Kenya imeiacha Tanzania parefu sana kimaendeleo, shida ni nini?

Kenya imeiacha Tanzania parefu sana kimaendeleo, shida ni nini?

Wakenya ni wapambanaji wakubwa (Hustlers) wametapakaa kila pembe ya dunia kusaka fursa pia wanapeana sapoti wao kwa wao kwenda ughaibuni kusaka fursa na demokrasia yao ipo vizuri hasa sera ya kuruhusu Uraia pacha kwa raia wake.

Hii inawasaidia watu kwenda nje kutafuta ujuzi, Ajira na "in return" fedha wanazopata kama Diaspora zinachangia ukuaji wa uchumi

Pia Kenya wana mfumo mzuri wa Elimu na katiba yao pia ni nzuri.

Njoo bongo sasa Kupata pasipoti ya kusafiria tu hadi uzungushwe weeeehh!!! Utoe Rushwa weeeh! Uhojiwe maswali ya kijinga! Uambiwe mara leta barua ya uthibitisho uendako,mara barua ya Afisa mtendaji, Mara wakwambie majina yako kwenye vyeti hayafanani!!???? Process kibao!

Tz bado ina wajinga wengi sana na sera za kijinga na kipumbavu za Uchawa na kusifia ujinga wa viongozi wao.

Tanzania is doomed to remain poor!!!
Umenikumbusha mbali sana, nilikuwa naenda chuo nje ya nchi. Niliomba passport mwezi septemba 2021 nimeipata AUGUST 2022.Kisa jina la Babu yangu mzaa mama jina lake limefanana na majina ya BURUNDI aiseeee.
 
shirika lao la ujasusi linafanya kazi Kwa weledi ktk kuboresha uchumi wa nchi yao, wakati sisi Tiss wapo bize na wanasiasa.
TISS walipiga kambi Zanzibar wakati wa uchaguzi na kukiteka kiwanda cha uchapaji cha SMZ huku wakijifungia ndani mwezi mzima wakichapisha kura feki na kuratibu uchaguzi na kulitumia jeshi kuuwa watu ili kumweka kibaraka wao kutoka Mkuranga Mwinyi
 
Uwongo the gap is widening. Miaka ya 90-2000 GDP ya Tanzania na Kenya zilikuwa zafukuzana. Leo uchumi wa Kenya unaelekea kuwa mara mbili ya wa Tanzania kwa GDP
fungua akili yako achana na maisha ya kukariri, nyang'au unabishana na data! Kweli tz tuko karibu kuwapita!
 
Umenikumbusha mbali sana, nilikuwa naenda chuo nje ya nchi. Niliomba passport mwezi septemba 2021 nimeipata AUGUST 2022.Kisa jina la Babu yangu mzaa mama jina lake limefanana na majina ya BURUNDI aiseeee.
Ukiweka cheti cha kuzaliwa na namba ya NIDA , passport unapewa one week tu , ofcourse uwe unamjua mtu pale na uweke na chai kidogo laki mbili! Umepita njia ndeeeeefu kama treni ya kigoma iliyojazwa mabehewa chakavu ya mtumba ya bilioni mbili mbili na treni nzima iliyoondoka Dar kwenda kigoma ina thamani ya trilioni kumi yani thamani ya mabehewa na vichwa viwili vyote mtumba!!
 
..wenzetu wanafuga kisasa zaidi.

..wanaongoza Afrika Mashariki kwa kuzalisha maziwa ingawa Tanzania inaongoza kwa idadi ya mifugo.

..pia tuna mengi ya kujifunza toka kwao ktk kilimo cha mbogamboga na matunda, kuongeza thamani ya mazao, na ku-EXPORT.
Fanya research vizuri mzee,kidata hao wakenya wametuzidi kwenye maziwa ila kiuhalisia tumewazidi miles,kamwe kenya huwezi kukuta maziwa yakiuzwa kiholela kama TZ,kwa mfano huku kimara tu kuna wafugaji zaidi ya 100 na asubuhi mpaka saa 6 ukuti maziwa,huo ni mfano wa sehemu ndogo tu,serikali ikiamua kuingia deep kenya hawatuwezi maana huko kwao ukuti maziwa yakiuzwa mtaani
 
Fanya research vizuri mzee,kidata hao wakenya wametuzidi kwenye maziwa ila kiuhalisia tumewazidi miles,kamwe kenya huwezi kukuta maziwa yakiuzwa kiholela kama TZ,kwa mfano huku kimara tu kuna wafugaji zaidi ya 100 na asubuhi mpaka saa 6 ukuti maziwa,huo ni mfano wa sehemu ndogo tu,serikali ikiamua kuingia deep kenya hawatuwezi maana huko kwao ukuti maziwa yakiuzwa mtaani

..tuna mengi ya kujifunza toka Kenya kuhusu kilimo na ufugaji wa kisasa.

..tuache ubishi na ujuaji usio na faida kwetu.

..Na Watanzania tusipojizatiti Uganda nao wanakuja kwa kasi sana ktk kilimo.

..Mfano mdogo, Uganda wameshatu-overtake ktk kilimo cha Chikichi ingawa sisi tuliwatangulia ktk kilimo hicho.
 
..tuna mengi ya kujifunza toka Kenya kuhusu kilimo na ufugaji wa kisasa.

..tuache ubishi na ujuaji usio na faida kwetu.

..Na Watanzania tusipojizatiti Uganda nao wanakuja kwa kasi sana ktk kilimo.

..Mfano mdogo, Uganda wameshatu-overtake ktk kilimo cha Chikichi ingawa sisi tuliwatangulia ktk kilimo hicho.
Bila kusahau maparachichi kutoka Uganda kila siku yanasafirishwa kwenda nchi za uarabuni Dubai,Saudia,Bahrain,Qatar nayashuhudia kwa macho yangu ila ya Tanzania sijawahi kuyaona.
 
Bila kusahau maparachichi kutoka Uganda kila siku yanasafirishwa kwenda nchi za uarabuni Dubai,Saudia,Bahrain,Qatar nayashuhudia kwa macho yangu ila ya Tanzania sijawahi kuyaona.

..Jaribu kumsikiliza mkulima wa parachichi wa kenya.

..sitaki kuongeza yangu. Msikilize halafu utoe tafsiri ya ulichokiona na kukisikia.

 
Ni kweli kabisa, na mimi hutembelea Kenya mara nyingi. Wabongo wengi hapa watasoma hii mada kuwa Wakenya wana viwanda vingi, majumba makubwa na barabara nzuri. Hivyo wanavyo. Lakini maendeleo hasa ya Kenya ni juu ya watu wake. Wakenya wako mbali sana kifikra na kielimu, kiasi ambacho Mkenya hu fit popote ulimwenguni. Maelfu ya Wakenya wafanya kazi Ghuba, tena siyo kazi za kufagia tu...kuendesha ndege, mabenki, polisi, jeshini... (kazi ambazo Mtanzania hata kuziomba hawezi!) Na hivyo hivyo Ulaya na Marekani.
Watanzania ni wafinyu wa upeo wa ulimwengu, waoga, wachache wa elimu....kwa ujumla 'binadamu Mtanzania amejawa na shida, hofu na mashaka'. Ikitokea kwamba amekwenda nje, aghalabu ni hizo kazi za maboksii, kuosha wazee....ndiyo, pengine wawili watatu watakuwa tofauti.
Nitasema tena: hii inatokana na utawala wa muda mrefu wa vitisho na ukandamizaji- police state, unaoendelea hadi leo. Aidha elimu ya kujua kusoma na kuandika tu (hata hiyo siku hizi ni mbinde). Nakubali maneno ya mchangiaji hapo juu 'Tanzania is doomed to be poor.
Watasema tuko uchumi wa kati, hahahahaa! Ni nani huyo? Sijakutana na Mtanzania wa uchumi wa kati miye!
Nini kifanyike?
Si vyema kulaumu tu bila kutoa ufumbuzi.
1- Tupambane kuleta katiba mpya. Bila ya hii hatutoki. Maana tatizo kubwa la Tanzania ni siasa na uongozi. Viongozi mbumbumbu wenye madaraka makubwa ya kupita kiasi, huchagua mbumbumbu wenzao katika sehemu nyeti. Tukiliondoa hili, tukapata viongozi weledi wenye madaraka yatokayo kwa umma, tutakuwa tumepiga hatua ya mwanzo.
2- Kubadilisha kabisa mfumo wa elimu. Ikibidi tu copy and paste mfumo wa jirani zetu uliofanikiwa. Tulete walimu kutoka Kenya, Uganda, Zimbabwe, nk kwa miaka mitano. Wakati huo tunarudia kuwa train walimu wtu na hatimaye tuchague wenye sifa tu. (Ndiyo, tutumie matrilioni, hata ikibidi tukope).
3- Kuvunjwa kabisa kwa jeshi la polisi na kurudia kulisuka upya, kupata polisi wenye elimu ya kiraia na wenye maadili.
4- Kupambana na rushwa ikiwezekana adhabu ya kifo kwa atakayeiba, kula rushwa ya sh. milioni 20 na kuendelea. Hawa ni wauaji kama wauaji wengine, isipokuwa madhara ya mauaji yao hayajulikani (can't be quantified)
Utaona hapo nimejikita kwenye kumtengeneza mtu kwanza, kabla ya vitu.
Sasa endelea......kuleta mapendekezo ya kilimo, biashara, viwanda nk.
Tukiweza, hayo yatakuwa maendeleo ya kweli.
Duuuh! Idadi kubwa tumekuelewa sana
 
1. Katiba yenu ni mbovu inakiuka sheria za natural justice mtu anaweza kaa jela without trial for a long time.
2. Mfumo wenu wa kibiashara to foreign investors kidogo unaweka vikwazo ambavyo nchi inayojaribu kuwa competitive haifai kuwa nazo. Mfano work permit ni ngumu kupata na tena very expensive. The world is now a global village wacheni kuji-isolate.

3. Foreigners can't own land unless for investments above $500,000. Land is a basic factor of production. Na hata ukiwa na iyo $500,000 lazima ungoje iyo process ikamiliki for more than 1 yr. Yaani mnataka investor angoje for that long?

4. Too many centers of power with unpredictable policies. Mara kwa mara huwa ninaona ma Regional commissioners in Tanzania wakiwaingilia investors hadharani ili kufurahisha wananchi na pia enforcing policies ambazo kana kwamba they are revenging against investors. Kutokuwa na katiba inayotoa ulinzi kwa investors haisaidii.

5. Kiswahili. Nyerere was very wise to teach you swahili ili kuunganisha makabila tofauti ya Tanzania but the effect of that too was to isolate you from mfumo wa globalisation ambao ndio ulikuwa unaenea kote duniani from the 1980's. Ukweli ni kwamba languages kama English ndio global languages, I can't imagine a Tanzanian youth trying to learning coding ili ajihusishe kwa hii dunia ya artificial intelligence yet their primary language ni kiswahili. Iyo inafanya mambo yake kuwa magumu sana.

6. Policy enforcers wenu are loyal to the president not constitution. Of course Kenya to some extent tuko hivyo but the amount of bootlicking in Tanzania is mind-boggling. Hii nafikiri explains ile point yangu ya policies kukuwa unpredictable.

7. Watanzania ni ngumu sana kukosa chakula kwa hivyo hamjihusishi sana na biashara kubwa kubwa. I cannot believe that kule mikoa ya Iringa mtu anaweza akanunua eka moja ya shamba na $100. Na hata sehemu za morogoro I saw sijui $400.
8. Remittances from Tanzanians living abroad ziko chini sana.

Bila hivyo vikwazo nimetaja hapo, Tanzania would be the largest economy in East Africa. Sioni vile Kenya tungewafikia. You guys can feed yourselves na bado mko na mashamba makubwa sana yako idle. Mko na natural resources ambazo sisi hatuna. Barabara na infrastructure mnazidi kujenga. Umeme mnazidi ku invest katika iyo sekta.

Having said that, Tanzania is the most beautiful country in East Africa. Mko na ecosystems mbalimbali na natural beauty mzuri sana. I still don't think you have explored your potential in Tourism that much.

One notable observation that I have made about TZ ni kuwa if a person is upper middle class na kuendelea in Tanzania then they are rich rich hakuna kubahatisha. While huku kenya mtu anaweza kuwa hivyo lakini kuna cycles ambazo anashukashuka na kupanda. But in Tanzania if you are rich, you are rich. It looks like upward mobility in Tanzania ni ngumu sana kwa wale wako chini.

Tanzania,kama una pesa is the best country to live in hapo hata mimi ninakubali. Middle class yenu niko sure they enjoy sana, kama vile middle class ya south africa does.
Mtu akikukosoa hivi unamsikiliza na kumpa hata juisi ya sharubati.
 
Tofauti yetu ni Elimu/exposure kati ya Kenya na Tanzania kuanzia viongozi wa kisiasa hadi raia.
Hapo kwenye Elimu mwingine anaweza kuniuliza ina maana Tanzania hakuna wasomi?
Jibu ni kwamba Tanzania pia wasomi wapo ila wamekosa exposure hii inafanya kudumaza akili na kuishi kwa mazoea.
Mtu aliyeishia high school Kenya anaweza akawa mjanja sana wa kuona mambo na kuchungulia nje ya box kuliko mwenye Graduate Degree wa Tanzania kutokana na kukosa exposure.
Hapa sijui naeleweka
Exposure kwa huyo wa high school una maanisha nini?
 
Mnabwabwa ujinga tupu.
Nyie ndio mapopoma mnao zungumziwa...wajinga kama wewe ndio mnafanya Tanzania izidi kuwa Maskini.

Mada zenye tija kama hii huwa mnakazana kuzipinga mnataka mada za simba&Yanga, mada za Udini uislamu vs ukristo na wanawake.

Umaskini wa Tanzania sio kiuchumi tu hata kifikra na kiakili kwa raia kama wewe na jopo jingi la wajinga lililopo!!!
 
Nyie ndio mapopoma mnao zungumziwa...wajinga kama wewe ndio mnafanya Tanzania izidi kuwa Maskini.

Mada zenye tija kama hii huwa mnakazana kuzipinga mnataka mada za simba&Yanga, mada za Udini uislamu vs ukristo na wanawake.

Umaskini wa Tanzania sio kiuchumi tu hata kifikra na kiakili kwa raia kama wewe na jopo jingi la wajinga lililopo!!!
Kasage chupa umeze na panado we mlalamikaji usiyekuwa na majawabu ya unachokilalamikia! IDIOT!
 
Back
Top Bottom