Kenya: Mwanamke akamatwa kwa kuishi na wanaume wake wawili ndani ya nyumba moja

Mwanamke huyo amekamatwa baada ya majirani kulalamika na kutaka mamlaka husika kumchukulia hatua wakidai kitendo hiko sio sahihi.

Chifu wa eneo hilo David Onyango amesema kwamba mwanamke huyo amekuwa akiishi na waume hao wawili kwa pamoja kama waume zake wa ndoa, kwa muda wa wiki mbili sasa ndani ya nyumba moja.

Ndoa hiyo ya mitala kwa wanaume hao ilitokea pale baada ya Maurine ambaye aliolewa na Robert Ochieng ambaye pia amezaaa naye watoto wawili, kurudi nyumbani akiwa na mpenzi mpya aliyetambulika kwa jina la John Ochola aliyempata kwenye shughuli zake za kuuza samaki huku akimtaja kuwa mteja wake muaminifu, na kuamua kuishi nao wote kwa pamoja.

Chifu huyo ameendelea kwa kusema kwamba wanachunguza ni kwa namna gani watatu hao wamekubaliana kuishi ndani ya nyumba moja, na kwamba ndoa hiyo ya pili ya Maurine na John imethibitishwa na mama wa John ambaye amekiri na kusema kwamba mkwe wao huyo huwa anaenda mara kwa mara kuwatembelea nyumbani kwao.

Hata hivyo uongozi wa kijiji umesema kwamba hakuna sheria ambayo inaweza kutumika kuwashtaki, isipokuwa wataangalia namna ya kuwatenganisha watatu hao, ili kuepusha majanga yoyote ambayo yanaweza tokea.
 
It is known as polyandry. Ujinga wa Watanzania wengine ni kukosa uelewa wa kinachoendelea duniani kwa kuwa this is a normal thing in different cultures around the globe...but Danganyika uchanganye na Tanzagiza kisha uongeze LDC na Maji Maji rebellion upate most stupid Africans to ever roam this continent.
Lakini hayo yametokea Kenya
 
And this is wrong how? Whatever consenting adults decide to do in their bedroom is none of anyones business. Live and let live
 
Sasa kuna ubaya upi, jamaa wamekubali kuishi ivyo. Majiran tupunguze wivu jamani
 
‪Maurine Atieno wa Kenya amekamatwa na Polisi nchini humo baada ya kuonekana akiishi na Waume wawili Robert Ochieng na John Ochola ndani ya nyumba moja, inaelezwa Maurine amekuwa akiishi na Waume wake hao ambao pia wamekamatwa ndani ya nyumba 1 kwa wiki 2 sasa.

Mwanamke huyo amekamatwa baada ya majirani kulalamika na kutaka mamlaka husika kumchukulia hatua wakidai kitendo hiko sio sahihi.

Chifu wa eneo hilo David Onyango amesema kwamba mwanamke huyo amekuwa akiishi na waume hao wawili kwa pamoja kama waume zake wa ndoa, kwa muda wa wiki mbili sasa ndani ya nyumba moja.

Ndoa hiyo ya mitala kwa wanaume hao ilitokea pale baada ya Maurine ambaye aliolewa na Robert Ochieng ambaye pia amezaaa naye watoto wawili, kurudi nyumbani akiwa na mpenzi mpya aliyetambulika kwa jina la John Ochola aliyempata kwenye shughuli zake za kuuza samaki huku akimtaja kuwa mteja wake muaminifu, na kuamua kuishi nao wote kwa pamoja.

Chifu huyo ameendelea kwa kusema kwamba wanachunguza ni kwa namna gani watatu hao wamekubaliana kuishi ndani ya nyumba moja, na kwamba ndoa hiyo ya pili ya Maurine na John imethibitishwa na mama wa John ambaye amekiri na kusema kwamba mkwe wao huyo huwa anaenda mara kwa mara kuwatembelea nyumbani kwao.

Hata hivyo uongozi wa kijiji umesema kwamba hakuna sheria ambayo inaweza kutumika kuwashtaki, isipokuwa wataangalia namna ya kuwatenganisha watatu hao, ili kuepusha majanga yoyote ambayo yanaweza tokea.

Chanzo Eatv News

View attachment 877530
Jamaa mbona wanaonekana kama wabwia unga
 
uchi wa kwake," yeye mwenyewe na hao wanaume wake wameridhika," hiyo hali".... so hao majirani iweje waone wivu
 
Sijui kwanini Waafrica hua tunapenda sana kuingilia privacies za watu....

Tunasikitisha sana.
 
It is known as polyandry. Ujinga wa Watanzania wengine ni kukosa uelewa wa kinachoendelea duniani kwa kuwa this is a normal thing in different cultures around the globe...but Danganyika uchanganye na Tanzagiza kisha uongeze LDC na Maji Maji rebellion upate most stupid Africans to ever roam this continent.
MTz gani inayemzungumzia hapa?
 
Back
Top Bottom