Kenya kama kwetu, Maandamano halali na haramu sambamba leo

Kenya kama kwetu, Maandamano halali na haramu sambamba leo

Tatizo ni wenye madaraka kutotokea kwenye mazungumzo wakiwa na nia njema.

Angalia hii mbuzi:

View attachment 2606882

Huyu anaelewa nini kuhusiana na maridhiano yenye tija? Huyu si kama kina Tyson wa kwetu tu?

"Huwezi kuja kwenye maridhiano na misimamo yako mfukoni."

Dawa ya moto ni moto!

Tutaelewana tu.
Mama kaongea mishahara tuliza kalio. Ya wakenya waachie wao. Kwa sasa unaongoza kwa kiherehere humu
 
Mama kaongea mishahara tuliza kalio. Ya wakenya waachie wao. Kwa sasa unaongoza kwa kiherehere humu

Siyo kuwa mtuliza kalio inabidi uwe wewe? Si kuwa unayeongoza kwa kiherehere ni wewe? Kwani umeitwa hapa?

Bure kabisa!
 
Wakenya wanajitahidi kuiwajibisha serikali tofauti na watanzania wengi ni kusifia tu huku serijaki ikifanya mamvo ya hovyo haijawahi kutokea toka uhuru.taarifa y CAG imeonesha uhovyo wa serikali ya sasa ya tanzani

Tuna mavijana ya hovyo mengi. Kama watanzania wenyewe ni kama haya makina Mikojo Mburahati huko utegemee nini mkuu?
 
Kama Nia ya maandamano ni kutaka Bei ya UNGA ishuke, waandamanaji wangeshiriki shughuli za kulimo time hii mvua zinanyesha Ili kuona chakula kitapatikana kiasi Gani.

Kuandamana this time mvua inapotelea ground bila kulima Si sawa.

June ingekuwa time sahihi Kwa maandamano maana wangekuwa ktk nafasi nzuri kuona RUZUKU ya mbolea Serikali iliyotoa imeleta impact ipi ktk Bei za vyakula nchini mwao.

Mbali na hapo, naeza Sema maandamano wameyazoea.
 
Tatizo hao waandamanaji wengi ni wezi wanaiba mali za watu serikali isifumbie macho huo upuuzi.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app

Ungependa tutafute haki zetu ikiwamo Katiba Mpya ikibidi kwa maandamano?

Wewe hujui kuwa hata kwetu Polisi au wale FFU ni kawaida kuanzisha vurugu au uporaji ili kujipa uhalali wa kuzuia maandamano, kupiga, kukamata au kuuwa watu kinyume cha haki?

Au wewe ni mlamba asali, mhuni au kijana wa hovyo?
 
Maandamano halali kisheria japo mtawala anayaita haramu, lakini waandamanaji kwa kutambua haki zao wanaandamana bila kuogopa kitisho cha mtawala wa vyombo vya dola.

Tujiulize, Vipi kwetu tupo tayari hata kama Katiba Mpya ikipatikana ambayo inaweza isiondoe vitisho vya watawala licha ya sheria kuruhusu maandamano?
 
Watu huwa hawako tayari bila kutayarishwa. Cha kujiuliza ni kuwa wametayarishwa? Yuko wapi Raila Amolo Odinga?

Mwone hapa alivyokuwa shupavu:

Screenshot_20230503-042635.jpg

"Same meeting point, same people, same petitions!"

Ruto lazima apate tumbo la kuhara
 
Wakenya wanajielewa, sisi tuliokulia kwenye siasa ya udanganyifu ya ujamaa ni matatizo matupu. Kiongozi wa nchi akizingua ni lazima awajibishwe kwa kufuata Katiba - kupitia demonstrations.
 
Wakenya wanajielewa, sisi tuliokulia kwenye siasa ya udanganyifu ya ujamaa ni matatizo matupu.

Kujielewa huku hakutoki mbinguni.

Vinavyoelea vimeundwa!

Kwetu watu wamehamasishwa ya kutosha kuchukua hatua? Nani anafanya kazi hiyo?
 
Watu huwa hawako tayari bila kutayarishwa. Cha kujiuliza ni kuwa wametayarishwa? Yuko wapi Raila Amolo Odinga?

Mwone hapa alivyokuwa shupavu:

View attachment 2608431

"Same meeting point, same people, same petitions!"

Ruto lazima apate tumbo la kuhara
Lissu ndie Odinga wetu bahati mbaya yupo kimya..
 
Raila Odinga (baba) atakuwapo barabarani leo 0600 kwenye maandamano yaliyoitwa haramu na serikali huko. Kwamba:

1. Wana ujumbe wao kupeleka ikulu
2. Wana ujumbe wao kupeleka hazina
3. Wana ujumbe wao kupeleka tume ya uchaguzi.

Hizo ni ofisi za umma na katiba inawaruhusu kufanya hivyo kwa amani.

"Kwamba gharama za maisha zishuke, shakahola watu walikufa, mishahara jana haikupanda, servers (vyungu) havijafungiliwa nk, ni uvunjifu wa katiba ya Kenya kuyaharamisha maandamano yao."

#Maandamano: Protests will begin at 6am, defiant Raila tells Ruto

Haramu huu wategemee sekeseke na polisi kama kwetu tu awamu ile.

Upande wa pili ni ule wa watawala, yaani Kenya Kwanza. Huu utafanyikia nyumbani kwa rais mataafu wa huko, bwana Uhuru Kenyatta. Kenya Kwanza inamtambua huyu, kuwa ndiyo kinara wa maandamano ya Odinga.
Madai makubwa ya Kenya Kwanza ni Uhuru kutambua kuwa walioko madarakani sasa hivi ni wao, na si yeye. Hivyo awape muda japo wa kupumua basi? Hawa songombingo za polisi kama CCM vile halitawahusu.

CS Kuria: We will hold our own protest outside Uhuru's home

"kumbe wenye kuona ukabila kwenye maandamano ya huko ni sisi tu wa kule Mburahati."
Ukabila wa wakeny uko tanzania tu😅😅
 
Nawakubali sana hawa Jamaa kwa mikakati!
IMG_20230503_151644_647.jpg
 
Back
Top Bottom