DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
Kenya imeidhinisha rasmi kuanza kutekeleza mfumo wa Recognition of Prior Learning - RPL mfumo ambao unatambua ujuzi wa vitendo na stadi za kazi zilizopatikana nje ya elimu ya darasani na kuutoa kama njia halali ya kupata vyeti na kujiendeleza kielimu.
Hatua hii imeibua mjadala mpana ukanda wa Afrika Mashariki, huku ikifufua hoja ambayo nchini Tanzania imewahi kuibuliwa bungeni mara kadhaa na Mbunge Eric Shigongo.
Eric Shigongo ambaye katika miaka ya karibuni amelisukuma suala hilo kwa nguvu alipolizungumza mara kadhaa bungeni akishinikiza Serikali irejeshe mfumo huo uliositishwa Mwaka 2017.
Katika michango yake Bungeni, Shigongo aliwahi kusisitiza kuwa RPL ni mfumo unaotumika kwa mafanikio katika mataifa mengi na umewezesha watu wenye ujuzi mkubwa lakini wasio na vyeti kutambulika rasmi, kuendelea na masomo au kupata ajira zinazolingana na uwezo wao.
Kutangazwa kwa mfumo huo nchini Kenya mwaka huu imekuwa ni mfano mpya unaoonyesha umuhimu wa RPL katika kuwainua vijana na wabunifu wanaojifunza kupitia vitendo. Kwa hatua hiyo ya majirani zetu, wadau wa elimu na ajira nchini Tanzania wameanza kurejea mjadala wa Shigongo aliyeendelea kusisitiza kuwa maelfu ya Watanzania wana ujuzi wa thamani lakini hukosa fursa kwa sababu tu hawana vyeti.
Swali ambalo sasa linaibuka upya ni kama Tanzania inaweza kuchukua hatua kama ilivyofanya Kenya na kufufua mfumo uliowahi kuonekana kuwa na manufaa makubwa kwa jamii.