Kenya is not serious ona hii


Ni sawa kabisa kuwa tuna tofautiana kilahaja na Unguja. Lkn ukweli tukubali ukweli kwamba kunapokuwa na mabishano au mgongano wa neno au kifungu cha maneno kati ya Tanzania na kenya, au na nchi nyingine yoyote, rejea iwe kiswahili cha Tanzania.
Umetaja vizuri sana mfano wa nchi zinazo zungumza kiingereza. Lkn nao wana kanuni moja. Mgongano ukitokea, basi rejea yao haiwi mahala pengine popote, bali ni kiingereza cha Uingereza.
 
Wacha ujinga ,hii ni sawa na "colour" ya Uingereza na "color" ya Marekani ama "truck" ya Marekani na neno "lorry' linalotumiwa Uingereza ....hizo neno zote ni sawa na hakuna nchi moja wanaojiona wajuaji zaidi.
au tyre na tire.... ni the same.
 


Umesha anza kuwa msemaji wa watu humu ndani!!?
Nani kakwambia hakizingatii kiswahili??
 


Hayo uansema wewe ndugu kadiri unavyojisikia wala huna ushahidi wowote. N anakuelewa sana,kwamba hivyo ni vile unajisikia, hisia zako zinakutuma hivyo. Linapokuja matumizi ya lugha, humpangii mtumiaji. Si unaona hata hapa kwetu, BAKITA, TUKI na siku hizi tuna TATAKI, wanajitahidi kuja na msamiati kwa maneno mageni hasa ya tekolojia lakini mzungumzaji gani umesikia anasema tarakilishi badala ya kompyuta, nani anasema vimbaka badala ya toothpick n.k.?

Mfano huo hapo juu ni wa ndani, nyinyi kwa nyinyi, sasa kama hata kitaifa kuna changamoto hizi , kimataifa je? Wewe ni nani umshurutishe nchi nyingine kuongea utakavyo? Hapa haijalishi lahaja yako ni bora au la, msingi wa lugha upo kwenye kuwasiliana, wenyewe wanawasilaina, wewe ni nani uwaambie hivyo ni vibaya?

Umetoa mfano wa Kiingereza cha Marekani na UK, usemacho si kweli, si kweli, si kweli, si kweli hata chembe.Hakuna hata mmoja kati ya nchi mbili hizi inayokubali Kiingereza cha mwenzake. UK inaona US ni takataka, wao ndiyo wenye Kiingereza, na US inakiona ki-UK ni ubabu, kimepitwa na wakati na ni lahaja ya kikoloni. Na kuna mazingira uchumi unasaidia kuifanya lugha yako kuwa juu, hivyo, kwa sasa UK amekaliwa kwani kwenye uchumi na teknolojia lahaja maarufu ni ya USA. unakutana na kompyuta, itakupa machaguo kama unataka UK ama USA, cha ajabu default ni USA, na ni kama inakulazimisha, mara kwa mara inakurudisha USA.

Kwa kifupi lahaja zote kati ya USA na UK hutumika. Kinachotakiwa mwandishi usiyumbeyumbe, unashauriwa ukichagua lahaja moja baki hapohapo kuepusha mkanganyiko.
 
Ahsante kwa Maelezo mujaarabu mkuu
 
Kwani wahaya hawawezi kuongea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…