Hili swala la ushoga ni gumu, linatisha, na sensitive. Ushoga unapingwa na kukataliwa kifamilia, kijamii, na kidini. Ni wazi kuwa kitu chochote kinachokataliwa kifamilia, kijamii, na kidini pia serkali inatakiwa ikikatae au isiwe na sheria zenye kulinda kile kinachokataliwa kifamilia, kijamii, na kidini.
Kwa upande mwingine ushoga upo na ni "real" na upo kila jamii. Kuna nchi ambazo ziko kimya kuhusu ushoga, kuna nchi zenye kuukataza ushoga, na kuna nchi ambazo hazikatazi ushoga. Tanzania, kama nchi zote zilizokuwa chini ya Wainereza zinakataza "sodomy" (ulawiti) ambayo ni tamati ya ushoga. Kumekuwa na ubishi kuhusu ulawiti/ushoga wengi wakisema hii haikuwepo Afrika. Ukweli ni kuwa ushoga una historia dunia nzima Afrika ikiwemo, lakini ushoga siku zote umekatazwa katika mila zetu pamoja na kuwepo.
Katika dini zote pamoja na zile za Kiafrika kumekuwa na katazo la ushoga, lakini hii haina maana haukuwepo. Nchi nyingi, hasa zile za Magharibi, shida imekuwa, kwanza kutambua kuwa ushoga upo, kukubali ushoga siyo koa la jinai, na mwisho shoga awe na haki sawa za kibinadamu kama vile kiutobaguliwa na jamii katika mambo muhimu ya jamii kama vile kupata kazi. Ukweli ni kuwa Afrika hakujawapo na msukumo wa kuwatenga na kuwabaguwa mashoga. Mara nyingi watu wa namna hiyo wamekuwa "ignored" na wao kuishi bila kufuatiliwa. Tatizo linakuja pale ambapo swala la ushoga linakuwa kama la "activist" kama vile kunaubaguzi wowote ambao unawalenga wahusika. Kama mila, dini, jamii, na familia zingapinga ushoga basi ni kawaida wahusika kuomba ukatazwaji wa ushoga.
Mataifa ya Magharibi siku zote yanajisifia kuwa ni mataifa ya Kikristu yanayoendeshwa kufuatana na "christian ethics" kwa mantiki hiyo ni lazima yapinge ushoga. Kitu ambacho siungi mkono ni kwa mfano mtu kunyimwa kazi ambayo ana uwezo, ujuzi, na taaluma nayo eti kwa sababu ni shoga. Mtu kuwa shoga kusmuondolee haki zake za msingi kama binadamu. Lakini pia tupinge ufiraji wa aina yoyote na kkuona kama ushoga. Kwa mfano tusihalalishe ufiraji wa wanawake maana huu ni sawa na nusu ushoga!