KENYA: Raila Odinga(NASA) ajitoa kugombea urais wa Kenya uliokuwa ufanyike 26 Oktoba, 2017

KENYA: Raila Odinga(NASA) ajitoa kugombea urais wa Kenya uliokuwa ufanyike 26 Oktoba, 2017

8257fdfbffd8cbec5480157dca9918a1.jpg
 
Raila ameona hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoka kwenye siasa akiwa bado ana heshima!
 
Nilitarajia Raila sio kichaa na nikweli sio kichaa.
Ukichaa= Kufanya jambo lilelile kwa njia zilezile ukitarajia matokeo tofauti.
Kama tatizo ilikua ni uwajibikaji wa tume kusimamia uchaguzi kwa mujibu wa sheria , ni nini kilisababisha mwanzo wasiwajibike na kuufanya uchaguzi uishe kwa haki?

Ili uchaguzi uwe wa haki lazima washiriki wa uchaguzi wawe na imani na wasimamizi wa uchaguzi la si hivyo tutaona matatizo makubwa punde baada ya uchaguzi.
Ukiona tume sio huru na hauiamini ukaingia kwenye uchaguzi ili ukiisha uchaguzi uanze kulalamika huo ni utoto na ni upotevu wa nguvu bila msingi.
 
Wewe humjui huyu jamaaa.Kila kitu kwake ni malalmiko,kuanza vitisho na kuchochea.Hakuwa na imani na tume ya uchaguzi ,hana imani na KDF ,hana iamani na jeshi la polisi ,hana imani na chochote serikali inachofanya na hii tume mpya ndiye alifanya ichaguliwe juzi ati sababu hakuwa na imani na ile tume ilyovunjwa.
Kwa hapa Tanzania upinzani wana imani na nini kati ya hivyo ulivyovitaja?
 
Kila jambo kuhusisha chadema ni sawa na kichaa , ukabila usikupumbaze kiasi hicho mkuu , iko siku utakuja kutuomba radhi mjomba .
Mwenzenu anajitoa kwakuona hakuna lolote atakalopata chini ya tume ileile.. Ninyi mnashiriki alafu bado mnalalama
 
I can smell a burning fish coming from Kisumu,African democracy at its best behavior.
 
Alichofanya ni sahihi kabisa kama hana imani na tume ya uchaguzi.

Jambo ambalo nimekuwa nikiwashauri wapinzani wa Tanzania kwa muda mrefu.

Kwa nini mtu ushiriki uchaguzi unaoendeshwa na tume ambayo huna imani nayo?
Fuatilia vizuri toka apate ushindi mahakamani kama alikuwa ni mgombea wa kweli au sanaa tu kwasababu alijuwa atashindwa tena!
 
Nilitarajia Raila sio kichaa na nikweli sio kichaa.
Ukichaa= Kufanya jambo lilelile kwa njia zilezile ukitarajia matokeo tofauti.
Kama tatizo ilikua ni uwajibikaji wa tume kusimamia uchaguzi kwa mujibu wa sheria , ni nini kilisababisha mwanzo wasiwajibike na kuufanya uchaguzi uishe kwa haki?

Ili uchaguzi uwe wa haki lazima washiriki wa uchaguzi wawe na imani na wasimamizi wa uchaguzi la si hivyo tutaona matatizo makubwa punde baada ya uchaguzi.
Ukiona tume sio huru na hauiamini ukaingia kwenye uchaguzi ili ukiisha uchaguzi uanze kulalamika huo ni utoto na ni upotevu wa nguvu bila msingi.
Yule bwana alishindwa ktk chaguzi za ngazi zote! Aliokolewa na mahakama iliyo amua kesi kwa misingi ya ukabila. Toka day one baada ya hukumu hajawahi kuonyesha kama atagombea sasa anaelewa kwamba alishindwa kihalali. Tatizo lake ni kuendelea kuwadanganya Wajaluo wenzake anaweza kushinda urais huku akiwatukana Wakikuyu na washirika wao!
 
Fuatilia vizuri toka apate ushindi mahakamani kama alikuwa ni mgombea wa kweli au sanaa tu kwasababu alijuwa atashindwa tena!
That's a lame excuse.

Raila does have some very valid points.

The same people who screwed up the first election can't run the rerun election!

It's just common sense.
 
October 10, 2017
Nairobi, Kenya

"Consequence of a withdrawal means there will be no elections on the 26th October 2017 in Kenya " Felix Owuor

Source: KTN News Kenya
 
October 10, 2017
Nairobi, Kenya

Hatua ya Odinga kujiondoa yaacha wanasheria wakikuna vichwa

Kujiondoa kwa Raila Odinga kutoka kwenye kinyang’anyiro cha urais sasa kumeibua masuali ya kisheria kuhusu hatma ya uchaguzi uliokuwa umepangiwa kufanyika tarehe 26 Oktoba 2017.

Muungano wa NASA ukiegemea uamuzi wa mahakama ya upeo (Supreme Court) katika uamuzi wa utata wa uchaguzi wa 2013 aya ya 290 mgombea akijitoa au kufa, unaosema kuwa uchaguzi huo sasa utafutiliwa mbali na shughuli ya uteuzi kufanyika, mrengo wa Jubilee unaegemea kipengee cha katiba kuwa mgombea wa uchaguzi akiwa mmoja, atangazwe rais mteule kando na kufanya marekebisho ya kupiga msasa utata huo.

Source: Kenya CitizenTV
 
Back
Top Bottom