Kwenye hili, pamojana kwamba umri wangu si haba. Yeyoteakiitishamaandamano yakupinga huu mkataba wa kishenzi, nami nikiwepo nchini, nami nitashiriki, liwalo na liwe.
Swela hela. Miaka 55 si haba. Mkwawa aliondoka bila kufikia hata umri huu. Aliona aheri kimtokee chochote kuliko kudhalilishwa.
Vanyalukolo va Kulilinga, watani zangu Nyumbihi bombihi,na wananzengo wa pale Tabora, ule ujasiri wa baba zetu akina Mkwawa, Chabruma na Isike, tumeutupia wapi hata tukabakia mapakacha tu?
Baba zetu, kukiwa hakuna duka la simu, duka la panga wala nyu do wala sululu, mzungu akiwa ana bunduki mpaka mizinga, bado walipambana mpaka kufa kulinda rasilimali zao, utu wao na heshima yao. Leo tukiwa na kila kitu, tunaogopa rungu la polisi au mahabusu! Tumerogwa na nani? Yaani hata ile tofauti ya mwanaume na mtoto, tofauti ya mwanaume na mwanamke, i.ebakia tu kwenye mavazi, lakini siyo vitendo.
Wanaume kamili kabisa, 10,000 tu wakisema huu mkataba wa kijinga hautekelezwi kwenye ardhi hii ya akina Mkwawa, Isike, Chabruma na Mirambo, huo upuuzi hautafanyika. Tumekuwa legelege mno, kiasi mpaka cha kugikia kuchezeshwa shere na akina mama, na sisi tukiogopa, eti tutawekwa mahabusu.
Mbowe alisema akirudi tu atalianzisha. Arudi haraka, atangaze maandamano ya kupinga mkataba wa kishenzi ni lini, tujiandae.