Tetesi: Kenya na Uganda zinapenyeza majasusi kupitia shule za binafsi Tanzania

Tetesi: Kenya na Uganda zinapenyeza majasusi kupitia shule za binafsi Tanzania

Naiona Tanzania ikiwa kisiwa .
Tukoanza kuwabagua waafrika wenzetu kwa kweli tutakua watu wa ajabu sana.
Timekumbatia Wachina wasio na faida yoyote kwetu kama waafrika na hatuna hata chembe ya vinasaba nao lakini tunaanza kujenga Chuki dhidi ya ndugu zetu kwa sababu tu ya kuwa na mipango isiyoridhisha ya kukuza uchumi na ajira.

Mungu tunusuru na hii roho ya unaguzi inayopandikizwa miongoni mwetu mana kesho watasema kabila Fulani waondolewe kwenye shule za mkoa Fulani.
Mbaya sana.
Ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu.
 
tena wanapewa na ukuu wa shule kabisa. Serikali iwe makina. Selikari iliwahi kusema kazi zinazoweza kufanywa na watanzania. Zisiajili wageni.! Hivi Hakuna watanzania wanaoweza kuwa wakuu wa shule!?
Ndio maana munaambiwa mujenge mazingira ya dunia kuwa kama kijiji ili na sisi tuende S.A ,Kenya,Rwanda ,Kongo,Burundi n.k mana kuna faida kubadilishana watoa taaluma.
Simshabikii wala kumuunga mkono Mleta Mara mana ni mbaguzi na anataka kuumaza kiwango cha elimu ya watoto wetu.
Shule binafsi zinajitegemea kama vamekosa nafasi aende Serikali ni asubiri ajira zenye huo mfumo wa wazawa.

Mwisho tutaomba na Kabisa kubwa la kidunia lililojaa wazungu kuwachunguza mana tuaanza kuwaita majasusi.
 
MUNGU
Naikumbusha serikali ifwatilie shule za private zinazofundishwa na wakenya na waganda kuna mashushushu wengi sana wanatupeleleza kutokujua kwetu kingereza ni upenyo wa wenzetu kuingiza majasusi hatari kwa usalama wa taifa letu nimewatambua baadhi ninaoishi nao mtaani wana mienendo isiyo ya kawaida tiss kuweni makini
TISS imara ilikuwa enzi za Mwalimu,tiss ya sasa ipo busy kuilinda CCM
 
Mkuu mada niliyoileta ni genuine cc ni wa Tanzania kukitokea lolote ovu dhidi ya jamhuri tutaungana chini ya jpm bila kujali hata kidogo tofauti za itikadi ila napenda kujua hii kitu ya Russia spy wing in USA
Porojo tu. Acha uzushi ndugu. Jifunze kuamini kuwa dunia hii maisha ni utandawazi na utandawazi ndiyo maisha. Kama kuna mtu / mwalimu specific unaeamini kwamba ni jasusi basi kamripoti huyo huyo kwenye mamlaka husika kama ambavyo ungemripoti mhalifu yoyote mwingine katika jamii badala ya ku generalize kwamba eti walimu wanaotoka nchi hizo ni majasusi. Wangekuwa ni majasusi kweli ndiyo wawe wanaishi nchini bila vibali, woga na kujipendekeza kwa viongozi au wamiliki wa shule kama baadhi ya wachangiaji walivyodai? Si serikali za nchi zao zingekuwa zinawawezesha kupata nyaraka zote muhimu ili waweze kupata vibali vya kufanya kazi nchini? Na pia wangekuwa na uhakika wa kuwa na ajira ya kueleweka ya ujasusi katika serikali za nchi zao iweje waishi kwa woga au kujipendekeza kwa viongozi au wamiliki wa shule wakati hawana cha kupoteza hata wasipoendelea kufanya kazi katika shule hizo?

Kama wewe ni mwalimu na kiingereza chako ni cha kuungaunga kama mimi hapa usianze fitina kwa hao walimu wenzio badala yake tenga muda wako kujifunza zaidi kiingereza ili hatimaye uweze kufaidi mema yanayotokana na uwezo mkubwa wa kuongea na kuandika kwa lugha hiyo.

Ikikupendeza ujibu hii post yangu kwa majibu yaliyoshiba na si kwa sentensi moja kwa kiingereza ili tuanzie hapo.
 
Na wengi hawana vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini.Wenye shule huwa wanawaficha wakati wa ukaguzi
 
Labda tu kwa sababu ya soko huria lkn sioni kipya ambacho wana ki deliver hawa wakenya na waganda ambacho watanzania hawakiwezi. Ni kasumba tu
 
You deserve a pet. Habari hizi ni muhimu kupitia kiasi. Wahusika tafadhali msichelewe kuzifanyia kazi.
 
Wana mienendo gani hao uliokutana nao? Ili na sisi tukikutana na wengine maeneo yetu huku tuweze ku connect dots na kuwabaini.
Halafu mtawafanya Nini wakati serikali imewapa vibali vya kuishi na kufanya kazi? Litakalofuata ni kuambiwa waongo na mnachuki binafsi
 
Labda tu kwa sababu ya soko huria lkn sioni kipya ambacho wana ki deliver hawa wakenya na waganda ambacho watanzania hawakiwezi. Ni kasumba tu
Kosa letu ni tangu 1967 tulipobadili lugha ya kufundishia elimu ya msingi kwa shule za serikali. Na hapo ndipo waKenya na waUganda wanapopata chati ya kufundisha ktk English medium zetu. Kwani walimu wetu wengi kwa asilimia kubwa si wazuri ktk English. Hasa cha kuongea , Na ni kwa sababu ya msingi wetu wa elimu ulivyokuwa huko nyuma .

Kiswahili ni kweli imetuunganisha waTz , lakini tunakuwa ma bubu nje ya mipaka yetu. English is an international
 
Naikumbusha serikali ifwatilie shule za private zinazofundishwa na wakenya na waganda kuna mashushushu wengi sana wanatupeleleza kutokujua kwetu kingereza ni upenyo wa wenzetu kuingiza majasusi hatari kwa usalama wa taifa letu nimewatambua baadhi ninaoishi nao mtaani wana mienendo isiyo ya kawaida tiss kuweni makini
Watatuharibia watoto wetu Walimu wa kigeni upenda kupenyeza mambo ambayo hayana msingi mzuri kwa kizazi hiki.
 
Mna nini cha kupelelezwa? Huo ni wivu wako tu kwa wanaofundisha English. Ungekuwa na uwezo wa kuangalia the bigger picture ungebaini kwamba in the next 5-10 years, hao watoto waTZ wanaofuzu kutoka kwenye hizi shule za English medium watakuwa na uwezo wa kufundisha kiingereza kwa hivyo shule hazitawahitaji wageni kufunza. Rwanda na Ethiopia pia zimeajiri walimu wengi kutoka Kenya wa English ila wenyeji wameanza kuchukua nafasi hizo baada ya kuhitimu. Ati majasusi, hahaha
 
Na wengi hawana vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini.Wenye shule huwa wanawaficha wakati wa ukaguzi
Hilo kweli lipo na si kwa upande wa walimu pekee yao bali hata katika sekta zingine. Lakini haihalalishi madai ya mleta hoja kwamba ni majasusi. Mimi ninachoamini ni kwamba wangelikuwa ni majasusi kweli waliotumwa na serikali zao hizo serikali zao zisingeshindwa kuwaandalia nyaraka zote muhimu ili kuwawezesha kupata vibali vya kuishi na kufanya kazi bila usumbufu na hivyo kufanikisha lengo la serikali yao la kufanya ujasusi.
 
Naikumbusha serikali ifwatilie shule za private zinazofundishwa na wakenya na waganda kuna mashushushu wengi sana wanatupeleleza kutokujua kwetu kingereza ni upenyo wa wenzetu kuingiza majasusi hatari kwa usalama wa taifa letu nimewatambua baadhi ninaoishi nao mtaani wana mienendo isiyo ya kawaida tiss kuweni makini
Safi sana wakenya na Uganda sisi wa kwetu wanapambana na chadema kwanza
 
Porojo tu. Acha uzushi ndugu. Jifunze kuamini kuwa dunia hii maisha ni utandawazi na utandawazi ndiyo maisha. Kama kuna mtu / mwalimu specific unaeamini kwamba ni jasusi basi kamripoti huyo huyo kwenye mamlaka husika kama ambavyo ungemripoti mhalifu yoyote mwingine katika jamii badala ya ku generalize kwamba eti walimu wanaotoka nchi hizo ni majasusi. Wangekuwa ni majasusi kweli ndiyo wawe wanaishi nchini bila vibali, woga na kujipendekeza kwa viongozi au wamiliki wa shule kama baadhi ya wachangiaji walivyodai? Si serikali za nchi zao zingekuwa zinawawezesha kupata nyaraka zote muhimu ili waweze kupata vibali vya kufanya kazi nchini? Na pia wangekuwa na uhakika wa kuwa na ajira ya kueleweka ya ujasusi katika serikali za nchi zao iweje waishi kwa woga au kujipendekeza kwa viongozi au wamiliki wa shule wakati hawana cha kupoteza hata wasipoendelea kufanya kazi katika shule hizo?

Kama wewe ni mwalimu na kiingereza chako ni cha kuungaunga kama mimi hapa usianze fitina kwa hao walimu wenzio badala yake tenga muda wako kujifunza zaidi kiingereza ili hatimaye uweze kufaidi mema yanayotokana na uwezo mkubwa wa kuongea na kuandika kwa lugha hiyo.

Ikikupendeza ujibu hii post yangu kwa majibu yaliyoshiba na si kwa sentensi moja kwa kiingereza ili tuanzie hapo.
Mwambie akajifunze kichina mana muda sio mrefu Afrika itakua koloni la China . Kinge wenzake walishakijua mapema.

Sisi tusioipenda China na Mifumo yake ya kibaguzi tunahitaji watoto wetu wapate walimu bora kiufundishaji . Ulaya na Canada wanaupungufu mkubwa wa nguvu kazi na maviwanda yapo kibao wanahitaji nguvu kazi toka Afrika. Tunaandaa watoto wetu kuhamia huko . Yaye abaki na siasa za chuki na ubaguzi dhidi ya ndugu zetu na marafiki zetu Wakenya.
Wakenya ni watu poa sana kwenye kutoa huduma kwa jamii hawana maringo na mapozi ya kijingajinga.

Anasema eti Ujasusi anafikiri ni rahisi kihivyo kuingia nchi jirani na kufanya ujasusi, ajaribu kwenda kufanya ujasusi Hata Hapo Namanga tu tena wala asivuke boda wiki moja atatiwa nguvuni na Watanzania wenyewe ili ajue kuwa TISS sio Musiba.
 
Halfu wakati wa uchaguzi wa 2015 wote waligeuka wapiga debe wa Lowassa. Pamoja na hawa wanaokuja kwa kivuli cha dini! Hata magazeti mengi ya Kenya na wachambuzi wao wanapenda kurusha madongo sana kwa rais wetu.
Majungu kama yepi mkuu taja hata 2
 
Back
Top Bottom