Kenya vs Tanzania: Mbona Kuna Chuki?


Kwa jinsi unavyotapatapa naona umeishiwa na hoja, sasa umekwenda kwa mambo ya ushindani kitu ambacho sijakitaja, sasa tushindane na nyie kwa lipi wakati nyote mko nyuma yetu kwa kila kitu. Kama ni suala la ushindani, labda tukashindane na walio mbele yetu, lakini tukianza kupoteza muda na kugeuza ili tushindane na walio nyuma yetu tutaachwa.

Tungekua tunaendesha nchi kimihemko kama mfanyavyo, leo hii tungekua nyuma sana, kumbuka nchi yetu ni ndogo, nusu yake kame tupu na hatuna madini kama nyie, raslimali ni chache, lakini pamoja na hayo tunajituma balaa na kutawala ukanda wote huu kwa kila kitu, kielimu, kiuchumi n.k.

Sisi hatushindani, tunapambana kuiboresha nchi yetu kwa ajili ya watu wake, tunatafuta masoko Afrika yote, na kama ilivyo kawaida ya biashara, kuna kupoteza na kupata, unaweza ukapoteza soko upande mmoja lakini kama ukiwa na akili utabuni masoko kwengine. Leo hii kama nilivyotaja hapo awali, tumeanza kufungua fursa kwa Waarabu wa Sudan na Libya, kumbuka tumeanza kuingia Ethiopia ambayo ilikua haiingiliki

Ninachofahamu, mataifa yote yaliyotuzunguka ipo siku wataboresha viwanda vyao na kupunguza utegemezi wa bidhaa zetu, ambapo ni jambo nzuri maana kwa njia moja au nyingine jirani akipaa kiuchumi hata wewe utafaidika, lakini pia kadiri majirani zetu wanainuka na sisi pia tunabuni mikakati mipya ya kibiashara na kusonga mbele, Kenya ya leo sio iliyokuwepo miaka 20 iliyopita.
 

Chaajabu bado mko nyuma na mbio zote mlizo zilombiza miaka 50 ya Uhuru na kufuata sera za kibepari. Hakuna haki kwa kila raia, hakuna fursa sawa kwa kila raia, hakuna usalama kwa kila raia, kukubwa zaidi hakuna chakula cha kutosha kwa kula raia. Mkisema mko mbele sijuwi mbele ya nani ikiwa nchi kama Ethiopia iliyokuwa na njaa kali miaka ya 90s leo inawaacha.

Ikiwa mnaona hizi nchi ziko chini sana kwenu (ni kichekesho) sasa mnafanya nini kwemye soko la EAC? Si muende kule mnakoona ni wa level yenu? Kifupi ni kwamba Kenya haiwezi kupumua hata pumzi moja bila EAC, tena Kenya haiwezi kupumua bila hata Somalia kama unaelewa nasema nini.
 
 
Ipo siku nitakuwa kiongozi wa Taifa(Raisi) afu nitaifanya Afrika kuwa moja kimabavu iwe kwa damu au chuma, yeyote atakae leta fyokofyoko ataenda kupuliza moto wa Jehanamu.
I like that! your avatar carries gun to symbolize your wish. Kudos
 
Kweli kabisa unganisha afrika kwa lazima maana mijitu mijinga sio ya kuipa nafasi kwenye maamuzi ya msingi.
 
Kuna mijitu inawasema eti wakenya wana roho mbaya. Kwani watanzania tuna roho nzuri?? Nchi imejaa wivu, majungu na unyanyasaji wa kisiasa kila kona. Ona chaguz zetu haki zinavyominywa. Watu wanaokotwa coco beach wamewekwa virobani. Wengine wamepigwa risasi na wengine wamepotea hadi leo kisa siasa. Kibiti pale watu karibia 40 wamepoteza maisha kiutatanishi. Tunachoma moto wezi kisa simu za elfu 50.
Sijaona ubaya wa wakenya mimi unaofanya tuwaseme vibaya. Waafrika tupendane tusonge mbele kimaendeleo. Kuchukiana hakutisaidii.
 

Hehehe!! Punguza povu maana zinafanya ushindwe kufikiria kabla ya kuandika....

Hakuna taifa lolote dunia hii lenye usawa, hata mataifa yanayoongoza dunia kiuchumi, huko utakuta baadhi ya raia wao hawapo nafuu.
Hata mataifa ya kiujamaa kwa mfano nchi yenu huwa tunaona jinsi huo mfumo uliwaharibia nchi, leo hii mlifaa kuwa viongozi wa Afrika, ni aibu sana kwa liinchi lote hilo lenye kila aina ya raslimali lakini bado linatajwa ndani ya mataifa maskini, haileti picha kabisa.

Kenya haiwezi ikachoka na majirani wake, sisi ni wafanya biashara na kama kawaida mwanabiashara hawezi akachoka na wateja, hata kama wateja wenyewe wana hulka za kizezeta. Kila mteja ni muhimu na lazima ubembeleze, hata wakati mnajitoa ufahamu na kutia moto viranga kisa wamenunuliwa kutoka Kenya, bado tutaendelea kuwafanya muhisi kuwa nyie ni wafalme.

Tunahitaji kila shilingi, hata kama itabidi tukwepe mabomu Somalia, Sudani ya Kusini, au tuvumilie chuki zenu tutakuja tu na kufanya biashara. Mkenya ni mtu mvumilivu na hujituma sana, utamkuta hata vijijini Malawi, Msumbiji, Zambia n.k. akisaka fursa za kibiashara. Kuna maeneo huwa nakutana na Wakenya nabaki kinywa wazi, hivyo nawaambia muamini msiamini siri ya kuwafikia Wakenya ipo kwenye kujituma, ila kwa nyie kulea chuki, machungu na majungu havitawasaidia, mtaendelea kuumia bure.
 
Usiogope kijana.
Ni ushindani wenye afya tu, hauliwi mtu. Wakenya wapo huku bongo tunaishi nao kwa upendo kabisa.
 
Nikimkuta mwizi anachomwa na kama kweli kaiba hiyo simu ya elfu 50, nitaimba afe tu na akaliwe na atupwe mtoni awe chakula cha mamba, huku Tz tuna zero tolerance na wezi ndio maana mjini unapita kwa amani na mwizi akionekana ni kila mtu anamshambulia.
Kenya tomboya street unakabwa na vibaka ila wapita njia wanakuangalia tu kama kideo.
 

Huwa nacheka sana watu wakisema Kenya ni nchi ya kibepari, Kenya sio nchi ya kibepari wala ya wafanyabiashara. Kenya ni nchi ya "Mabwana na Watwana", ni nchi iliyogawanyika vipande-vipande. Nchi zote kubwa za kibepari zimefanikisha kupunguza kero za wananchi wao kwa asilimia 90%. Nyumba, maji safi, umeme, usalama wa raia, magonjwa, usafirishaji, elimu, kazi nk. Tena wala sio nchi zilizo anza zamani kama Marekani au bara la Ulaya. Nchi kama Malaysia, South Korea, Argentina, Israel, Singapore nk, ambazo miaka 60 zilikuwa na changamoto sawa za Kenya, na walipewa fursa za masoko makubwa kama vile Kenya ilipewa. Tatizo lenu ni wizi ndio umewapoteza, wakubwa wachache wanawaibia wadogo walio wengi. Badala ya kuingiza hiyo hela kwenye mzunguko, wakubwa wanajiwekea wao na familia zao. Halafu mnaleta maneno mengi hapa JF kutuambia Kenya iko juu, iko juu ya nani ikiwa nnashidwa hata kulipa madeni yenu? Alfred Mutua ameongea maneno ya maana sana kwa wakenya kwamba urais si wa watu wachache ni wa kila Mkenya. (Anzia 4:14)

 

Not all are the same...Some are decent and very open minded...In both countries...
 
sasa hapo tuwasifu wakoloni au wakenya
 
wakenya na wa tz wanamaudugu na maingiliano kuzidi nchi yeyote EAC, huwez ni twins hivyo tarajia hayo but all in all Kenya is a country Tanzanian love than any in the world
 
Tatizo huku kwetu tokea mlipovunja EAC 1977 na Kenya mkanufaika na investment kubwa zilizokuwa za pamoja especially rasilimali za ndege,, wa TZ tunakuwa makini sana kwa kila kitu ili lisije likajirudia tena,, waswahili tunasema ukiishaumwa na nyoka ukiguswa na jani unadhtuka sana
 
most kenyan ni show off san,wabaguzi hata wenyew kwa mwenyew na tabia hiyo amuachagi hata mkija nchi za watu,mkenya ndio anajifanya amestaarabika kuliko waafrica wengine wageni n watalii wakija utasikia peoples from tz wako vile au hivi kwa maendeleo mliofikia had hapo mnajion kma vile mpo bara la ulaya na sio africa ni machache tu hayo lakin yapo mengi
note:sio wakenya wote wapo ivyo..ni hyo tuu
 
namaanisha kenya imeanza kujegwa kitambo kiasi kwamba tz haikuwa na mazingira rafiki kwa mabwanyenye sasa sisi tumeamka mda si mrefu na tunapambana nao ila wenyewe kenya yao imejengwa kitambo
Acha utoto basi rafiki kuanza kitu ndo kushinda mwisho ,walipajenga sio kama makazi ya kudumu bali banda la shambani ,don find any pride in being colonised,ni sawa na vilema wawili kujisifia huyu aligongwa na mercedes ya 2014 huyu aligongwa na carina ya 1999 ,grow up eti unajisifia mkeo kuwa na bwana mwenye hela
 
Huyu jamaa profile yake inaonyesha yumo jf tangu mwaka 2012 ili jamaa ni jambazii kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…