Muache aende zake Kenya is bigger than him.Huyu jamaa amekuwa akifikiri ataiteka nyara Kenya kila wakati hadi apate chake.Tumechoka na uchaguzi usio na mwisho ,uharibifu wa mali ,maandamano na kuhujumu uchumi ili tu mtu mmoja apate mamlaka.Go home and never come back Fake Joshua.Bora astaafu siasa kwa heshima maana kushinda uchaguzi wa marudio ni ndoto!
Vyama vya upinzani kama vingesusa chaguzi zote tangu hiyo 1995, unafikiri ingesaidia kukuza demokrasia ya nchi yetu.
Kila jambo kuhusisha chadema ni sawa na kichaa , ukabila usikupumbaze kiasi hicho mkuu , iko siku utakuja kutuomba radhi mjomba .Kama hana imani na tume basi kafanya jambo jema [kama habari ni ya kweli].
Huku kwetu CHADEMA huwa wanashiriki chaguzi za NEC halafu wakishindwa wanaanza kudai tume haiko huru.
Kila jambo kuhusisha chadema ni sawa na kichaa , ukabila usikupumbaze kiasi hicho mkuu , iko siku utakuja kutuomba radhi mjomba .
Umesoma vizuri lakini alichosema Odinga, amehamasisha pia wafuasi wake waandamane unajuaSidhani kama umewahi hata kupitia machapisho ya kuanzishwa ICC. Kujitoa kunahusikaje na ICC
kweli kabisaAfrica ni shida sana yaani
Kwa sababu ni mvivu wa kusomaHuyu jamaa haeleweki anataka nini
Raila Odinga ajiondoa kugombea urais wa Kenya, kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 26, 2017
Miongoni mwa sababu kubwa za kujitoa ni;
- Wamehisi kuwa IEBC haina nia ya kuhakikisha yale makosa yaliyosababishwa kufutiliwa mbali matokeo ya urais Augost 8 kuwa hayatajirudia tena.
- Pia wameona wapianzani wa Jubilee wataka kufanyia Katiba mapinduzi na kurudisha udikteta, wanaona kuwa Jubilee wanataka tu kuwe na uchaguzi ila wao wanataka uchaguzi bora
- Pia IEBC kutokufuata masharti waliyotoa ambayo yangeakikisha kuwepo kwa uchaguzi bora na wa haki
Raila Odinga akiongea na waandishi wa habari amesema;
“Kwenye demokrasia ya Kikatiba, hatakiwi kulumbana kuhusu uchaguzi huru na wa haki. Tulitakiwa tushirikiane kwa kufanya kazi pamoja kuhakikisha tunashikilia maadili haya ambayo sio tu maadili ya taifa letu bali pia ni msingi wa mfumo wa uchaguzi wa kuaminika”
"Tumeshinda vita ya demokrasia ya vyama vingi na ya Katiba mpya. Tutashinda vita ya uchaguzi huru na wa haki"
Wakati huo huo, Raila Odinga amewataka wafuasi wake nchi nzima kuandamana kesho kupinga kitendo cha Tume ya Uchaguzi kugoma kubadili uongozi wake.
Baada ya Tamko hilo, Mbuge Ndindi Nyoro amesema;
Kwanza mimi nafurahi sana vile amejiondoa kwa sababu ni kuonyesha wakenya ya kwamba vile tumekuwa tukisema kama watu wa Jubilee, NASA haijawahi kuwa ready kwa elections. Tulianza 8 august even before that walikuwa wanashinda kortini kulalamika huko.
Hii ni kwa sababu hawa-take any chance ya ku-face wakenya.
Maoni yangu ni kumuapisha rais wetu Uhuru, kwa sababu hatuwezi kuwa na mtu mmoja kwa sababu ya greedy yake ya kuongoza watu anazungusha nchi yetu kila siku
Uhuru Kenyatta amemjibu Raila kwa kusema hivi
===============================================================================
Tamko la NASA kujiondoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi, 26 Oktoba 2017
Kuandamana kunampeleka mtu ICC? In fact hayo maandamano hayana nguvu....ni sehem ndogo ya Kibera, kisumu na mombasa.Umesoma vizuri lakini alichosema Odinga, amehamasisha pia wafuasi wake waandamane unajua
Kaka upo sahihi kabisa, lakini senario hii kwa nchi yetu bado saana, CDM kwa namna yoyote siwashauri wasisuse uchaguzi wowote ule hata huu ujao wa 2020, kwa mazingira yetu ni bora ushiriki upate utakachopata then ulalamike. Ukisusa CCM wanakomba mboga zote na hutaenda kushitaki popote.Hususi tu bila sababu.
Unasusa kwa sababu ya/za msingi ili kumulika kasoro kwa lengo la kutanabahisha umma na kutia shinikizo la mabadiliko au marekebisho.
Wewe humjui huyu jamaaa.Kila kitu kwake ni malalmiko,kuanza vitisho na kuchochea.Hakuwa na imani na tume ya uchaguzi ,hana imani na KDF ,hana iamani na jeshi la polisi ,hana imani na chochote serikali inachofanya na hii tume mpya ndiye alifanya ichaguliwe juzi ati sababu hakuwa na imani na ile tume ilyovunjwa.Alichofanya ni sahihi kabisa kama hana imani na tume ya uchaguzi.
Jambo ambalo nimekuwa nikiwashauri wapinzani wa Tanzania kwa muda mrefu.
Kwa nini mtu ushiriki uchaguzi unaoendeshwa na tume ambayo huna imani nayo?