Kenya wateta unafiki wa Profesa Kabudi kuipa Kenya kisomo dhidi ya ukabila

Kenya wateta unafiki wa Profesa Kabudi kuipa Kenya kisomo dhidi ya ukabila

Wakenya Wana akili Hadi wanaudhi. Wamegundua kuwa macho ya palamagamba Ni Kama ya paka mwanga.
 
Huyu mwandishi kaamua kwa makusudi kuikashifu Tanzania na viongozi wake wakuu hivyo apuuzwe maana haya ni maoni yake binafsi na sio ya Wakenya waliomualika Kabudi.
Haya uliyoandika nayo ni maoni yako. Sasa unataka tumpuuze mwandishi kwa maoni yake?
Kwanini tusianze na wewe?
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Haya uliyoandika nayo ni maoni yako. Sasa unataka tumpuuze mwandishi kwa maoni yake?
Kwanini tusianze na wewe?
Huyo Jamaa anatakiwa apuuzwe sababu anajifanya msemaji wa Wakenya wakati hawajamtuma kuandika hayo.
 
Hongera kwa kuliona hilo lakini pia kuna shida zilitokea huko Kenya hata baada ya kuipata Katiba mpya mpaka mizozo ikawa mibaya. Katiba mpya haifanyi kitu chochote kama hakuna Political Will au utashi wa kisiasa kwenye jambo lenyewe. Ni kama vitabu vitakatifu vipo ( Biblia na Quoran) vinakataza kufanya mabaya lakini yanafanyika tu.
Alafu jambo lingine wenzetu kwa upande wa upinzani wanapaswa kulijua ni kwamba kususia uchaguzi halisaidii sana mana kama kule Znz walisusia uchaguzi kwa hiyo munawalahisishia upande wa chama tawala mambo yao yaende vizuri bila upinzani wowote. Make sure munawapa "tuff time" sio KITONGA style kama inavyotokea.

Ni kheri kususia kuliko kushiriki katika uchaguzi ambao 96% ya wagombea wako wamekatwa, hapo unashiriki ili iwe nini.

Waache washinde freely bila ya kupingwa kuliko kushiriki katika mazingira yatakayowapa hizo hizo 99.99% na itakuwa mmewapa justification, ni sawa na kupambana na mtu ana machine gun wakati wewe hauruhusiwi hata kutumia mawe. Ni upuuzi wa hali ya juu.

Kenya kwenye utawala bora,utawala wa sheria na haki za raia wametuacha mbali sana. Hii inachangiwa pia na exposure na elimu.
 
Phillipo Bukililo, Ndiyo maana tunasema Kabudi ni mnafiki.

Utawezaje kwenda kumshauri jirani yako ambaye zamani alikuwa na tatizo la chuki katika familia yake na sasa ameondoa chuki na anaweka mikakati ya kuhakikisha chuki hairudi tena kwenye familia yake. Lakini wewe zamani chini ya mkuu wa familia mwingine kulikuwa hakuna chuki, baada ya wewe kuchukua uongozi wa familia umeamua kujenga chuki kwa nguvu zote? Umefuta uelewano wote ambao zamani familia ilikuwa nao.

Ambacho wewe kwako umeona hakina maana, umeamua kukifuta, utawezaje kumfundisha mtu mwingine akizingatie unachokiona siyo muhimu?

Sidhani kama kumewahi kuwepo kipindi chochote kile katika Taifa letu tumewahi kuwa na viongozi wanaopenda chuki na upendeleo kama awamu hii. Kwa sasa kila anayepinga au kukosoa chochote kinachofanywa na serikali, Rais au kiongozi wa CCM, ni adui mkubwa wa serikali. Huyo inaonekana hastahili hata kuishi. Unaoenda kuwashauri, hawana huo ujinga. Halafu unaenda kuwaambia wavumiliane. Mbona wewe umeshindwa kuvumia mawazo ya wengine nchini kwako?

Kama Kabudi ana ujasiri basi aende mbele ya Rais amwambie kuwa 'unachofanya siyo sahihi. Unatakiwa kuwa mvumilivu kusikia hata usiyoyapenda. Ndiyo faida ya kuwa wengi. Kila mmoja anafikiri tofauti'.
 
Phillipo Bukililo,
Kabudi ni mpuuzi kwakuwa aliongea unafiki mtupu, matatizo ya nepotism yaliyopo Bongo na ambayo yanaku kwa kasi ndiyo anapaswa kuyazungumzia kabla hajakimbilia mambo ya majirani ambao wanaendelea kutatua dosari zao hatua kwa hatua.
 
Eti kilichomfanya siku ile kuhama kutoka kiswahili na kuzungumza lugha ya malkia Ni nini!!!!!!.Lugha ya kiswahili alizungumza vizuri(ila Kuna mahali alisema NACHUKUA NAFASI HII)..sijui Kwa wataalam wetu wa kiswahili kama alikuwa sahihi watanisaidia...ila msemakweli mpenzi wa Mungu Waziri Yuko vizuri..anajua kujieleza vizuri na kikubwa ana ufahamu Mkubwa wa historia ya mambo mbalimbali...(ila Waziri siku nyingine ukiamua kutumia Kiswahili au lugha ya malkia..tumia mwanzo mwisho
Kabudi historia anaijua sana ya Tanzania na Africa tena sio kwa juu juu tu anaweza kukupa na sababu za logic kwanini vitu fulani vipo vilivyo leo au kwanini watu wanafanya mambo fulani; ukatoka umejifunza jambo jipya.

Lakini namna yake ya uwakilishi unawalakini mkubwa he just doesn’t know how to address an audience politely and has poor choice of words.
 
Viongozi wa CCM wanatudhalilisha Watanzania wote.
Screenshot_20191204-162902.jpeg
 
Kwa hivyo ni unafiki mkubwa kwa kina Palamambanga kuwapa mwaidha wakenya kuhusu uongozi bora na ukabila ikiwa nchi yake inaendeleza uovu huo.Kweli nyani haoni kundule!
Kama nilivyoahidi kurudi kwenye mada hii, nimeona nianzie mwisho wa andiko kama alivyoliwasilisha mleta mada; kwa maana maneno ya mistari hiyo miwili ndio hasa ilistahilri iwe hoja ya mwandishi, na sio kuishambulia Tanzanaia.

Nitaeleza, lakini kwanza nimueleze mwandishi kwanza.

Kiswahili: Mwandishi anataka aonekane anaimudu lugha ya kiswahili, na kama nilivyoeleza mara ya kwanza, kajitahidi vya kutosha. Ila, mtu aliyezaliwa na kukulia Nyeri au Kiambu kujifanya kuwa na lugha ya kiunguja au Kwale ni kazi ngumu sana.
Kwa hiyo katika maandishi yake kuna maneno na miundo ya sentensi ambayo inaweza kumpa msomaji matatizo. Nitatoa mifano:
Kwenye kichwa cha habari katumia neno 'kinaya' - sielewi hapa ana maana gani, au alikuwa na maana ya "kinyaa" au "kinai"?
Maneno 'alitowa, ilosheheni, ukwasi wa luhga, mahanjani mengi ya kiabunuasi...
Misemo isiyoendana na mifano, 'akibwabwaja kama cherehani ya kijerumani...
Maneno: 'twaweza, twasema, twaona...
Nikiri, sikutumia kamusi, lakini nina wasiwasi na 'changamoto sufufu'
Sijui 'swala la sugu
' lina maana gani, kama ilivyo 'ziada ya yote'...

Kwa hiyo, mwandishi asitake kujionyesha yeye ni mjuaji wa kiswahili cha kiunguja huku hana uwezo nacho.
Anataka watu waone kiremba cha sultan wa kiarabu kuwa ni sawa na kile cha singa singa. Hapana, hivi ni vilemba mbalimbali kabisa.

Lakini tukiacha usanifu wa lugha, kuna jambo mhimu la kujua mwandishi anao upeo kiasi gani katika anayoyaandika hata katika kusoma lugha anavyoitumia, hata kama sio lugha aliyoizoea.
Katika maandishi yake ametaka kutuonyesha jinsi gani kenya walivyoelimika kuliko Tanzania. Sasa kutokana na yaliyoandikwa kwenye mada hili inadhihirisha kwamba mwandishi hana elimu ya kipekee sana kuwazidi waTanzania ambao anataka wamsome na waone mfano wa elimu yake iliyofana.

Nimemalizana na kumchambua mwandishi, ngoja niende kwenye hoja alizoleta tuzisome.

Ukirudi kwenye ule mstari wa juu kabisa niliom'quote', "Kwa hiyo ni unafiki mkubwa kwa kina Palamagamba kuwapa mawaidha (?)wakenya kuhusu uongozi bora na ukabila ikiwa nchi yake inaendekeza uovu huo. Kweli nyani haoni kundule".

Mimi nisingetatizwa na lolote kama mada yake ingejikita kwa hao viongozi, akina Palamagamba na aliyemtuma kwenda huko. Pengine nami ningejiunga katika kushangilia mada yake. Lakini yeye kwa sababu zake kaamua kushambulia nchi, Tanzania na kuifanya ionekane kuwa na madhaifu waliyonayo huko kwao. Hili ndilo sikubaliani nye, hasa anapomlinganisha Mwalimu Nyerere, na kiongozi wao Jomo Kenyata, mlinganisho ambao ni usiku na mchana na nitaeleza hapa chini.

Lakini kwanza nimuulize mwandishi: hivi Kalamaganda kafikaje huko Kenya? Alialikwa, au alijipeleka mwenyewe?
Na kama alialikwa (sijui na nani), kulikuwa na sababu za kumwalika hadi kumpa nafasi ya kutoa hotuba? Mbona majirani zenu wengine hamkuwaalika. Somalia ipo hapo jirani, Ethiopia, Sudan Kusini, Uganda, na hata Rwanda na Burundi, mbona hatuona wakiwepo hapo, ila mkaona waalikwe viongozi toka Tanzania, kwa nini?

Mleta mada, naomba ulijibu hili swali.

Mimi ninayo majibu ya swali hilo, lakini ngoja niyabakishe kapuni kwanza, nisikie wewe unasemaje.

Nisilifanye hili andiko liwe refu sana na kuwachosha wasomaji. Ngoja haraka haraka niandike kidogo juu ya Mwalimu Julius Nyerer na Mzee Jomo Kenyatta, kwa sababu mleta mada katoa shutuma zisizostahili kabisa kwa Mwalimu.

Mwalimu alikuwa ni msomi mzuri sana, kwa hiyo asingeweza kuidharau elimu hata kidogo. Tanganyika wakati inapata uhuru wake 1961, kulikuwa na wasomi wachache sana Tanganyika kiasi cha kwamba hata watumishi serikalini ilikuwa shida sana kujaza nafasi. Wakati Mwalimu anang'atuka, Tanzania ilikuwa inasifika kwa kiasi cha wasomi ilioweza kuwaandaa na hata kuwa moja ya nchi zilizosifika barani afika kwa kuwezesha wananchi wake kujua kusoma na kuandika. Nafasi zote za juu maofisini zilikuwa zimeshikwa na waTanzania.
Jomo hakuwa na elimu ya maana, asingeweza kuweka juhudi za watu wasome. Tom Mboya ndiye anayejulikana kwa Kenya kuwezesha wat wasome, hasa ile 'Airlift' ya Marekani, ya akina Obama sr.
Hata sasa huwezi ukasema Kenya wamesoma kiasi cha kuwazidi waTanzania.
Naelewa mleta mada anapozungumzia maendeleo makubwa kenya, kwa sababu yeye anatazama tu pale Murang'a, au Kiambu, ama kwa yule binti pale Kirinyaga haangalii kabisa kuwa kuna Kilifi, au Turkana, au Kisumu, au Wajir, au Lamu, Kwale n.k. Hii ndio kawaida ya watu wa aina ya mleta mada ambaye najua kwa uandishi wake ni mtu wa 'Central.'

Wakati nyerere analijenga taifa moja la waTanzania, mzee Kenyatta alikuwa akiwalisha kiapo kikuyu wenzake pale Itchawele, ili wamlinde na wamsaidie kuwatawala makabila mengine.

Wakati Mwalimu akifanya kila juhudi kutafuta uhuru wa nchi zilizokuwa zimebaki katika ukandamizaji wa ukoloni, Mzee Kenyatta alikuwa akijishughulisha katika kupora ardhi za maskini kila sehemu ya kenya hasa kule Pwani na Rift valley.

Wakati Mwalimu Nyerere akitafuta njia za kujikwamua kutoka kwenye makucha ya unyonyaji, Mzee Kenyatta ndio alikuwa akishirikiana na hao waliopora ardhi ya wakenya. Makubaliano yenyewe ya kupata uhuru kenya, ulisisitiza 'settlers' waendelee kukalia ardhi walizopora wenyeji wa kenya na kuwafanya 'squarters' hadi hii leo'

Wakati Mwalimu Nyerere akipigana vita kumwondoa Nduli Amin. Mzee kenyatta ndio kwanza alikuwa akishiriki kuikabidhi kenya kuwa 'satellite' state na kuomba misaada ya kumkinga zidi ya nchi kama Somalia! Bila shaka mwandishi anamkumbuka vyema waziri Bruce McKenzie, na Attorney General Njonjo, au sio walivyotumwa kwenda Uingereza kuwalilia wakoloni wawape ulinzi.

Wakati Mwalimu anakataa masharti toka popote kwetu, mzee Kenyatta ndio kwanza anawakaribisha wamarekani na kuifanya Mombasa kuwa kituo cha wanamaji wa Kimarekani, na kule Laikipia, amesahau Waingereza hadi leo wapo?

Uchumi anaojigamba nao mwandishi umeshikiliwa kwa kiasi kikubwa na watu wa nje, Mashamba makubwa ya Chai, akina Williamson, James Finlay,n.k.; Hata Horticulture sasa hivi inayoingiza pesa nyingi, sehemu kubwa ni wageni, waholanzi wameshikilia maua. Aende Kisumu, Isiolo, Turkana, Kakamega, Homa Bay, Migori, nakwingineko, halafu aje atuambie hapa kuwa Kenya wameendelea.

Ukabila siwezi kuondoka bila kuuzungumzia, kwa sababu hili ndilo tatizo kubwa sana Kenya, pamoja na kwamba mwandishi anataka kulikana.
Lakini ngoja nimwambie tu kwa kifupi.
Tatizo kubwa la ukabila kenya linawahusu hasa Kikuyu. Pangetokea mtu (kiongozi) akajua jinsi ya kuwa'neutralize' hawa, Kenya ingepata nafuu sana. Moi aliwakandamiza, kidogo walikosa namna ya kufurukuta, lakini na yeye kaangukia kule kule alikoangukia Mzee Kenyatta, kaingiza ukabila wa kabila lao. Kikuyu kwa Kenya ni sumu kubwa sana, na bila ya kutafuta njia ya kuwazuia, siku zote litakuwa ni tatizo
Ukiangalia makabila mengine makubwa kama Luhya na Kamba, hawana tofauti yoyote na makabila mengine yaliyopo Tanzania. Na kwa bahati mbaya, Kikuyu wanawatumia hawa na kuwa'manipulate' nyakati za uchaguzi, kama ilivyofanyika wakati wa Kibaki.

Rushwa kwa Kenya ni jipu lisilo na dawa.

Nimalize kwa kusema haya. Hata katika ushirikiano wetu kati ya nchi zetu hizi za Afrika mashariki, matatizo yetu mara nyingi yanatokana na misuguano kati ya Tanzania na Kenya (sema kikuyu). Tanzania haiwezi kamwe kuangukia katika matatizo yanayotokana na watu wanaosababisha misuguano kati ya jamii. Walidhani watakuja hapa kupora ardhi wakakuta tupo macho, tena sana.
Kenya sasa hivi inafanywa kuwa 'outpost' ya mashirika na nchi za nje kuja kupora hapa. Hawatafanikiwa.

Mleta mada ni kazi yake kujua kwa nini Kalamaganda alipewa heshima ile ya kukaribishwa kwenye kikao kile. Kama yeye ni Kikuyu, ajue dawa yake inasukwa, na pengine ndio itakuwa nafuu kwa raia wa makabila mengine nchini Kenya. Kama mpango utafanikiwa.

Sikuhariri.
 
Ila mtoa mada angesifia kakitu kokote ingekuwa Wakenya wamkubali Jiwe. Poleni wana mapambio wa Lumumba.
Huyu mwandishi kaamua kwa makusudi kuikashifu Tanzania na viongozi wake wakuu hivyo apuuzwe maana haya ni maoni yake binafsi na sio ya Wakenya waliomualika Kabudi.
 
Kwa vipi?
Yaani huu upuuzi wa huyu aliyeandika sijui ni kiluhya au kiluo au kamba sijui kiwaterere warere ndo unaleta hapa. Ile hotuba aliyoitoa kabudi wewe hutawahi itoa mahali popote mpaka unamaliza mwendo wako hapa duniani.
 
Bams,
Hakuna chuki Tanzania. Ni kundi fulani la watu lilizoea kuishi kwa kula bata kwa kutumia aina fulani ya upendeleo uliozuka kuanzia awamu ya tatu.

Katika awamu hii kundi hili linarudishwa kwenye mstari kwa kukumbushwa kuwa keki ya taifa ni ya wote haipo kwa ajili ya watu fulanj wachache.

Baada ya kundi hili kukumbushwa juu ya uhalisia basi imekuwa nongwa, ndio tunasikia haya malalamiko ya udikteta na haki za binadamu.

Kundi hili linajaribu kujenga picha mbaya kimataifa lakini haliwezi kufanikiwa kwani nchi hii inao ulinzi wa Mungu.

Ni Tanzania hii ya awamu ya tano ambapo wafipa wanaishi Tanga bila hofu. Wagogo wanaishi Kagera bila hofu. Wachagga wapo Ruvuma bila hofu.

Kabudi anayo mamlaka kimaadili kuongea alichoongea pale Kenya. Hizi kelele za chuki zinatoka kwa watu waliojisahau wakadhani kufanikiwa kimaisha ni haki yao tu, na sio haki ya kila mtanzania.
 
HIVI HAPA KABIDI HAKUINGILIA MAMBO YA NCHI NYINGINE?
Alitoa ushauri kama unavyoweza kumshauri jirani yako kuhusiana na lolote lile kimaisha.

Bill Clinton alishawahi kwenda Russia na akatoa ushauri juu ya masuala ya kidemokrasia.
 
Hivi hapa kwenye hii thread kuna mkenya?

mbona woote mleta mada,wachangiaji ni watanzania?

Hivi kenya inayoongelewa hapa ni ipi?
sio ile wanayouwana kwa maelfu kama sio mamia kila baada ya uchaguzi?

sio kenya ile waliyomuua Chriss musando msimamizi wa IT wa tume ya uchaguzi ya kenya wakati huo.?

kenya ina lipi la kutusema watanzania?
au huyu ni tundu lizzu kaanza kuwaandikia wakenya kuwalisha maneno?

shame on all of wasaliti.

mtaropoka mpaka mdondoshe ulimi lakini JPM Yupo hadi 2025[emoji1241][emoji818]
 
Alienda kufundisha kuchamba wakati yeye na kundi lake hawachambi
 
Kabudi ni mpuuzi kwakuwa aliongea unafiki mtupu, matatizo ya nepotism yaliyopo Bongo na ambayo yanaku kwa kasi ndiyo anapaswa kuyazungumzia kabla hajakimbilia mambo ya majirani ambao wanaendelea kutatua dosari zao hatua kwa hatua.
Leo ndio inaonekana nepotism!! Enzi za Mkapa na Kikwete hamkiona nepotism!!.

Tuachane na haya maisha ya kinafiki, duniani hakuna administration ya nchi ambayo kiongozi mkuu hana watu wake wa karibu kwenye nafasi nyeti.

Ukiona kiongozi mkuu hana wasiri wake katika watu wenye vyeo nyeti ujue huyo hafai kuwa kiongozi mkuu, na hiyo sio nepotism.

Nyerere alikuwa na Butiku, Warioba na Nyirabu.

Mwinyi alikuwa na Marehemu Diria.

Kila kiongozi anao watu wake anaowaamini.
 
Back
Top Bottom