Kwanini usitoe ushauri na siyo kusubiri tukae miaka Ili tuanguke? Kila kitu kina vita hata kuongoza familia tu kuna watu wanajitahidi wakurudishe nyuma, sasa ngazi ya nchi ni zaidi na Mama kutaka tujichanganye na wakenya kwenye biashara wala siyo vibaya kila mtu atajenga kwake maana kila nchi inasheria zake na mipaka yake inailinda, hivi wakati hatuna barabara kutoka Mwanza kuja dar situlikuwa tunapita kenya kwenye barabara zao Ili tufike upande mwingine mwa nchi yetu na tulipo jenga tukaanza kupita kwetu maana tuliona hiyo fursa na kuna watu wamewekeza kwa kuiga kenya tulivyokuwa tunakula kwenye migahawa yao na kupanda mabasi yao, sasa tunachotakiwa nikuiga vile vitu vizuri kwao Ili tutengeneze kwetu , ni vitu vingi vizuri wanavyo, ndo maana kuna watu wanalilia nafasi Kama hizo huko Ulaya waliko endelea kwenda kufanya kazi wapate maarifa waje huku wawekeze tatizo linakuwa akili zetu zinakuwa bado zikitamani kuishi kizamani kuvaa mitumba na makazi mabovu na kuitwa wanyongwe ndo tunaona fahari wakati hata Mungu hapendi vitu vinyonge, tuchangamane na mataifa yanayoendelea Ili tukimbie kifikira na kiuchumi, kila mtu apate nguvu na uchumi wa kujenga familia yake kwa kuondoa uoga na uvivu, nachotaka mama Samia afanye nikuleta katiba na mifumo inayojisimamia vitu vitajipanga vyenyewe maana kila mtu atasimama kwenye Sheria za nchi hata akija mugeni atasimama kwenye Sheria zetu.Tunza hii kauli yako. Ndani ya miaka miwili haipiti, utasikia jambo la Wakenya kuhusu Tanzania. Mimi sipingani na Samia kwasababu anachokifanya ni kwa ajili ya Watanzania. Nitapingana kwa yale ambayo naona hayana manufaa kwa Tanzania. Ninyi kwa Upambavu wenu, ujinga wenu, uzwazwa wenu na ukilaza wenu, umbumbu wenu, kila kitu mnamsingizia hayati. Niulize Uganda kuzuiwa kuingiza Mahindi Kenya nayo ni sababu ya Hayati? Uganda kuzuiwa kupeleka Maziwa Kenya ni kwa sababu ya Hayati? Naweza kuwa nabishana na kajitu kasiko jielewa. Angalia mambo kwa upana wake kama Mtanzania unayelipenda Taifa lako. Serikali si Taifa. Anza na Nchi yako. Majirani zetu wale inatakiwa tule nao kwa umakini. Au nikukumbushe jambo, Kipindi Mheshimwa Jakaya Kikwete yupo Madarakani ilikuja Suala la Jumuiya ya Africa Mashariki ambapo walitaka Wananchi wawe huru kwenda kokote na kumiliki Ardhi. Watanzania kwa akili moja walikataa na Wabunge wakakataaa kwa kauli moja kisa tunawaogopa Wakenya walivyo.
Mama yetu Samia atafanya anayoona yanafaa kwa Taifa letu. Ila tusijiachie nao hasa kufungua mipaka yetu eti waje kufanya ajira huku kwa wingi. Tutakuwa tumeisha.
Rostam kalalamika, anajua alivyoteswa. Kwasisi Watu Wazima tunajua hata ya Miaka ya 90 huko tuliyofanyiwa na Wakenya. Tusicheze ngoma ya Adui, tuwe na Tanzania yetu.