Kenya wameingiza Embroy ya Girolando(Gir) Dairy cow kutoka Brazili.

Kwenye mashamba ya ASAS hawapo hawa? Au ni mpaka wawepo kwenye ranch za taifa ie MABUKI etc.
 
Kuna mdau humu aliwataja na kutoa namba za simu kuwa wapo Tanga na Arusha!
 
..kwa Tanzania wapi unaweza kupata embryo za ng'ombe wa kisasa?
jaribu SUA miaka ya nyuma nilihudhuria nane nane dodoma walikuwa na sperm bank kubwa WANASEMA WANAHIFADI HATA KWA MIAKA HAMSINI, wana hata za nyati na ngombe mbalimbali duniani, kuna mzee yupo iringa alikuja na ng'ombe watano ni wakubwa haswa kuliko hata hiyo picha na mbegu alichukua kwao.
 
Hi breed kuna mmoja alishavunja world record kwa kukamuliwa lita 127 kwa siku yaani ndoo sita za lita 20 na kidogo ,

Mtu akiweza kuwaagiza ndama wengi akaja kuuza kama mbegu atapata hela sana ,
Hili swala lilipaswa kufanywa na serikali kupitia wizara ya kilimo, hao wakenya wananipa mashaka maana kiwango wanachotoa hakilingani na kiwango wanachotoa mbuzi wa brazil
 
Nilibahatika kuona ng'ombe wawili aliopewa zawadi Mw. Nyerere na chuo cha Sua.
Walikuwa wamehifadhiwa kwa rafiki yake baba ukubwa wake mpaka leo sijawahi kuona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…