KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

Hakika Kenya kuna wanaume! Sio kama nchi ile yenye watu wanaoshinda vibarazani kuzungumzia ya udaku na mpira.
 
Itakumbukwa Tanzania kwa upande wa Zanzibar tulifanya uchaguzi wa marudio wa rais baada ya ule uchaguzi mkuu wa 2015 kufutwa

Chakushangaza dunia Maalim Seif alisusia, na CCM ikafanya uchaguzi na kushinda kwa kishindo

Maalim hapa unatakiwa ujifunze, sio kususa tu
kama kweli umeshinda utashinda tena na tena uchaguzi utakaporudiwa

Lakini tofauti hapa kwetu ni katiba kutokuruhusu matokeo ya uchaguzi wa rais kupingwa mahakamani, hivyo Maalim ulitakiwa urudie uchaguzi tu kulingana na taratibu zetu
 
Ni wakati kujiuliza kwamba ni lini CCM watafanya Tanzania kuwa na mahakama huru kama Kenya; wala siyo aibu kwa Chadema ni Muda wa Chama tawala kujifunza!!
 
unafiki utawaua hao jamaa.
leo ingekuwa kete yao hata jf ingezima kwa wingi wa threads na comments
 
Na sisi turudie uchaguzi Tz kwa kuwa haukuwa HURU na HAKI
 
Sio Kenyatta, ni Lowasa alimfuata na kumshobokea kwa niaba ya UKAWA, sasa aibu juu ya nyumbu.
warudie kuwaridhisha tu NASA awamu hii KENYATTA atamwacha Odinga kwa kura nyingi sana hata zaidi ya m2.5
 
Alafu Kenya hamna sikukuu ya Eid? Mbona mahakama inafanya kazi leo
 
Mimi nilishangaa sana. Ile percent ya ya kura za Uhuru Kenyata na Raila ilikuwa ni 54.24 na 44.32. Haishuki wala haipandi kila kura zikihesabiwa au kuletwa kutoka hata kama poling station ni moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maamuzi haya ni ushahidi kwamba there are still Honorable persons in this world.

Sahihi kabisa, ila wachache sana. Kwa hapa Tanganyika unaweza kukuta hakuna
 
Uhuru Kenya ameuthibitishia ulimwengu kwamba sio kila mtawala wa Afrika ni kikohozi na kikojozi, bali pia Afrika ina VIONGOZI. Uhuru alikuwa na uwezo wa kuvuruga mwenendo wa kesi na kuiminya mahakama. Ila ameacha muhimili uchukue nafasi yake.

HONGERA UHURU KENYATTA. Wewe ndio jembe.
 
Back
Top Bottom