eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,807
- 16,477
Wewe ndo mpangaji wa ratiba za hapa Duniani?
Unajua maana ya ratiba?
Wewe ndo mpangaji wa ratiba za hapa Duniani?
Kwa vipi?
Ni kujihisi tu, mnatafuta sababu za malalamiko yasiyo na ulazim. Miaka ya Mkapa pale TRA kulikuwa na wakurugenzi nane wenye kutoka kabila moja la kaskazini.Sasa kama huko nyuma kulikuwa na nepotism ndiyo iwe justification ya Magu kuiendeleza? Tena anai'upgrade kwa kasi sana, let's call spade a spade kuwa afanyacho ni kibaya na kinatia nyufa katika mshikamano wa taifa.
Trustees si lazima wawe watu wa kijijini kwenu tu au wa kabila lenu tu.
ukabila ndio uliowasaidia kenya kama sio ukabila wengekuwa wanakhanisiwa na Kanu kama ccm inavyowakhanisi wabongoWakenya ni kweli ukabila umewasumbua kwa miaka mingi tangu wapate uhuru. Tatizo ukweli huwa huchukua upande moja na huwa unauma unaposemwa hadharani.
Sisi hatuna ukabila na tumekuwa hivyo kwa miaka mingi. Nyerere alikuw mzanaki Kawawa alikuwa mngoni.
Magufuli mtu wa Chato, Samia mzanzibari Kassim mtu wa Ruangwa, hatuna asili ya vyama vya kikabila.
Kenya mpaka kuwa na katiba mpya walikufa watu zaidi ya 1000 chanzo kikiwa ni siasa mbovu za kikabila.
Kabudi aliongea kwa nia ya kujenga umoja kulingana na dhima ya jambo lililompeleka kule, tatizo letu wabongo ni lile lile la negative mindset kwenye kila jambo tunaloliongelea.
Kabudi aliongea aliyoyaongea, jee hapa kwetu kuna nia njema ya kuepuka siasa za mpasuko wa kikabila na kimajimbo? Tuache kuwa lecture Wakenya kana kwamba sisi hatuna mengi ya kujifunza kutoka kwao.Wakenya ni kweli ukabila umewasumbua kwa miaka mingi tangu wapate uhuru. Tatizo ukweli huwa huchukua upande moja na huwa unauma unaposemwa hadharani.
Sisi hatuna ukabila na tumekuwa hivyo kwa miaka mingi. Nyerere alikuw mzanaki Kawawa alikuwa mngoni.
Magufuli mtu wa Chato, Samia mzanzibari Kassim mtu wa Ruangwa, hatuna asili ya vyama vya kikabila.
Kenya mpaka kuwa na katiba mpya walikufa watu zaidi ya 1000 chanzo kikiwa ni siasa mbovu za kikabila.
Kabudi aliongea kwa nia ya kujenga umoja kulingana na dhima ya jambo lililompeleka kule, tatizo letu wabongo ni lile lile la negative mindset kwenye kila jambo tunaloliongelea.
Huyu mwandishi kaamua kwa makusudi kuikashifu Tanzania na viongozi wake wakuu hivyo apuuzwe maana haya ni maoni yake binafsi na sio ya Wakenya waliomualika Kabudi.
Huyo Jamaa anatakiwa apuuzwe sababu anajifanya msemaji wa Wakenya wakati hawajamtuma kuandika hayo.
Kiongozi wetu mkuu anazo kauli kali na zenye kuogopesha, lakini bahati njema tunao wazee watatu, na siku zote nyumba yenye wazee huwa inaweza kuikwepa misukosuko.Kabudi aliongea aliyoyaongea, jee hapa kwetu kuna nia njema ya kuepuka siasa za mpasuko wa kikabila na kimajimbo? Tuache kuwa lecture Wakenya kana kwamba sisi hatuna mengi ya kujifunza kutoka kwao.
Hivi hapa kwenye hii thread kuna mkenya?
mbona woote mleta mada,wachangiaji ni watanzania?
Hivi kenya inayoongelewa hapa ni ipi?
sio ile wanayouwana kwa maelfu kama sio mamia kila baada ya uchaguzi?
sio kenya ile waliyomuua Chriss musando msimamizi wa IT wa tume ya uchaguzi ya kenya wakati huo.?
kenya ina lipi la kutusema watanzania?
au huyu ni tundu lizzu kaanza kuwaandikia wakenya kuwalisha maneno?
shame on all of wasaliti.
mtaropoka mpaka mdondoshe ulimi lakini JPM Yupo hadi 2025[emoji1241][emoji818]
Ndio. Na nilisema 'sikuhariri'. 'Dhidi' ninaifahamu vyema.He he heeeeee! Mwalimu wa Kiswahili, uwafundishaye jirani zetu lugha adhimu. Sio kwamba una vyeti feki mwalimu?
Ndugu mwalimu, neno sahihi la Kiswahili lenye kumaanisha versus ni DHIDI sio ZIDI.
Kiongozi wetu mkuu anazo kauli kali na zenye kuogopesha, lakini bahati njema tunao wazee watatu, na siku zote nyumba yenye wazee huwa inaweza kuikwepa misukosuko.
Pamoja na hiyo misukosuko ya kisiasa sisi bado tunayo sauti yenye kuheshimika tunapoongea mbele ya wakenya.
Jiulize, ni kwanini katika tukio muhimu la kisiasa kwa majirani zetu hawakuona ni muhimu kuwaalika marais wa nchi kama Somalia, Sudan, Uganda na hata Rwanda.
Kinaya kwa Tanzania kuipa Kenya kisomo dhidi ya ukabila
Majuzi katika kongamano la kitaifa la mchakato wa kuunganisha nchi al maaruf BBI (Building Bridges Initiative) kule Bomas, Nairobi kulizuka mgeni wa nchi jirani aliyehutubu na kuacha maswali mengi kwa wadadisi wa kisiasa.
Bwana huyu ni Waziri wa mambo za nchi za nje wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi. Sambamba na hulka na sifa za watanzania alitowa hotuba ilosheheni ukwasi wa lugha teule ya Kiswahili na mahanjam mengi ya kiabunuasi. Akibwabwaja kama cherahani ya Mjerumani mfano wa baba yao wa taifa Julius Nyerere bwana huyu mwenye macho makubwa ya kung’ara kama bundi ama paka mwanga alisema mengi ambayo ni ya kutatanisha.
Aidha aliwaomba wakenya waache ukabila na kuungana huku akidai kuwa huo ni ujumbe wa kiongozi wake John Pombe Magufuli ambaye alimtajataja zaidi ya maradufu mfano wa nukuu za kitabu kitakatifu.
‘Hebu simameni na kila mmoja ashike mkono wa mwenzake na kusema hatutaki ukabila’ aliropoka bwana huyu kama aliyepandwa na maruhani ya kikwao na kulazimu waliomo kusimama kama wanajeshi kambini wakiwemo Rais Uhuru,Ruto na Raila. Palamagamba alidai kuwa viongozi hao watatu yaani Uhuru, Ruto na Raila ndio wanaosimamia Kenya.
Je, alimaanisha kuwa bila hawa watatu hakuna nchi? Sidhani. Tukitathmini hotuba ya Palamagamba twaweza kusema kuwa imetoka kwa mtu ambaye hastahili kamwe kusema aliyoyasema. Twasema kuwa Tanzania haina sifa ya kuwapa wakenya mawaidha kuhusu utawala bora ama kuhusu athari za kikabila kwani ina changamoto hizo zinazotokota ndani kwa ndani.
Tukipima Tanzania na Kenya twaona kuwa kuna tofauti kubwa za kihistoria na hususan kmaendeleo iwe kisiasa, kijamii na kiuchumi. Ukweli usiofichika ni kuwa siasa za Kenya ni kali kushinda za Tanzania.
Hii ni kwa sababu wakenya wameelimika zaidi na hivyo kujua haki zao mapema kuliko watanzania. Watanzania wameanza kuamka majuzi kutoka katika maisha ya kale kwani hata elimu yao ni duni. Mwalimu Nyerere atalaumiwa kwa kutozingatia elimu kwa watanzania.
Mwalimu Nyerere alihimiza siasa za kichina za ujamaa na kujitegemea huku akiwadanganya watanzania wakae vijiji vya ujamaa badala ya kujikuza kimataifa. Upande wa Kenya Jomo Kenyata aliboresha elimu kwa wakenya bila hiyana , wivu, uoga ama shaka za Nyerere na wengi wakaelimika huku watanzania wakiboresha lugha ya Kiswahili, Matokeo ni kwa wakenya kuerevuka zaidi na hivyo kujua haki zao mapema kuliko watanzania waliokuwa katika maisha ya kishamba ya kilimbukeni.
Ajabu Nyerere sungura mjanja alielimika hadi chuo kikuu lakini hakutaka watanzania wasome akihofia wangetisha uongozi na falsafa yake mbovu ya ujamaa ambayo mwisho aliikana na kukiri alifeli !. Swala la ukabila ni la kidunia.Karibu kila nchi kuna ukabila.Kenya ukabila uko lakini umedhibitiwa kwa sababu wakenya wanajali na kulinda nchi yao ingawa ukabila uko.
Kenya haijakuwa kama Rwanda ambapo karibu watu milioni moja waliangamia katika mauaji ya halaiki ya 1984. Tukumbuke Rwanda ni ndogo na ilihusisha makabila mawili tu ya Hutu na Tutsi ilihali Kenya ina makabila takriban 43. Tanzania ina makabila zaidi ya 100. Twaweza kusema changamoto za kikabila ziko kila mahali lakini huzidi katika nchi yenye makabila machache ama moja lenye nguvu na watu wengi linalotaka kutawala makabila mengine.
Wingi wa makabila Tanzania ambayo mengi ni madogo madogo dhaifu pia hupunguza ukabila tofauti na Kenya ambapo makabila makubwa ni machache lakini yenye nguvu kama wakikuyu na waluo. Ni kinaya kikubwa kwa Tanzania kuwapa wakenya mawaidha ya kuacha ukabila kwani wao pia wana changamoto sufufu za kisiasa ambazo hazijatatuliwa na chama cha kidikteta cha mapinduzi -CCM.
Rais Magufuli anaonekana ni kiongozi wa kiimla ambaye anawahangaisha waandishi wa habari kwani anapenda kusifiwa lakini hapendi kukosolewa. Bwana huyu mfupi wa miwani kama daktari wa kibaniani amelaumiwa na asasi za kulinda haki za binadamu za kimataifa kama AMNESTY kwa kuwatesa , kuwafurusha, kuwafunga na hata kuwaua waandishi wa habari na wakereketwa wa kisiasa.
Swala la sugu la Zanzibar pia ni kero Tanzania kwani wazanzibar wamelalama kuwa hawana haki kwa kunyanyaswa kila uchao hadi kudaI taifa lao huru. Tanzania mpaka sasa wanajikokota katika kutekeleza ama kuwa na katiba ya taifa ilivyo Kenya.Hapa Kenya imekuwa nchi ya pekeeAfrika kuwa na katiba mpya ya wananchi. Ziada ya yote viongozi kwenye utawala wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta wamewashirikisha wapinzani katika mwelekeo wa taifa kwa mfano Raila Oginga.
Mbona Magufuli hataki kuwashirikisha wapinzani kina Augustine Mrema wa TLP, Freeman Mbowe wa Chadema, Sheikh Shariff Hamad wa CUF alivyofanya Uhuru kwa Raila? Majuzi vyama vya upinzani vilisusia uchaguzi ambapo chama tawala cha CCM kilishinda karibu viti vyote.Kiongozi wa Chadema Freeman Mbowe asema walisusia kwa kunyanyaswa na gandamizi za Magufuli. Kwa hivyo ni unafiki mkubwa kwa kina Palamambanga kuwapa mwaidha wakenya kuhusu uongozi bora na ukabila ikiwa nchi yake inaendeleza uovu huo.Kweli nyani haoni kundule!
Uliloliandika hulijui zaidi ya kuongozwa na chuki binafsi kwa serikali ya awamu ya tano.Hana lugha ya kumuogopesha yoyote zaidi ya kauli za kinafiki na matendo ya kujenga chuki. Hakuna aliyemuita Kabudi, bali alikuwa huko Kenya kwenye mambo mengine, kwa bahati ndio hilo jambo likaweko hivyo Uhuru akamualika. Wakenya wanatujua na unafiki wetu wote na wanajua ni jinsi gani haturidhiki na mambo ila ni makondoo wa kiwango cha juu.
Uliloliandika hulijui zaidi ya kuongozwa na chuki binafsi kwa serikali ya awamu ya tano.
Kama nilivyoahidi kurudi kwenye mada hii, nimeona nianzie mwisho wa andiko kama alivyoliwasilisha mleta mada; kwa maana maneno ya mistari hiyo miwili ndio hasa ilistahilri iwe hoja ya mwandishi, na sio kuishambulia Tanzanaia.
Nitaeleza, lakini kwanza nimueleze mwandishi kwanza.
Kiswahili: Mwandishi anataka aonekane anaimudu lugha ya kiswahili, na kama nilivyoeleza mara ya kwanza, kajitahidi vya kutosha. Ila, mtu aliyezaliwa na kukulia Nyeri au Kiambu kujifanya kuwa na lugha ya kiunguja au Kwale ni kazi ngumu sana.
Kwa hiyo katika maandishi yake kuna maneno na miundo ya sentensi ambayo inaweza kumpa msomaji matatizo. Nitatoa mifano:
Kwenye kichwa cha habari katumia neno 'kinaya' - sielewi hapa ana maana gani, au alikuwa na maana ya "kinyaa" au "kinai"?
Maneno 'alitowa, ilosheheni, ukwasi wa luhga, mahanjani mengi ya kiabunuasi...
Misemo isiyoendana na mifano, 'akibwabwaja kama cherehani ya kijerumani...
Maneno: 'twaweza, twasema, twaona...
Nikiri, sikutumia kamusi, lakini nina wasiwasi na 'changamoto sufufu'
Sijui 'swala la sugu' lina maana gani, kama ilivyo 'ziada ya yote'...
Kwa hiyo, mwandishi asitake kujionyesha yeye ni mjuaji wa kiswahili cha kiunguja huku hana uwezo nacho. Anataka watu waone kiremba cha sultan wa kiarabu kuwa ni sawa na kile cha singa singa. Hapana, hivi ni vilemba mbalimbali kabisa.
Lakini tukiacha usanifu wa lugha, kuna jambo mhimu la kujua mwandishi anao upeo kiasi gani katika anayoyaandika hata katika kusoma lugha anavyoitumia, hata kama sio lugha aliyoizoea.
Katika maandishi yake ametaka kutuonyesha jinsi gani kenya walivyoelimika kuliko Tanzania. Sasa kutokana na yaliyoandikwa kwenye mada hili inadhihirisha kwamba mwandishi hana elimu ya kipekee sana kuwazidi waTanzania ambao anataka wamsome na waone mfano wa elimu yake iliyofana.
Nimemalizana na kumchambua mwandishi, ngoja niende kwenye hoja alizoleta tuzisome.
Ukirudi kwenye ule mstari wa juu kabisa niliom'quote', "Kwa hiyo ni unafiki mkubwa kwa kina Palamagamba kuwapa mawaidha (?)wakenya kuhusu uongozi bora na ukabila ikiwa nchi yake inaendekeza uovu huo. Kweli nyani haoni kundule".
Mimi nisingetatizwa na lolote kama mada yake ingejikita kwa hao viongozi, akina Palamagamba na aliyemtuma kwenda huko. Pengine nami ningejiunga katika kushangilia mada yake. Lakini yeye kwa sababu zake kaamua kushambulia nchi, Tanzania na kuifanya ionekane kuwa na madhaifu waliyonayo huko kwao. Hili ndilo sikubaliani nye, hasa anapomlinganisha Mwalimu Nyerere, na kiongozi wao Jomo Kenyata, mlinganisho ambao ni usiku na mchana na nitaeleza hapa chini.
Lakini kwanza nimuulize mwandishi: hivi Kalamaganda kafikaje huko Kenya? Alialikwa, au alijipeleka mwenyewe?
Na kama alialikwa (sijui na nani), kulikuwa na sababu za kumwalika hadi kumpa nafasi ya kutoa hotuba? Mbona majirani zenu wengine hamkuwaalika. Somalia ipo hapo jirani, Ethiopia, Sudan Kusini, Uganda, na hata Rwanda na Burundi, mbona hatuona wakiwepo hapo, ila mkaona waalikwe viongozi toka Tanzania, kwa nini?
Mleta mada, naomba ulijibu hili swali.
Mimi ninayo majibu ya swali hilo, lakini ngoja niyabakishe kapuni kwanza, nisikie wewe unasemaje.
Nisilifanye hili andiko liwe refu sana na kuwachosha wasomaji. Ngoja haraka haraka niandike kidogo juu ya Mwalimu Julius Nyerer na Mzee Jomo Kenyatta, kwa sababu mleta mada katoa shutuma zisizostahili kabisa kwa Mwalimu.
Mwalimu alikuwa ni msomi mzuri sana, kwa hiyo asingeweza kuidharau elimu hata kidogo. Tanganyika wakati inapata uhuru wake 1961, kulikuwa na wasomi wachache sana Tanganyika kiasi cha kwamba hata watumishi serikalini ilikuwa shida sana kujaza nafasi. Wakati Mwalimu anang'atuka, Tanzania ilikuwa inasifika kwa kiasi cha wasomi ilioweza kuwaandaa na hata kuwa moja ya nchi zilizosifika barani afika kwa kuwezesha wananchi wake kujua kusoma na kuandika. Nafasi zote za juu maofisini zilikuwa zimeshikwa na waTanzania.
Jomo hakuwa na elimu ya maana, asingeweza kuweka juhudi za watu wasome. Tom Mboya ndiye anayejulikana kwa Kenya kuwezesha wat wasome, hasa ile 'Airlift' ya Marekani, ya akina Obama sr.
Hata sasa huwezi ukasema Kenya wamesoma kiasi cha kuwazidi waTanzania.
Naelewa mleta mada anapozungumzia maendeleo makubwa kenya, kwa sababu yeye anatazama tu pale Murang'a, au Kiambu, ama kwa yule binti pale Kirinyaga haangalii kabisa kuwa kuna Kilifi, au Turkana, au Kisumu, au Wajir, au Lamu, Kwale n.k. Hii ndio kawaida ya watu wa aina ya mleta mada ambaye najua kwa uandishi wake ni mtu wa 'Central.'
Wakati nyerere analijenga taifa moja la waTanzania, mzee Kenyatta alikuwa akiwalisha kiapo kikuyu wenzake pale Itchawele, ili wamlinde na wamsaidie kuwatawala makabila mengine.
Wakati Mwalimu akifanya kila juhudi kutafuta uhuru wa nchi zilizokuwa zimebaki katika ukandamizaji wa ukoloni, Mzee Kenyatta alikuwa akijishughulisha katika kupora ardhi za maskini kila sehemu ya kenya hasa kule Pwani na Rift valley.
Wakati Mwalimu Nyerere akitafuta njia za kujikwamua kutoka kwenye makucha ya unyonyaji, Mzee Kenyatta ndio alikuwa akishirikiana na hao waliopora ardhi ya wakenya. Makubaliano yenyewe ya kupata uhuru kenya, ulisisitiza 'settlers' waendelee kukalia ardhi walizopora wenyeji wa kenya na kuwafanya 'squarters' hadi hii leo'
Wakati Mwalimu Nyerere akipigana vita kumwondoa Nduli Amin. Mzee kenyatta ndio kwanza alikuwa akishiriki kuikabidhi kenya kuwa 'satellite' state na kuomba misaada ya kumkinga zidi ya nchi kama Somalia! Bila shaka mwandishi anamkumbuka vyema waziri Bruce McKenzie, na Attorney General Njonjo, au sio walivyotumwa kwenda Uingereza kuwalilia wakoloni wawape ulinzi.
Wakati Mwalimu anakataa masharti toka popote kwetu, mzee Kenyatta ndio kwanza anawakaribisha wamarekani na kuifanya Mombasa kuwa kituo cha wanamaji wa Kimarekani, na kule Laikipia, amesahau Waingereza hadi leo wapo?
Uchumi anaojigamba nao mwandishi umeshikiliwa kwa kiasi kikubwa na watu wa nje, Mashamba makubwa ya Chai, akina Williamson, James Finlay,n.k.; Hata Horticulture sasa hivi inayoingiza pesa nyingi, sehemu kubwa ni wageni, waholanzi wameshikilia maua. Aende Kisumu, Isiolo, Turkana, Kakamega, Homa Bay, Migori, nakwingineko, halafu aje atuambie hapa kuwa Kenya wameendelea.
Ukabila siwezi kuondoka bila kuuzungumzia, kwa sababu hili ndilo tatizo kubwa sana Kenya, pamoja na kwamba mwandishi anataka kulikana.
Lakini ngoja nimwambie tu kwa kifupi.
Tatizo kubwa la ukabila kenya linawahusu hasa Kikuyu. Pangetokea mtu (kiongozi) akajua jinsi ya kuwa'neutralize' hawa, Kenya ingepata nafuu sana. Moi aliwakandamiza, kidogo walikosa namna ya kufurukuta, lakini na yeye kaangukia kule kule alikoangukia Mzee Kenyatta, kaingiza ukabila wa kabila lao. Kikuyu kwa Kenya ni sumu kubwa sana, na bila ya kutafuta njia ya kuwazuia, siku zote litakuwa ni tatizo
Ukiangalia makabila mengine makubwa kama Luhya na Kamba, hawana tofauti yoyote na makabila mengine yaliyopo Tanzania. Na kwa bahati mbaya, Kikuyu wanawatumia hawa na kuwa'manipulate' nyakati za uchaguzi, kama ilivyofanyika wakati wa Kibaki.
Rushwa kwa Kenya ni jipu lisilo na dawa.
Nimalize kwa kusema haya. Hata katika ushirikiano wetu kati ya nchi zetu hizi za Afrika mashariki, matatizo yetu mara nyingi yanatokana na misuguano kati ya Tanzania na Kenya (sema kikuyu). Tanzania haiwezi kamwe kuangukia katika matatizo yanayotokana na watu wanaosababisha misuguano kati ya jamii. Walidhani watakuja hapa kupora ardhi wakakuta tupo macho, tena sana.
Kenya sasa hivi inafanywa kuwa 'outpost' ya mashirika na nchi za nje kuja kupora hapa. Hawatafanikiwa.
Mleta mada ni kazi yake kujua kwa nini Kalamaganda alipewa heshima ile ya kukaribishwa kwenye kikao kile. Kama yeye ni Kikuyu, ajue dawa yake inasukwa, na pengine ndio itakuwa nafuu kwa raia wa makabila mengine nchini Kenya. Kama mpango utafanikiwa.
Sikuhariri.
PumbavuKinaya kwa Tanzania kuipa Kenya kisomo dhidi ya ukabila