Kenya kunani? Matukio ya ajabu kila kukicha

Kenya kunani? Matukio ya ajabu kila kukicha

Mtuache

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
256
Reaction score
658
Polisi nchini Kenya wamemkamata Hellen Wanjiru Weri (62) ambaye anadaiwa kuongoza dhehebu tata nchini humo ambapo anadaiwa kuwashikilia watu 32 kwenye nyumba yake huku wakiwa dhaifu kiafya kutokana na kufunga kula chakula kwa zaidi ya wiki moja

Polisi wanasema watu hao ambao walikuwa katika nyumba iliyopo katika kijiji cha Kamwene 'B' Kihingo, katika kaunti ndogo ya Njoro , wanasemekana kuwa walikuwa dhaifu baada ya kufunga chakula kwa karibu wiki moja

Mwanamke huyo amekamatwa baada ya mwanamke mmoja kudai kuwa binti yake aliacha kazi na kwenda kwa mwanamke huyo kwa ajili ya maombi na kufunga na hakurudi tena nyumbani.
 
Mambo kama haya yakitokea nchini nitafurahi sana
Mwamposa coming soon watu walibebeshwa udongo na wakabeba akawaambia watoe hadi senti yao ya mwisho wajimalize sadaka ya kujimaliza hadi kile Cha mwisho ulichonacho wanakubari wanatoa wanatembea kwa mguu Kawe kuelekea Mbagala akiwaambia wasile wafunge mwezi mzima unafikiri wale vichaa watagoma ?
 
Nikisikia watu atleast 100 hv wameenda na maji nitafurahi mno.
 
'Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa'.
 
Mwamposa coming soon watu walibebeshwa udongo na wakabeba akawaambia watoe hadi senti yao ya mwisho wajimalize sadaka ya kujimaliza hadi kile Cha mwisho ulichonacho wanakubari wanatoa wanatembea kwa mguu Kawe kuelekea Mbagala akiwaambia wasile wafunge mwezi mzima unafikiri wale vichaa watagoma ?
Halafu yeye hajimalizi. Na si kwamba hizo sadaka anaenda kupanua "Huduma" anaenda kujenga hoteli Mbeya.
 
Kuna yule alikua anasema watu waende na mavuzi yakaombewe, Serikali ikampiga Rolex wangemuachia yule ungesikia kaangamiza wajawazito
Eh hy sijaisikia, ilkuwa wapi hy
 
Yesu alifunga siku 40 usiku na mchana.

Na sisi hatuwezi kushindwa. Si eti eeh?
 
Back
Top Bottom