Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kitu muhi.u kabisa ni hiki.Nimeona tangu juzi kupitia luninga ya ITV naibu waziri wa afya wa Kenya akitangaza maambukizi mapya ya Corona kwa raia wa Tanzania ambao ni madereva.
Msingi wa swali langu ni kwanini Kenya inawatangaza ilhali haiwatibu?
Kwa mfano leo wametangaza kuwapima madereva nane ambao wamekutwa na Corona na kwamba wamerudishwa Tanzania.
Sasa hiyo idadi kwa mujibu wa takwimu za WHO itasomeka kuwa ni maambukizi ya Corona nchini Kenya au Tanzania?
Maendeleo hayana vyama!
Wamesema ukweli au uongo?
Kama ni kweli, hakuna shida.
Pia, walipima watu waliotaka kuingia Kenya. Hawakuja Tanzania kupima Watanzania wasiotaka kuingia Kenya.
Mikataba ya kimataifa ya mambo ya afya inazitaka serikali zote kutoficha habari za milipuko ya magonjwa.
Sasa hapa swali la kuuliza si kwa nini Kenya inatoa habari hizi.
Swali ni, kwa nini serikali ya Tanzania inaficha habari hizi?
Kwa nini watu wa Tanzania kugunduliwa inabidi mpaka waende mipakani?
Sent using Jamii Forums mobile app