umeconclude man, umeandika kitaalam zaidi nq ndio hali halisi ya Kenya kwa anaejua
 
Watu wenye kiwango chako cha akili ndio walioletewa yale mabehewa chakavu!!

Huwezi kutoboa kwa akili kama zako za kijamaa!

Kwasasa world economy is characterized by competition, lazima tuipite Kenya kiuchumi na sio mbali sana!! Soma data za WB nimeweka utaona foreign investors wanatua tz sio kenya tena!!
mimi na wewe na maguma kama siyo wewe unasifia ujamaa na viongozi wako wa ccm wanalogwa na kukimbiza mwenge nimeishi kenya vijijini na mijini nimeishi uganda vijijini na mjini nimeushi japan vijijini na mjini na tanzania nimeishi vijijini vingi vya shida sisi tukubali tumepitwa tunazo resimali lakini sifuri tunataka katiba mpya ndiyo tunaweza kuwakuta wakenya ndugu
 
Wakuu twende mbele turudi nyuma, nchi ya Kenya imeitupa Tanzania mbali sana kimaendeleo. Nakiri sijawahi kufika Kenya, lakini nimekuwa mfuatiliaji sana wa mafanikio ya wenzetu kupitia kupitia Luninga na hasahasa Google Earth ambayo inaweza kukupeleka popote pale na kukuonesha mandhari mbalimbali duniani.

Nchi ya Kenya eneo lake kubwa ni Jangwa kama ionekavyo hapo chini ukifananisha na Tanzania. Pia eneo lake ni dogo ukilinganisha na Tanzania.

Sijaainisha ni maendeleo gani wametupita ila karibu nyanja zote utakazozifikiria wewe wao wapo mbele yetu.
Sisi Tz tunakwama wapi?
~ Je, ni historia ndio iliyoturudisha nyuma?
~ Je, ni mfumo wa Elimu?
~ Je, ni wanasiasa?

Shida ni nini hasa? Au sisi ni wavivu kufanya kazi? Nchi yetu imebarikiwa kila rasli mali, mito mingi, maziwa yametuzunguka, bahari, mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro, madini mbalimbali... Tufanye nini kuisaidia nchi yetu kusonga mbele?

Nimewiwa tu kuandika hivi nikiamini wapo wajuvi humu ndani na tunaweza kujadili pamoja.

Mungu ibariki Tanzania.

View attachment 2456941
Wananchi wanalia njaa Kila siku, Kenya tajiri ni tajiri na maskini ni maskini
 
Ni kweli kabisa, na mimi hutembelea Kenya mara nyingi. Wabongo wengi hapa watasoma hii mada kuwa Wakenya wana viwanda vingi, majumba makubwa na barabara nzuri. Hivyo wanavyo. Lakini maendeleo hasa ya Kenya ni juu ya watu wake. Wakenya wako mbali sana kifikra na kielimu, kiasi ambacho Mkenya hu fit popote ulimwenguni. Maelfu ya Wakenya wafanya kazi Ghuba, tena siyo kazi za kufagia tu...kuendesha ndege, mabenki, polisi, jeshini... (kazi ambazo Mtanzania hata kuziomba hawezi!) Na hivyo hivyo Ulaya na Marekani.
Watanzania ni wafinyu wa upeo wa ulimwengu, waoga, wachache wa elimu....kwa ujumla 'binadamu Mtanzania amejawa na shida, hofu na mashaka'. Ikitokea kwamba amekwenda nje, aghalabu ni hizo kazi za maboksii, kuosha wazee....ndiyo, pengine wawili watatu watakuwa tofauti.
Nitasema tena: hii inatokana na utawala wa muda mrefu wa vitisho na ukandamizaji- police state, unaoendelea hadi leo. Aidha elimu ya kujua kusoma na kuandika tu (hata hiyo siku hizi ni mbinde). Nakubali maneno ya mchangiaji hapo juu 'Tanzania is doomed to be poor.
Watasema tuko uchumi wa kati, hahahahaa! Ni nani huyo? Sijakutana na Mtanzania wa uchumi wa kati miye!
Nini kifanyike?
Si vyema kulaumu tu bila kutoa ufumbuzi.
1- Tupambane kuleta katiba mpya. Bila ya hii hatutoki. Maana tatizo kubwa la Tanzania ni siasa na uongozi. Viongozi mbumbumbu wenye madaraka makubwa ya kupita kiasi, huchagua mbumbumbu wenzao katika sehemu nyeti. Tukiliondoa hili, tukapata viongozi weledi wenye madaraka yatokayo kwa umma, tutakuwa tumepiga hatua ya mwanzo.
2- Kubadilisha kabisa mfumo wa elimu. Ikibidi tu copy and paste mfumo wa jirani zetu uliofanikiwa. Tulete walimu kutoka Kenya, Uganda, Zimbabwe, nk kwa miaka mitano. Wakati huo tunarudia kuwa train walimu wtu na hatimaye tuchague wenye sifa tu. (Ndiyo, tutumie matrilioni, hata ikibidi tukope).
3- Kuvunjwa kabisa kwa jeshi la polisi na kurudia kulisuka upya, kupata polisi wenye elimu ya kiraia na wenye maadili.
4- Kupambana na rushwa ikiwezekana adhabu ya kifo kwa atakayeiba, kula rushwa ya sh. milioni 20 na kuendelea. Hawa ni wauaji kama wauaji wengine, isipokuwa madhara ya mauaji yao hayajulikani (can't be quantified)
Utaona hapo nimejikita kwenye kumtengeneza mtu kwanza, kabla ya vitu.
Sasa endelea......kuleta mapendekezo ya kilimo, biashara, viwanda nk.
Tukiweza, hayo yatakuwa maendeleo ya kweli.
 
Yote hayo ni uongozi legelege.Tulianza kuelekea pazuri baadae tena nchi imevurugwa.
 
Wakenya ni wapambanaji wakubwa (Hustlers) wametapakaa kila pembe ya dunia kusaka fursa pia wanapeana sapoti wao kwa wao kwenda ughaibuni kusaka fursa na demokrasia yao ipo vizuri hasa sera ya kuruhusu Uraia pacha kwa raia wake.

Hii inawasaidia watu kwenda nje kutafuta ujuzi, Ajira na "in return" fedha wanazopata kama Diaspora zinachangia ukuaji wa uchumi

Pia Kenya wana mfumo mzuri wa Elimu na katiba yao pia ni nzuri.

Njoo bongo sasa Kupata pasipoti ya kusafiria tu hadi uzungushwe weeeehh!!! Utoe Rushwa weeeh! Uhojiwe maswali ya kijinga! Uambiwe mara leta barua ya uthibitisho uendako,mara barua ya Afisa mtendaji, Mara wakwambie majina yako kwenye vyeti hayafanani!!???? Process kibao!

Tz bado ina wajinga wengi sana na sera za kijinga na kipumbavu za Uchawa na kusifia ujinga wa viongozi wao.

Tanzania is doomed to remain poor!!!
Yes, you are very right...

Tena Kenya sera zao, sheria zao za kibiashara ziko very flexible...

Kule biashara zote; mfano banking, maduka, supermarkets, transportation nk nk ni 24hrs, 7days a week...

Hakuna business restrictions za kipuuzi kama ilivyo hapa kwetu Tanzania...

Yaani serikali inawawekea watu vikwazo vingi vya kibiashara na ufanyaji kazi na wakati huohuo serikali hiyohiyo inawekekea watu wake tozo na kodi za kufa mtu za kila siku...

Hebu ona tu tatizo la umeme na maji yanavyorudisha maendeleo ya watu na nchi nyuma huku viongozi wakionekana kama kutojali chochote...

Haiwezekani tukawa hatuna vyombo vinavyo forecast mbele kujua kuwa zisipochukuliwa hatua A, B, na C sasa miaka miwili kutakuwa na shida ya maji au umeme ili hatua zichukuliwe kabla ya tatizo kutokea. Serikali ya Tanzania ni defensive zaidi kuliko kuwa offensive...

Mimi nasema moja ya tatizo linaloi - disqualify CCM na serikali yao ni namna wanavyo-deal na changamoto ya maji na umeme..

Yaani ni kana kwamba tulikuwa vitani au hatukuwa na serikali before...!

Ukirudi tena kwenye maswala ya biashara, ni matatizo matupu...

Mfano sheria ya kulazimisha biashara ya bar na maeneo ya starehe, usafirishaji wa abiria kutofanyika masaa 24 ni ya nini...?

Jamani, ni kweli tupende tusipende shida za umasikini na udhaifu wa uchumi wetu ni la kimfumo zaidi...

Mfumo huzaa tatizo la kiuongozi na hawa viongozi ndiyo hutuandalia sera na mipango ya hovyo inayozaa matatizo haya...
 
Hapo kwenye kilimo mbona umetupiga mkuu,60% ya chakula kenya wanategemea Tanzania,kilimo gani walichotupita wakenya!?

..wenzetu wanafuga kisasa zaidi.

..wanaongoza Afrika Mashariki kwa kuzalisha maziwa ingawa Tanzania inaongoza kwa idadi ya mifugo.

..pia tuna mengi ya kujifunza toka kwao ktk kilimo cha mbogamboga na matunda, kuongeza thamani ya mazao, na ku-EXPORT.
 
Tofauti yetu ni Elimu/exposure kati ya Kenya na Tanzania kuanzia viongozi wa kisiasa hadi raia.
Hapo kwenye Elimu mwingine anaweza kuniuliza ina maana Tanzania hakuna wasomi?
Jibu ni kwamba Tanzania pia wasomi wapo ila wamekosa exposure hii inafanya kudumaza akili na kuishi kwa mazoea.
Mtu aliyeishia high school Kenya anaweza akawa mjanja sana wa kuona mambo na kuchungulia nje ya box kuliko mwenye Graduate Degree wa Tanzania kutokana na kukosa exposure.
Hapa sijui naeleweka

..nadhani lugha ya Kiingereza inatunyong'onyeza tunaposhindanishwa na Wakenya kimataifa.

..pia unaweza kukuta wasomi wetu sio wazuri ktk kutumia tehama, lakini nadhani hiyo gap imepungua sasa hivi.

..ukija kwenye mtaala naamini mtaala wa NECTA ni mzuri na mgumu kuliko mtaala wa nchi zote Afrika Mashariki.

..Kwa hiyo Mtanzania akishachangamka kwenye lugha na tehama majirani lazima wakae chini.
 
Wakuu twende mbele turudi nyuma, nchi ya Kenya imeitupa Tanzania mbali sana kimaendeleo. Nakiri sijawahi kufika Kenya, lakini nimekuwa mfuatiliaji sana wa mafanikio ya wenzetu kupitia kupitia Luninga na hasahasa Google Earth ambayo inaweza kukupeleka popote pale na kukuonesha mandhari mbalimbali duniani.

Nchi ya Kenya eneo lake kubwa ni Jangwa kama ionekavyo hapo chini ukifananisha na Tanzania. Pia eneo lake ni dogo ukilinganisha na Tanzania.

Sijaainisha ni maendeleo gani wametupita ila karibu nyanja zote utakazozifikiria wewe wao wapo mbele yetu.
Sisi Tz tunakwama wapi?
~ Je, ni historia ndio iliyoturudisha nyuma?
~ Je, ni mfumo wa Elimu?
~ Je, ni wanasiasa?

Shida ni nini hasa? Au sisi ni wavivu kufanya kazi? Nchi yetu imebarikiwa kila rasli mali, mito mingi, maziwa yametuzunguka, bahari, mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro, madini mbalimbali... Tufanye nini kuisaidia nchi yetu kusonga mbele?

Nimewiwa tu kuandika hivi nikiamini wapo wajuvi humu ndani na tunaweza kujadili pamoja.

Mungu ibariki Tanzania.

View attachment 2456941
Huijui Kenya, na hata kusoma habari zake unazisoma lakini huzielewi.

Nina hamu sana ya kukujibu kwa kirefu, lakini sina muda wa kufanya hivyo sasa hivi.

Nikushauri tu kwa sasa hivi, ondoa kasumba kichwani mwako kwanza. Fungua akili uelewe mambo kwa uhalisia wake.
 
Back
Top Bottom