komora096
JF-Expert Member
- Sep 26, 2018
- 20,548
- 5,647
Bwahahahaaa....we sema hujui tuKaangalie ile post yako kama uliandika neno makinikia.... wewe uliandika kitu kingine kabisa, maana ulianza na silabi ku na siyo ma.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bwahahahaaa....we sema hujui tuKaangalie ile post yako kama uliandika neno makinikia.... wewe uliandika kitu kingine kabisa, maana ulianza na silabi ku na siyo ma.
Hapo itakuwa shida kidogo. Kuna suala la lahaja, wao Kenya wana Kiswahili chao na sisi Tz kuna chetu. Kama pande zote tumekubaliana kuwa hiki ndicho Kiswahili sanifu hapo sawa. Ni kweli, sote tunafahamu historia ya usanifishaji wa Kiswahili kuwa Kiunguja ndicho kiikubalika na kuwa lahaja iliyotumika kusanifisha Kiswahili, lakini, ni kweli mpaka leo Kiunguja ndicho kinatumika ukanda wote wa Afrika ya mashariki kama rejea ya Kiswahili sanifu? Jibu ni hapana,kwani hata Tz bara bado tuna tofauti kubwa na Kiunguja, aidha, ni kawaida kwa wabara kuwabeza waunguja kwa matamshi ama miundo yao ya lugha ya Kiswahili, na wao pia wamekuwa wakifanya hivyo kwetu. Kwahiyo hali ipo hivi, wakati wewe una umeme, mkenya ana stima, wewe una ugali ,mkenya ana sima, wewe una mlinzi, mkenya ana bawabu n.k.
Pengine hoja yako itufungue masikio sasa, tuanze kufikiria kuwa na msamiati sanifu tutakaoutumia pande zote. Jambo la kuzingatia ni kuwa hii si kwa Kiswahili pekee, hata lugha kama Kiingereza hukutana na changamoto hizi, Kimarekani, Kiautsralia, Ki-british n.k havifanani hata. Na wao kila mmoja ana standard yake, hawajakubaliana kuwa na lahaja moja sanifu. Ukijifunza lugha zao inabidi ujue najifunza cha wapi.
Bwahahahaaa....we sema hujui tu
au tyre na tire.... ni the same.Wacha ujinga ,hii ni sawa na "colour" ya Uingereza na "color" ya Marekani ama "truck" ya Marekani na neno "lorry' linalotumiwa Uingereza ....hizo neno zote ni sawa na hakuna nchi moja wanaojiona wajuaji zaidi.
Sasa unamfunza mtu mwenye hta kiswahili hakitilii maanani....mwenzako huyo ana lugha zenye yupo vizuri sana hta zaidi ya kiswahili..
Ni sawa na kumchukua msukuma wa usukumani au wale jamaa wa kagera na bukoba....halafu useme wanaongea kiswahili sanifu...[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
Ni sawa kabisa kuwa tuna tofautiana kilahaja na Unguja. Lkn ukweli tukubali ukweli kwamba kunapokuwa na mabishano au mgongano wa neno au kifungu cha maneno kati ya Tanzania na kenya, au na nchi nyingine yoyote, rejea iwe kiswahili cha Tanzania.
Umetaja vizuri sana mfano wa nchi zinazo zungumza kiingereza. Lkn nao wana kanuni moja. Mgongano ukitokea, basi rejea yao haiwi mahala pengine popote, bali ni kiingereza cha Uingereza.
Mbona kama ya Bongo View attachment 1133412
Hapo itakuwa shida kidogo. Kuna suala la lahaja, wao Kenya wana Kiswahili chao na sisi Tz kuna chetu. Kama pande zote tumekubaliana kuwa hiki ndicho Kiswahili sanifu hapo sawa. Ni kweli, sote tunafahamu historia ya usanifishaji wa Kiswahili kuwa Kiunguja ndicho kiikubalika na kuwa lahaja iliyotumika kusanifisha Kiswahili, lakini, ni kweli mpaka leo Kiunguja ndicho kinatumika ukanda wote wa Afrika ya mashariki kama rejea ya Kiswahili sanifu? Jibu ni hapana,kwani hata Tz bara bado tuna tofauti kubwa na Kiunguja, aidha, ni kawaida kwa wabara kuwabeza waunguja kwa matamshi ama miundo yao ya lugha ya Kiswahili, na wao pia wamekuwa wakifanya hivyo kwetu. Kwahiyo hali ipo hivi, wakati wewe una umeme, mkenya ana stima, wewe una ugali ,mkenya ana sima, wewe una mlinzi, mkenya ana bawabu n.k.
Pengine hoja yako itufungue masikio sasa, tuanze kufikiria kuwa na msamiati sanifu tutakaoutumia pande zote. Jambo la kuzingatia ni kuwa hii si kwa Kiswahili pekee, hata lugha kama Kiingereza hukutana na changamoto hizi, Kimarekani, Kiautsralia, Ki-british n.k havifanani hata. Na wao kila mmoja ana standard yake, hawajakubaliana kuwa na lahaja moja sanifu. Ukijifunza lugha zao inabidi ujue najifunza cha wapi.
Sasa unamfunza mtu mwenye hta kiswahili hakitilii maanani....mwenzako huyo ana lugha zenye yupo vizuri sana hta zaidi ya kiswahili..
Ni sawa na kumchukua msukuma wa usukumani au wale jamaa wa kagera na bukoba....halafu useme wanaongea kiswahili sanifu...[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
Safi sana mkuuAhsante kwa Maelezo mujaarabu mkuu