Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Serikali nchini Kenya imepiga maarufu maandamano katika maeneo ya katikati mwa miji ya Mombasa, Kisumu na Nairobi.
Kaimu Waziri wa Usalama Dkt. Fred Matiang'i amesema pia kwamba wanaopanga maandamano wanafaa kuwajibishwa kutokana na uharibifu wa mali unaotokea wakati wa maandamano.
Hatua hiyo Dkt. Matiang'i imetokea huku muungano wa upinzani National Super Alliance NASA chini ya kinara wao Raila Odinga ukiendelea na maandamano ya kushinikiza mageuzi katika tume ya uchaguzi IEBC.
Jumatano, visa vya uharibifu na uporaji wa mali viliripotiwa katikati mwa jiji la Nairobi.
Mmoja wa viongozi wa NASA James Orengo, ambaye alikuwa Naibu ajenti mkuu wa Bw. Odinga wakati wa uchaguzi wa mwezi Agosti ambao ulifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu, alitoa wito kwa wafuasi wa Muungano huo kuandamana kila siku.
Chanzo: BBC