Kenya: Walimu 3 wa Garrisa wameuawa mapema leo na watu wanaoaminiwa kuwa wanamgambo wa kundi la al Shabaab

Dini gani siyo spiritual?
anayepaswa kuwa spiritual au kutokuwa ni yule anayeabudu, dini inatoa mafundisho. Ukianza kuwa spiritual ndo hapo unatakiwa kujitathmin
 
Umesema kuna dini sio spiritual... Ndo nikakuuliza ipi hiyo??
Mimi naongelea mafundisho ya dini husika kama ni spiritual au sio spiritual???
Kwasababu hata yoga kuna watu wanaifanya bila kuwa spiritual lakini yoga ni spiritual.
 
... dini yao Mkuu! Wewe ni mgeni kwamba hujui magaidi wanatetea dini yao na wamekaa kidini zaidi?

Ni kweli huwa wanasema Wanatetea Dini yao pamoja na Yule Mungu wao!

Zaidi wanasemaga wanamtetea Yule Mungu na wanamtaja kwa jina kabisa!

Sasa mimi huwa najiuliza huyo Mungu anaetetewa na binadamu kwa nguvu kubwa hivyo na uovu mkubwa wa kuua watu wasio na hatia ni Mungu dhaifu kiasi gani?

Mimi nilizani kwa Mungu huwa Mkubwa na mwenye nguvu zote alipaswa kujitetea mwenyewe kwa nguvu zake na kuonesha utukufu wake lakini badala yake anatetewa na binadamu?! [emoji87][emoji87][emoji87]

Mbona inaleta mashaka?

Kinatetewa au kupiganiwa kidhaifu, Chenye nguvu kinapaswa kujitetea chenyewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumtetea Mungu ni sawa na watu fulani ambao wakifikaga airport wakati wa ukaguzi ukifungua masanduku na mabegi yao utasikia wanakwambia “polepole usije ukwmharibu Mungu wangu”

[emoji87][emoji87] imagine

Kwa hiyo Mungu wa watu fulani analindwa ma kutunzwa na binadamu sasa hapo anaepaswa kuabudiwa ni nani ?

Mungu ababebwa kwenye begi au sanduku?

Mungu analindwa na binadamu?

Inashangaza sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za punde zinasema watu 3; wote walimu wamauawa mapema leo kufuatia uvamizi watu wanaoaminiwa kuwa wanamgambo wa kundi la al Shabaab.

Tukio hilo lilitokea 3 am Jumatatu, Januari 13 katika Kamuthe Resource Centre mjini Garissa. Katika shambulizi hilo mnara wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom uliharibiwa.

Pia gari la polisi liliharibiwa kwa kuteketezwa moto. Maafisa wa polisi wanafuata nyayo za wavamizi hao huku kukiripotiwa huenda wanamgambo ao wamefukia ardhini vilipuzi ambvyo huenda vikatatiza polisi wanaowafuata.

Chanzo: TUKO
Hizi ni nyakati ambazo ungetarajia East African community isimame kwa pamoja kukataa ushenzi huu. Ni wakati ambapo tungepima nia njema ya huu ushirikiano kwa kusimama pamoja na kupambana na hili janga kuliko kuliona kama ni la wakenya peke yake.

Why EAC? Leo magaidi wanatamba Kenya, lakini nasema kweli kabisa, kesho mtawasikia Tanzania, Uganda, Burundi etc. Sasa kama hatutakaa chini na kupanga stratergy ya pamoja ili kukabili na kuliondoa tatizo hili wakati likiwa bado upande mmoja, tutalipa gharama kubwa baadaye.

Sote tunajua kuwa kwa sasa Somalia ni breeding ground kwa hawa terrorists, lakini tumekaa kama vipofu tukishabikia masahibu yanayowakuta ndugu zetu wakenya. Ifikie kipindi jumuiya hii iwe na uwezo wa kutatua instability kwenye ukanda wake, kwani itaathiri sana uchumi wetu.

Ningefurahi kusikia wakuu wa nchi za EAC wakiketi pamoja kutafuta namna ya kumaliza tatizo la Somalia. Tuwaache wamarekani washughulike na ya kwao, Africa for africans.

Natoa hoja.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Hapo nadhani suluhisho ni kenya kuondoa majeshi yake kule na Kupambana kulinda mipaka yake na ni kitu ambacho wakenya wengi wanakitaka, lakini serikali ya Kenya inaona aibu kuyaondoa majeshi yake kule maana walikurupuka,
Hivo hizo lawama unazoipa EAC wala hazina mashiko yoyote.
 
Sio kweli mkuu, serikali ya Kenya inatenda kwa ujasiei mkubwa na kufuata kanuni sahihi za kulinda maslahi mapana ya nchi yake. Hebu tujiulize, hivi ni kweli kwamba wanajeshi wa Kenya wakiondoka Somalia mashambulizi ya kigaidi yatakoma? Kwa mtazamo wangu yafuatayo yatadhihirika:

1. Alshaabab watatangaza ushindi na ufalme wao kwa ukanda huu. Kushindwa kwa wakenya huko Somalia kutakuwa ni kushindwa kwa nchi zote zinazoizunguka Somalia, zikiwemo EA.

2. Kwa sababu hiyo Al shaabab watapata nguvu mpya (strong motive) kufanya mashambulizi zaidi ili ikiwezekana kujenga influence yao ndani ya Kenya. Kwenye hili nchi zoote za EAC haziwezi kuwa salama.

3. Serikali ya Somalia itaanguka mara moja ndani ya mikono ya Al shaabab na ndio itakuwa stagging ground kwa ajili ya future ops zao.

4. Kwa wanaofuatilia mgogoro huu, Al shaabab wana malengo ya muda mrefu, ikiwamo kuingia hata hapa Tanzania, hivyo watapata wakati mzuri kutekeleza malengo yao. Kwa sasa Kenya imekuwa kama buffer zone kwa sababu ni enemy at hand hivyo imebidi al shaabab washughulike nao kwanza.

5. Wakenya wataishi maisha ya hofu zaidi kuliko ilivyo hivi sasa, hali itabadilika pia kwa nchi za EAC. Hofu hii itakuwa kubwa kote kote, kumbuka wako watanzania wengi tu waliokimbilia huko kwa al shaabab. Tusijisahau sana.

Nashauri tena kuwa janga hili ni la EAC na sio sahihi kabisa kuwaachia wakenya peke yako.

Acha kuhusisha EAC, hivi kama wamepashindwa kule why wasi focus na kulinda mipaka yao?
Watu hawataki amani why walazimishwe?
Hilo swala walikurupuka mnoo na wanashindwa namna gani wajitoe,
Hizo zote ni bla bla tu.
 
Sio kweli, sema siwezi kuongea zidi kwa sababu naona ueelewa wako wa mambo ya kiusalama umetofautiana sana na mimi. Tuchukulie basi hilo ni lao, sisi tuko salama

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Sio kweli, sema siwezi kuongea zidi kwa sababu naona ueelewa wako wa mambo ya kiusalama umetofautiana sana na mimi. Tuchukulie basi hilo ni lao, sisi tuko salama

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Sawa
 
Back
Top Bottom