Kenya: Serikali yapiga marufuku maandamano katikati ya miji ya Mombasa, Kisumu na Nairobi

Kenya: Serikali yapiga marufuku maandamano katikati ya miji ya Mombasa, Kisumu na Nairobi

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Serikali nchini Kenya imepiga maarufu maandamano katika maeneo ya katikati mwa miji ya Mombasa, Kisumu na Nairobi.

Kaimu Waziri wa Usalama Dkt. Fred Matiang'i amesema pia kwamba wanaopanga maandamano wanafaa kuwajibishwa kutokana na uharibifu wa mali unaotokea wakati wa maandamano.

Hatua hiyo Dkt. Matiang'i imetokea huku muungano wa upinzani National Super Alliance NASA chini ya kinara wao Raila Odinga ukiendelea na maandamano ya kushinikiza mageuzi katika tume ya uchaguzi IEBC.

Jumatano, visa vya uharibifu na uporaji wa mali viliripotiwa katikati mwa jiji la Nairobi.

Mmoja wa viongozi wa NASA James Orengo, ambaye alikuwa Naibu ajenti mkuu wa Bw. Odinga wakati wa uchaguzi wa mwezi Agosti ambao ulifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu, alitoa wito kwa wafuasi wa Muungano huo kuandamana kila siku.

Chanzo: BBC

03576663a12b1781d8573795c6aa15ad.jpg
15b5d1462caf22daf85c22f715bd3857.jpg
151e2e546cbe92cb20a8cf8a84b3239d.jpg
 
Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani, Fred Matiang'i amepiga marufuku maandamano katikati ya mji mitatu ya Mombasa, Kisumu na Nairobi.

Kaimu Waziri wa Usalama wa ndani huyo alisema kuwa marufuku hiyo inaanza kutekelezwa mara moja ili kuokoa uchumi

Aidha, amri hiyo imekuja kufuatia jana kuripotiwa kutokea kwa uharibifu mkubwa wa magari na bidhaa mbalimbali.

Wakati Waziri huyo akitangaza marufuku hiyo, vijana wa NASA wamejibu kuwa hawataacha kuandamana kwani ni haki yao kikatiba na kwamba maandamano hayo hayana lengo la kufanya uharifu kama Serikali ilivyochukulia.
Chandomo wapo?? Lowasa upo?? Mbow upo??
 
Tunaomba ndugu zetu wakenya mjitokeze mtufafanulie hili la upigaji marufuku wa maandamano ambayo mpaka sasa kwa ujumla yaekuwa ya amani kwa kiasi kikubwa, sababu iliyotolewa na Matiang'i ni ili kuokoa uchumi, wala sio fujo au uvunjifu wa amani, je katiba ya Kenya ambayo inasifiwa kuwa nzuri haijakiukwa na serikali yenyewe iliyokula kiapo kuilinda?, je ni funzo gani kama wakenya mnajifunza kutokana na huu mparaganyiko wa nchi yenu?, hamuoni kwamba serikali inataka kugeuza maandamano ya amani kuwa ya fujo?. is Kenya turns to be a dictotarship country?
 
Kuna watu msipotaja majina ya wanasiasa hamjisikii vizuri nadhani hata chooni hamuendi kabisa.

Mambo ya Kenya unataja wanasiasa wa Tanzania.

Hii nchi kuendelea mpaka wakoloni warudi kutawala upya.
Tunawapenda,ni wanasiasa wetu na sisi ni wazalendo.Je hutaki?
 
Tunaomba ndugu zetu wakenya mjitokeze mtufafanulie hili la upigaji marufuku wa maandamano ambayo mpaka sasa kwa ujumla yaekuwa ya amani kwa kiasi kikubwa, sababu iliyotolewa na Matiang'i ni ili kuokoa uchumi, wala sio fujo au uvunjifu wa amani, je katiba ya Kenya ambayo inasifiwa kuwa nzuri haijakiukwa na serikali yenyewe iliyokula kiapo kuilinda?, je ni funzo gani kama wakenya mnajifunza kutokana na huu mparaganyiko wa nchi yenu?, hamuoni kwamba serikali inataka kugeuza maandamano ya amani kuwa ya fujo?. is Kenya turns to be a dictotarship country?
Exactly Mkuu.. Nia Inaelezwa kuwa ni kufikisha malalamiko yao. Lakini kuna wale waharifu hujitokeza kwenye kwenye maandamano ambao lengo lao ni wizi.
 
Exactly Mkuu.. Nia Inaelezwa kuwa ni kufikisha malalamiko yao. Lakini kuna wale waharifu hujitokeza kwenye kwenye maandamano ambao lengo lao ni wizi.
Ni jukumu la polisi kuimarisha ulinzi ili hao wahalifu waspiate hiyo fursa ya kufanya uhalifu, waandamanaji wanatumia haki yao ya oikatiba, hivyo serikali inawajibika kuwasaidia ili kutekeleza haki yao ya kikatiba, serikali haiwezi kuwakataza kutumia haki ya kikatiba, ni kama kusema serikali imepiga marufuku wanafunzi wote walioko katika miji mikubwa wasiende shuleni kwa sababu baadhi ya wanafunzi wanafanya uhalifu huko njiani.

Lakini sababu iliyotolewa na serikali sio hiyo, ni kwamba serikali inataka kuokoa uchumi, hii ni kwasababu Uhuru Kenyatta alisema kama wanataka kuandama waacheni ila wasiharibu vitu vya watu barabarani, NASA wamekuwa wajanja sana, wamekuwa watulivu katika miji mingi maendeleo yamekuwa ya amani, lakini kwa ujumla athari kubwa ya maandamano sio hivyo vitu au maduka kuporwa, ni uchumi wa nchi kudhoofika kwa sura ya nchi kuchafuliwa na wawekezaji au watalii kuogopa kuitembelea Kenya, na kwasabu hakuna njia ya kuyazuia kwa sababu yamekuwa ya amani, serikali imejitia yenyewe kitanzi, sasa shuhudia fujo
 
Kuna watu msipotaja majina ya wanasiasa hamjisikii vizuri nadhani hata chooni hamuendi kabisa.

Mambo ya Kenya unataja wanasiasa wa Tanzania.

Hii nchi kuendelea mpaka wakoloni warudi kutawala upya.
Kichwani kumejaa mashudu huyo Mkuu..
Msamehe.
 
Katika maandamano kamahayo wezi ndio huvuruga maana wanachangamkia fursa yakuvunja na kuiba Mali zawatu.
 
Hatimaye bwana mkubwa wa Kenya mh Uhuru chini ya serikali yake wamepiga marufuku maandamano ya wapinzani.
Kuanzia sasa ukiandamana ni kichapo na kisha lockup.
Ingawa Magufuli alishauriwa amuige Kenyatta, ila inaonekana Kenyatta anafuata nyayo za kaka ake Magufuli.
IMG_20171012_201031.jpg
 
Sasa kiongozi wao Katia mpira kwapani....Maandamano ya nn kama sio Fujo
 
03576663a12b1781d8573795c6aa15ad.jpg
15b5d1462caf22daf85c22f715bd3857.jpg
151e2e546cbe92cb20a8cf8a84b3239d.jpg
Serikali nchini Kenya imepiga maarufu maandamano katika maeneo ya katikati mwa miji ya Mombasa, Kisumu na Nairobi.

Kaimu Waziri wa Usalama Dkt. Fred Matiang'i amesema pia kwamba wanaopanga maandamano wanafaa kuwajibishwa kutokana na uharibifu wa mali unaotokea wakati wa maandamano.

Hatua hiyo Dkt. Matiang'i imetokea huku muungano wa upinzani National Super Alliance NASA chini ya kinara wao Raila Odinga ukiendelea na maandamano ya kushinikiza mageuzi katika tume ya uchaguzi IEBC.

Jumatano, visa vya uharibifu na uporaji wa mali viliripotiwa katikati mwa jiji la Nairobi.

Mmoja wa viongozi wa NASA James Orengo, ambaye alikuwa Naibu ajenti mkuu wa Bw. Odinga wakati wa uchaguzi wa mwezi Agosti ambao ulifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu, alitoa wito kwa wafuasi wa Muungano huo kuandamana kila siku.

Chanzo: BBC

Hivi Wakenya hawana hobbies? I mean hata football hakuna kama kwetu Simba na Yanga?
 
Back
Top Bottom