MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Sitaki kuamini kama hapa ndio umemaliza, hapa ndio mwisho wa uwezo wako wa kulewa biashara za kinchi na kikanda. Kinacho nishangaza ni hili neno Ushindani, mnashindana na nani, wateja wenu? Nani mnunuzi wa bidhaa za Kenya na nani mnunuzi wa bidhaa za Tanzania, nani mnunuzi wa bidhaa za Uganda au Rwanda? Hivi kama Marekani ingeamuwa kushindana na bara la Ulaya baada ya vita ya pili ya Dunia, wangeweza kufanya biashara kama wanayoifanya hii leo? Badala ya kukaa meza moja na wateja au washiriki wenu wa kibiashara, nyinyi mnaazisha ushidani kama ule wa CoW. Hizo mbio mnazokimbia kusikojulikana mnategemea kupata nini mwisho wake?
Kwa jinsi unavyotapatapa naona umeishiwa na hoja, sasa umekwenda kwa mambo ya ushindani kitu ambacho sijakitaja, sasa tushindane na nyie kwa lipi wakati nyote mko nyuma yetu kwa kila kitu. Kama ni suala la ushindani, labda tukashindane na walio mbele yetu, lakini tukianza kupoteza muda na kugeuza ili tushindane na walio nyuma yetu tutaachwa.
Tungekua tunaendesha nchi kimihemko kama mfanyavyo, leo hii tungekua nyuma sana, kumbuka nchi yetu ni ndogo, nusu yake kame tupu na hatuna madini kama nyie, raslimali ni chache, lakini pamoja na hayo tunajituma balaa na kutawala ukanda wote huu kwa kila kitu, kielimu, kiuchumi n.k.
Sisi hatushindani, tunapambana kuiboresha nchi yetu kwa ajili ya watu wake, tunatafuta masoko Afrika yote, na kama ilivyo kawaida ya biashara, kuna kupoteza na kupata, unaweza ukapoteza soko upande mmoja lakini kama ukiwa na akili utabuni masoko kwengine. Leo hii kama nilivyotaja hapo awali, tumeanza kufungua fursa kwa Waarabu wa Sudan na Libya, kumbuka tumeanza kuingia Ethiopia ambayo ilikua haiingiliki
Ninachofahamu, mataifa yote yaliyotuzunguka ipo siku wataboresha viwanda vyao na kupunguza utegemezi wa bidhaa zetu, ambapo ni jambo nzuri maana kwa njia moja au nyingine jirani akipaa kiuchumi hata wewe utafaidika, lakini pia kadiri majirani zetu wanainuka na sisi pia tunabuni mikakati mipya ya kibiashara na kusonga mbele, Kenya ya leo sio iliyokuwepo miaka 20 iliyopita.