Kenya: Kanisa lapewa onyo kwa kupiga kelele usiku, waenda na kipimo alfajiri

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa raia Mkuu wa Idara ya Mazingira Geoffrey Mosiria, ameliomba moja ya kanisa nchini Kenya, kudhibiti kiwango cha kelele ili kuepuka usumbufu kwa jamii.
Mosiria amesisitiza umuhimu wa kanisa hilo kuhakikisha kuwa viwango vya kelele vinazingatia sheria na kanuni za mazingira, hasa katika maeneo ya makazi, ili kudumisha amani na utulivu katika jamii.
1726308438688.png
Ikumbukwe Novemba 27, 2022 Father Charles Kinyua aliwahi kusema "Makanisa ya siku hizi yana kelele sana. Yana kelele zaidi kuliko baa ambako watu huenda kwa ajili ya kunywa pombe," kasisi huyo alisema alipokuwa akiadhimisha Jumapili ya kwanza ya Majilio.

Soma pia;
=> Makanisa kupiga kelele usiku kucha na mchana kutwa Kahama/Lugera
=> Kelele usiku kucha Mtaa wa Alesika, Mbezi Beach kutoka Amigos Pub na Kanisa la Angels Ministry ni kero kubwa, tumechoka!
 
Huku Tanzania ndo wamezidi ni kero haswa kanisa lipo kwenye makazi ya watu halafu kelele wameweka spika kubwakubwa!,muda mwengine huwa najifikiria sijui naishi kwenye jamii gani!.
halafu sio kwamba viongozi hawaoni,ila ni kama wanaacha tu aijui wanaogopa nini..? na nahisi rushwa inachangia utitiri!
jamii huku chini inaozeshwa sana na mambo ya imani watu ukiwaambia wanakuona kama jitu la shetani! Africa sijui tu dah!
 
Ninapoishi cku hz siwashi redio na tv na angaliaa Kwa tabu Sanaa maana nimezungukwa na makanisa 5 matatu ya kilokole mawili n kkkt na katolic hawa hawanaga kelelle na ibada n jpili tu ,ss hawa walokole jmn😅😅😅😅🙏🙏 jtatu mpk jtatu n kelele mpk bc tushashtaki Sanaa tunaitwa ma freemason hatupendi neno la MUNGU aiseee ,kanisa hili wikii n mkutano ,wiki ijayo lingine yaan km yanashindana Kutafuta wauminii na ktk hyo mikutano hakuna ht kinachohubiriwa n utasikia tu jiooooooooniiiiiii ya Leo mbengu zitafunguka
 
"hao kondoo wamesema"😂jamaa aliegizwa kajitahidi mnooo Kutumia ustaraabu nadhani ni kiongozi mzuri sana
 
Baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa raia Mkuu wa Idara ya Mazingira Geoffrey Mosiria, ameliomba moja ya kanisa nchini Kenya, kudhibiti kiwango cha kelele ili kuepuka usumbufu kwa jamii.
Mosiria amesisitiza umuhimu wa kanisa hilo kuhakikisha kuwa viwango vya kelele vinazingatia sheria na kanuni za mazingira, hasa katika maeneo ya makazi, ili kudumisha amani na utulivu katika jamii.
Ikumbukwe Novemba 27, 2022 Father Charles Kinyua aliwahi kusema "Makanisa ya siku hizi yana kelele sana. Yana kelele zaidi kuliko baa ambako watu huenda kwa ajili ya kunywa pombe," kasisi huyo alisema alipokuwa akiadhimisha Jumapili ya kwanza ya Majilio.

Soma pia;
=> Makanisa kupiga kelele usiku kucha na mchana kutwa Kahama/Lugera
=> Kelele usiku kucha Mtaa wa Alesika, Mbezi Beach kutoka Amigos Pub na Kanisa la Angels Ministry ni kero kubwa, tumechoka!

MK254 anaweza kuwa muumini mwaminifu hapo
 
Ninapoishi cku hz siwashi redio na tv na angaliaa Kwa tabu Sanaa maana nimezungukwa na makanisa 5 matatu ya kilokole mawili n kkkt na katolic hawa hawanaga kelelle na ibada n jpili tu ,ss hawa walokole jmn😅😅😅😅🙏🙏 jtatu mpk jtatu n kelele mpk bc tushashtaki Sanaa tunaitwa ma freemason hatupendi neno la MUNGU aiseee ,kanisa hili wikii n mkutano ,wiki ijayo lingine yaan km yanashindana Kutafuta wauminii na ktk hyo mikutano hakuna ht kinachohubiriwa n utasikia tu jiooooooooniiiiiii ya Leo mbengu zitafunguka
😀 😀 😀 😀
 
Hakuna kinachonikera kama Yale makelele ya alfajiri kutokea misikitini.
 
Great!! wonder when will NEMC or any relevant institution wake up to these aspects..
 
Back
Top Bottom