KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

Kenya imeonyesha njia ambayo inaweza kutumika kama footstep kwa karibu labda tz kama wabongo wakikomaa mana uganda,rwanda na burundi hakuna dalili labda masia akirudi mara ya pili huko raisi ni kama kaka yake yesu au mtume!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama za Kenya ziko vizuri Sana na huru

Tatizo la mahakama zetu siyo majaji, ni Katiba. Tatizo letu kubwa ni KATIBA
tatizo sio katiba,tatizo ni majaji,plain and simple,

jaji anapofanya kazi huko anahofia nikifukuzwa kazi wanangu watakula nini,jaji huyo hawezi kutenda haki,
daima atapokea maagizo kutoka juu
 
naomba niwekwe kwenye kumbukumbu,uhuru bado atakua raisi wa kenya!
 
Huu ndo UKUDA wa nchi za AFRICA, Vijana hawana AJIRA, Kina mama wanateseka, PESA ZOTE ZINAPELEKWA Kwenye UCHAGUZI Masikini WANATESEKA. Hata huo UCHAGUZI wa MARUDIO hautakuwa PERFECT

Kwahiyo ulitaka mtu aliyeiba kura atawale eti sbb watu hawana ajira? Uwezo wako wa kufikiri uko chini sana aisee. Yaani kosa lihalalishwe sbb ya ttz jingine? Haya bana kila la heri
 
JF Bwana! kipindi cha uchaguzi waliokuwa upande wa Uhuru eti leo, wanaona Odinga kafanya vema! hahahahahahaha
ni kichaa tu kama wewe ambae hataona umuhimu wa kuwa na vyombo huru katika mihimili ya serikali. Huko Tanzania Majaji wanamuona magufuli kama mungu
 

Huku kwetu tuna "kaimu" jaji mkuu. Ili ateuliwe kuwa jaji mkuu lazima aonyeshe upendeleo kwa chama tawala na serikali yake
 
Kenya nitaendelea kuwaheshimu daima. Kwa Africa Mashariki na zaidi kwa Africa mmeonyesha kupiga hatua kubwa kidemokrasia kwa uamuzi huo wa mahakama.
 
Sisiemu ijifunze kuwa tume huru ya uchaguzi na matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani ni nguzo muhimu kwa ukuaji wa demokrasia. Ubakaji wa demokrasia ni kudumaza maendeleo ya nchi...
 
Mahakama kama haitawachukulia hatua walioharibu uchaguzi wao nao watakua mabwege. Tia kolokolon adabu iwepo, vinginevyo watafanya uchaguzi kila siku.
 
Hakika katika Africa Kenya ni nchi yenye demokrasia,wantanzania tunatakiwa tujifunze kitu hapa,mahakama nchini kenya imeonyesha mfano wa kuigwa.
 

Mkuu nafikiri uwepo mahakama huru, tume huru ya uchaguzi, katiba sahihi.. Sidhani kama hawa wapinzani wa Tanzania wataendelea kuandamana..
 
Watanzania tunalo la kujifunza kutoka Kenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…