Tony254, nilishakujibu yote mwaka Jana kabla hata SGR kipande cha Mombasa Nairobi kumalizika, labda unataka nijibu vile unavyotaka wewe sio vile ninavyoona mimi, ngoja nikukumbushe nilivyokujibu.
Nilisema hivi, katika miradi mikubwa iliyokuwa ikifanyika Kenya, mradi ambao ni muhimu na wenye tija kwa Kenya ni Galana Kulalu na barabara hasa za mashinani. Katika Miradi isiyo na tija kabisaa ni Lamu port/ Bagamoyo port, kwasababu hizi nchi tayari zinazo bandari zinazofanya kazi vizuri sana, hasa Kenya, ilipaswa kuimarisha bandari ya Mombasa, inauwezo wa kukidhi mahitaji ya Kenya for the next 50 years.
Kuhusu SGR ya Kenya sina sababu ya kurudia, kwasasa David Ndii alishamaliza kila kitu, na ukweli unaanza kujitojeza. Kwa kifupi huwa ninashindwa kuwaelewa viongozi wenu kwa jinsi wanavyochukua maamuzi ya kuanzisha miradi ya nchi, sijua hata huwa wabafikiria nini.
Kumbuka ni hawa hawa viongozi wenu walioamua kujenga Greenfield terminal na kuwashawishi wakenya kwamba ni muhimu sana kwa uchumi wa Kenya, wakafikia hatua ya ufunguzi ambapo viongozi na mabalozi wa nchibalimbali walihudhuria, Uhuru Kenyatta akatoa hotuba nzuri sana kuonyesha umuhimu wa huo uwanja kwa nchi na Africa kwa ujumla, three monthly later, rais huyo huyo akasema huo uwanja sio muhimu tena. Hiyo ndio Kenya ninayoijua Mimi.