Kenya: Rais Samia afungua kongamano la wafanyabiashara nchini Kenya, Rostam Aziz atema madini ukumbi mzima wamshangilia

Kenya: Rais Samia afungua kongamano la wafanyabiashara nchini Kenya, Rostam Aziz atema madini ukumbi mzima wamshangilia

Tunza hii kauli yako. Ndani ya miaka miwili haipiti, utasikia jambo la Wakenya kuhusu Tanzania. Mimi sipingani na Samia kwasababu anachokifanya ni kwa ajili ya Watanzania. Nitapingana kwa yale ambayo naona hayana manufaa kwa Tanzania. Ninyi kwa Upambavu wenu, ujinga wenu, uzwazwa wenu na ukilaza wenu, umbumbu wenu, kila kitu mnamsingizia hayati. Niulize Uganda kuzuiwa kuingiza Mahindi Kenya nayo ni sababu ya Hayati? Uganda kuzuiwa kupeleka Maziwa Kenya ni kwa sababu ya Hayati? Naweza kuwa nabishana na kajitu kasiko jielewa. Angalia mambo kwa upana wake kama Mtanzania unayelipenda Taifa lako. Serikali si Taifa. Anza na Nchi yako. Majirani zetu wale inatakiwa tule nao kwa umakini. Au nikukumbushe jambo, Kipindi Mheshimwa Jakaya Kikwete yupo Madarakani ilikuja Suala la Jumuiya ya Africa Mashariki ambapo walitaka Wananchi wawe huru kwenda kokote na kumiliki Ardhi. Watanzania kwa akili moja walikataa na Wabunge wakakataaa kwa kauli moja kisa tunawaogopa Wakenya walivyo.

Mama yetu Samia atafanya anayoona yanafaa kwa Taifa letu. Ila tusijiachie nao hasa kufungua mipaka yetu eti waje kufanya ajira huku kwa wingi. Tutakuwa tumeisha.

Rostam kalalamika, anajua alivyoteswa. Kwasisi Watu Wazima tunajua hata ya Miaka ya 90 huko tuliyofanyiwa na Wakenya. Tusicheze ngoma ya Adui, tuwe na Tanzania yetu.
Kwanini usitoe ushauri na siyo kusubiri tukae miaka Ili tuanguke? Kila kitu kina vita hata kuongoza familia tu kuna watu wanajitahidi wakurudishe nyuma, sasa ngazi ya nchi ni zaidi na Mama kutaka tujichanganye na wakenya kwenye biashara wala siyo vibaya kila mtu atajenga kwake maana kila nchi inasheria zake na mipaka yake inailinda, hivi wakati hatuna barabara kutoka Mwanza kuja dar situlikuwa tunapita kenya kwenye barabara zao Ili tufike upande mwingine mwa nchi yetu na tulipo jenga tukaanza kupita kwetu maana tuliona hiyo fursa na kuna watu wamewekeza kwa kuiga kenya tulivyokuwa tunakula kwenye migahawa yao na kupanda mabasi yao, sasa tunachotakiwa nikuiga vile vitu vizuri kwao Ili tutengeneze kwetu , ni vitu vingi vizuri wanavyo, ndo maana kuna watu wanalilia nafasi Kama hizo huko Ulaya waliko endelea kwenda kufanya kazi wapate maarifa waje huku wawekeze tatizo linakuwa akili zetu zinakuwa bado zikitamani kuishi kizamani kuvaa mitumba na makazi mabovu na kuitwa wanyongwe ndo tunaona fahari wakati hata Mungu hapendi vitu vinyonge, tuchangamane na mataifa yanayoendelea Ili tukimbie kifikira na kiuchumi, kila mtu apate nguvu na uchumi wa kujenga familia yake kwa kuondoa uoga na uvivu, nachotaka mama Samia afanye nikuleta katiba na mifumo inayojisimamia vitu vitajipanga vyenyewe maana kila mtu atasimama kwenye Sheria za nchi hata akija mugeni atasimama kwenye Sheria zetu.
 
Mbunge wa Zamani wa Igunga na Tajiri na namba moja Tanzania in terms of (Cash in hand), Leo akiwa na mama Samia Kenya ameongea Mambo ya kuwagusa wakenya moja kwa moja na kuonyesha uzalendo uliotukuka kwa nchi yake Tanzania, amesema haya
1.uwekezaji Kati ya Tanzania na Kenya uwe wa usawa
2. Tanzania tunapeleka nyanya wao wanaleta finished goods
3. Wakenya walimkatalia kuwekeza bilioni 300 nchini mwao.
4. Uhusiano uwe kwa manufaa ya nchi zote sio tu kuinufaisha Kenya

Hivyo ndiyo inavyokiwa kuwa Ili mapungufu yafanyiwe kazi, lakini hilo la nyanya kupeleka kenya mbona inahitajika akili kubwa tu kama wanakuuzia finished goods, na wewe una hela basi unatengeneza hizo finished goods maana tayari raw materials zipo za kutosha mpaka zinakwenda nje.
 
Nina imani, nchi yetu ipo kwenye njia sahihi baada ya kupotezwa kwa miaka mitano.

Tukazanie kujenga mifumo itakayozuia Taifa kuangukia kwenye uongozi wa watu wasio na uwezo. Mifumo iwezeshe, akitokea kiongozi wa hovyo, kuwe na utaratibu rahisi wa kumwondoa.

Fikirieni miaka mitano tuliyokosa uongozi sahihi, hasara kubwa tuliyoipata kwa sekta mbalimbali. Na ikumbukwe kulikuwa na hatari ya nchi kuburutwa kwa miaka kumi, na pengine zaidi.

Umetoa hoja za kisiasa kuliko uhalisia.

Wahenga walinena Hapendwi mtu ila pesa.

Katika mtazamo wa maisha kitaifa, pesa ni njia kuu za kiuchumi zinazomwesha mwanachi kutengeneza/kujipatia fedha na hizi si nyingine bali miundo mbinu imara ya usafirishaji wa mazao ya shamba na bidhaa za viwandani kwenda kwenye masoko ndani na nje ya nchi.

Uongozi wa Awamu ya Tano ndio ulizingatia hilo na kuwezesha kukusanya kodi ya kutosha hadi kuweza kuboresha huduma za jamii km maji, nishati, afya na elimu.

Awamu ya Sita inakuta, kwa kiwango kikubwa, ubora na uimara wa miundo mbinu ya usafirishaji, hivyo inaweza kujikita katika kutafuta masoko nje ya nchi. Soko la uhakika ni nchi za Jumuia ya Afrika Masharki. Hivyo basi, safari ya Rais SSH Kenya inafungua milango ya soko la bidhaa ambazo zimeanza kuzalishwa kwenye viwanda nchini.
 
Mbunge wa Zamani wa Igunga na Tajiri na namba moja Tanzania in terms of (Cash in hand), Leo akiwa na mama Samia Kenya ameongea Mambo ya kuwagusa wakenya moja kwa moja na kuonyesha uzalendo uliotukuka kwa nchi yake Tanzania, amesema haya
1.uwekezaji Kati ya Tanzania na Kenya uwe wa usawa
2. Tanzania tunapeleka nyanya wao wanaleta finished goods
3. Wakenya walimkatalia kuwekeza bilioni 300 nchini mwao.
Sasa ukisikia Samia alichosema mbele ya bunge la Kenya utatapika:

Nanukuu:

"Pamoja na madhaifu au mapungufu makubwa ya uwekezaji na biashara ya Tanzania dhidi ya Kenya, bado tunahitaji muje muwekeze kwa sababu sisi hatuna mtaji. Tuna ardhi, tuna madini, tuna gesi, tuna kila kitu lakini hatuna mtaji. Kenya mna mtaji, njooni Tanzania."

ROSTAM AZIZ yeye akasema EFF NO!
Hatukubali trade imbalance. Hatukubali kuendelea kuwa mateja wa Kenya.

ROSTAM AZIZ, of all the people, ameonyesha uzalendo kuliko Rais wa Tanzania.

Imagine that!
 
Sisi kama nchi tunanufaika zaidi makampuni yakija kwetu kuwekeza sio makampuni yetu kwenda kuwekeza Kenya ila kuwekeza kama kutanua biashara ni vizuri kwa nchi yetu, mafanya biashara na kwa wa kenya. lakini sitaona ufahari nikiona mfano kampuni A inatoka Tanzania inaenda kuwekeza Kenya napenda kuona sio kampuni 500 waje hata 2000 ni nzuri kwa nchi japo haitakuwa nzuri kwa watu kama Rostam sababu ushindani unakuwa mkubwa. Point nakubali wapate nafasi kuwekeza kule kwa urahisi ila ajira sisi tumenufaika.
Kiuchumi faida inayopatika nje ya nchi na kuletwa ndani ya nchi ni nzuri zaidi kuliko faida inayopatikana ndani ya nchi. Kasome economics utaelewa hii ishu, usijibu kwa hisia zako binafsi.....
 
Mwendazake hakuwa na hekima kabisa, alitanguliza Sana kiburi na majivuno wakati hata biashara ya dunia haijui. Diplomasia inataka majadiliano na uvumilivu
umeelewa lakini alichoongea rostam au unacomment tu
 
Kiuchumi faida inayopatika nje ya nchi na kuletwa ndani ya nchi ni nzuri zaidi kuliko faida inayopatikana ndani ya nchi. Kasome economics utaelewa hii ishu, usijibu kwa hisia zako binafsi.....
Uchumi hakuna formula moja sote tunajuwa usiniambie uwekezejji makampuni kuja ndani hauna faida hizo ajira zitatoka wapi? unakwenda nje ukiwa na mtaji mkubwa sisi hatuna tunahitaji mitaji iletwe kwetu sio kutoka sio level yetu. Foregn direct investment ina boost uchumi wa nchi kukua kwa ajira na technology ndio maana nyimbo kubwa inayoimbwa njooni muwekeze kwetu wanaleta ajira mnazalisha mnauza bishaa nje. Nadhani labda hujui hata ugomvi mkubwa wa Trump na China na pia Mexico aliyashurutisha makampuni yarudi USA manufactoring iwe USA na ajira ziwe USA badala ya magari kuwa assembly Mexico au Nike kuwa China sababu ya cheap labour. kuwekeza nje kuna faida pia lakini sio katika kutengeza ajira.
 
Sasa ukisikia Samia alichosema mbele ya bunge la Kenya utatapika:

Nanukuu:

"Pamoja na madhaifu au mapungufu makubwa ya uwekezaji na biashara ya Tanzania dhidi ya Kenya, bado tunahitaji muje muwekeze kwa sababu sisi hatuna mtaji. Tuna ardhi, tuna madini, tuna gesi, tuna kila kitu lakini hatuna mtaji. Kenya mna mtaji, njooni Tanzania."

ROSTAM AZIZ yeye akasema EFF NO!
Hatukubali trade imbalance. Hatukubali kuendelea kuwa mateja wa Kenya.

ROSTAM AZIZ, of all the people, ameonyesha uzalendo kuliko Rais wa Tanzania.

Imagine that!
Leo hii Rostam kawa mzalendo? eeh chineke
 
Uchumi hakuna formula moja sote tunajuwa usiniambie uwekezejji makampuni kuja ndani hauna faida hizo ajira zitatoka wapi? unakwenda nje ukiwa na mtaji mkubwa sisi hatuna tunahitaji mitaji iletwe kwetu sio kutoka sio level yetu. Foregn direct investment ina boost uchumi wa nchi kukua kwa ajira na technology ndio maana nyimbo kubwa inayoimbwa njooni muwekeze kwetu wanaleta ajira mnazalisha mnauza bishaa nje. Nadhani labda hujui hata ugomvi mkubwa wa Trump na China na pia Mexico aliyashurutisha makampuni yarudi USA manufactoring iwe USA na ajira ziwe USA badala ya magari kuwa assembly Mexico au Nike kuwa China sababu ya cheap labour. kuwekeza nje kuna faida pia lakini sio katika kutengeza ajira.
Hakuna sehemu nimesema uwekazaji wa nje kuja ndani hauna faida yoyote, soma tena vizuri nilichokiandika.

Kenya kuwa na makampuni zaidi ya 500 yaliyowekeza hapa nchini na sisi kuwa na makampuni yasiyozidi 30 kuwekeza kwao, tena kwa nchi ambazo zinakaribiana kiuchumi hauwezi kusema tupo vizuri au tunaenda pamoja. Hii ni sawa na kuwategemea wao watukuzie uchumi wetu alafu tutegemee tutapiga hatua.

Hata mama mwenyewe alisema tumekuja kuwekeza kenya kwa nguvu zote.

Ndio maana hata wachezaji mipira wanapendelea kwenda kucheza nje ya nchi badala ya kukomaa ndani na hata wasanii kufanya show nje ya nchi
 
Kuna neno Mama katamka wazi sisi tuna resource nyinyi mna mitaji hapo ndio utaelewa kwanini wao wana kampuni 500 na sisi 30. Tanzania hatuna mitaji. Mifano unayotoa ya wachezaji kwenda nje hapo ukiona wanatoka nje ujue cha nje kina ubora kuliko cha ndani ndio maana EPL huwakuti wachezaji wakienda nje sababu wanachopata kwao ni kikubwa hawezi kupata nje. Kenya wanavutiwa kuwekeza hapa kwa wingi sababu ya resource na pia labor bado ni cheap Tanzania. Kwa nchi na uhakika huwezi kutaja hata kampuni 50 kwa ukubwa wa kimitaji hatuna kihivyo na Bank zetu sio rafiki kabisa kuwezesha wafanya biashara.
 
Nina imani, nchi yetu ipo kwenye njia sahihi baada ya kupotezwa kwa miaka mitano.

Tukazanie kujenga mifumo itakayozuia Taifa kuangukia kwenye uongozi wa watu wasio na uwezo. Mifumo iwezeshe, akitokea kiongozi wa hovyo, kuwe na utaratibu rahisi wa kumwondoa.

Fikirieni miaka mitano tuliyokosa uongozi sahihi, hasara kubwa tuliyoipata kwa sekta mbalimbali. Na ikumbukwe kulikuwa na hatari ya nchi kuburutwa kwa miaka kumi, na pengine zaidi.
Mungu anawapenda sana watanzania... ila watanzania hatujipendi!!
 
Leo hii Rostam kawa mzalendo? eeh chineke

Kabisa, kabisa! Rostam Aziz kamzidi Rais wa nchi kutetea nchi.

Mbele ya Wakenya na mbele ya Samia Suluhu Rostam Aziz, of all the people, kakataa kujishusha na kujinyenyekeza kwa Wakenya, of all the countries.

Rais mmoja anasema tembeeni kifua mbele, msimuogope mduwanzi yeyote wa kigeni, mwingine anakuja anatamka wazi wazi sisi hatuna hela, Wakenya njooni muendeshe uchumi wetu!

Mama anauza nchi, hana uchungu na Tanganyika anyway. Mwambieni basi akaite Waarabu waje ku commandeer the Zanzibar economy tuone.
 
Wasukuma mtakufa kwa kihoro !! Rais SSH bado yupo sana. Mwendazake huyo tulimfukia Chato na MAUJINGA yake yote na sasa ni chakula ya minyoo.

Tanzania ni nchi ya amani, haki, upendo na ukarimu.
 
Kabisa, kabisa! Rostam Aziz kamzidi Rais wa nchi kutetea nchi.

Mbele ya Wakenya na mbele ya Samia Suluhu Rostam Aziz, of all the people, kakataa kujishusha na kujinyenyekeza kwa Wakenya, of all the countries.

Rais mmoja anasema tembeeni kifua mbele, msimuogope mduwanzi yeyote wa kigeni, mwingine anakuja anatamka wazi wazi sisi hatuna hela, Wakenya njooni muendeshe uchumi wetu!

Mama anauza nchi, hana uchungu na Tanganyika anyway. Mwambieni basi akaite Waarabu waje ku commandeer the Zanzibar economy tuone.
Kuita wawekezaji ni kuuza nchi?
 
Kuita wawekezaji ni kuuza nchi?
Ndio, ni uwekezaji ule ni kuuza nchi.

Kwani Wachina wa Bagamoyo sio wawekezaji ?

Tuliwakataa kwa sababu uwekezaji ule ni kuuza nchi.

Julius Nyerere 1972 alikataa Sweden wawekeze kwenye madini, alisema anataka 51% ya mapato. Sweden wakataa, Nyerere akawaambia siwezi kuuza nchi. Kwa nini madini ya kwangu wewe upate cha juu kikubwa zaidi yangu ???

Hawa walikuwa rafiki zake waliokuwa wana bankroll Socialism Experiment ya Mwalimu. Na bado akakataa kuuza nchi.

Samia Suluhu Hassan hawezi kuelewa maslahi ya nchi ni nini, hana uzalendo.
 
Back
Top Bottom