Wengine hata passport hawana lakini unawaripoti wapi kwa mfano, kama tu TISS yenyewe inapoteza imani kwa raia taratibu ila kwa uhakika, polisi ndiyo basi kabisa, JWTZ na yenyewe inazidi kutumika kisiasa na kupoteza muono wa kulinda taifa na kubaki nyenzo ya tabaka tawala tu.
Mimi nakutana nao sana lakini siwezi kuwaripoti kwa watu ambao wanajilinda wao badala ya kulinda taifa na raia wake. Acha tu wawafanyie ujasusi maana Tanzania si yetu tena bali ya kikundi cha watu fulani wanaojiona miungu watu.