KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

Kuwa Jydge Tanzania ni Usakala mtupu. Unakua na Judge kama Warioba anafanya kazi kiueledi kabisa halafu anashambuliwa na kupingwa, baadaye anaitwa meza kuu anaanza kupingana na kile al8chokua akikiamini. Eti Magufuli anatosha. Yaani all over sudden Magufuli anakua ni mtu bora kabisa kuliko Katiba.

Damn
Njaa mbaya sana
 
Mahakama za Kenya ziko vizuri Sana na huru

Tatizo la mahakama zetu siyo majaji, ni Katiba. Tatizo letu kubwa ni KATIBA
 
akili zako we jamaa hatar tupu kwa kuwa ni mpinzani basi wapinzani wanatakiwa kumuunga mkono hii mpya tanzania bana kwa hiyo magufuli kahuzunika natokeo ya uhuru yalivyofutwa kwa kuwa uhuru sio mpinzani.
Ishu ni kama kawaida, kutokuwa na msimamo! Mlimsapoti odinga, ghafla mkamtupa kisa kapiga picha na Magufuli!
 
Je NASA itakubali uchaguzi wa marudio kusimamiwa na hiyo hiyo IEBC ambayo ndio wachafuzi? Naona Serikali ya mpito Kenya. Nusu mkate reloaded!
 
Tanzania tume ya uchaguzi ikimtangaza mtu mshindi urais, hakuna kupinga mahakamani.

Ujima tu.

Sent from my Kimulimuli
 
Mtoa mada ungejielimisha kidogo kabla ya kujifedhehesha kiasi hiki, unalinganisha kenya na zanzibar? You are not serious

sent from my Sony Xperia using jamii forums mobile app
 
Duh..majaji wanatumia kiingereza kigumu mimi sjaambulia kitu
Sio kigumu kiivyo. Katika kusaidiana na kuelimishana.....nenda kwenye GOOGLE TRANSLATE...weka English na Swahili, kopi maneno ya kiingereza ukaya-paste huko na itakutafsiria kwa kiswahili....
 
Tunasimamia pale pale kwamba Kenyatta ameonyesha demokrasia ya hali ya juu.
1.Ameipa Mahakama haki yake ya kutoa maamuzi bila uoga tofauti na hapa kwetu Mahakama itoa order usivunje nyumba unaenda kubomoa halafu unasema haukujua.
2.Alisema atakubaliana na maamuzi ya Mahakama nayo ni kwa rais anayejua nini maana ya Demorasia kuliko wa kwetu wameshindwa bado wakaamrisha kufuata uchaguzi.

CCM jifunzeni toka Kenya.
Uhuru hana mamlaka ya kuipa uhuru wa maamuzi Mahakama. Hata hapa kwetu Magufuli hana hayo mamlaka kwani angekuwa nayo Lisu angekuwa hapati ushindi Mahakamani au angekuwa aliishafungwa siku nyingi.

Sasa kwa maamuzi ya Mahakama ni aibu kwenu chadema kwani mlifurahia sana ushindi wa Uhuru wakati haukuata misingi ya kidemokrasia ambayo mmekuwa mkisema huku Tz haifuatwi....sasa watanzania hatuwaelewi.
 
CHADEMA ilijipambanua wazi kuungana na mwizi Uhuru kwa keti dhaifu sana ya kumkomoa Raila.

Wengi walisema, imekosea. Imekosea kwa sababu wao ni wapinzani na si watawala.

Nasema CHADEMA ni aibu na wanatetea wezi kwa kiwango hiki. Tunawambia kila siku, chama kisiendeshwe na mtu ila sera za pamoja na zinazojisema zenyewe. Kitendo cha Lowassa kutaka kutumia chama kujitukuza matokeo yake ni kukosa mwelekeo.

Lowassa anatafuta utukufu wake binafsi na sasa matokeo yake tunaona.

Mfumo huu wa CHADEMA wa kutetea hata uovu iwe fundisho.

Mwenyekiti aamuke na kuendesha chama kama taasisi na si matamko ya watu au fikra zao.
 
Kama huo uamuzi wa mahakama utafuatwa...bac Kenya watakua mfano wa kuigwa Africa..hasahasa si watanzania, tujufunze kuheshimu mahakama na kutokuingilia maamuzi ta mahakama..
Kenyatta...nae anapaswa kupongezwa....sababu angekua kiongozi wa Kiimla hata hiyo kesi kupelekwa mahakamani isingefika....Chukulieni mfano wa hapa kwetu....mara uchaguzi unafutwa ovyoovyo....etc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama za Tanzania haiwezi kufanya kitu kama hiki walichokifanya Kenya....
Kikatiba, matokeo na uchaguzi wa rais tanzania hauwezi pingwa au amriwa na mahakama!

Kwa kilichotokea tz na kenya maalim seif lazima atakuwa anajutia maamuzi yake
kwani angerudia uchaguzi angeshinda kama ilivyo kwa Uhuru kakubali na atashinda tena

D.A "Mwanaume mashine"
 
Back
Top Bottom