Kenya wateta unafiki wa Profesa Kabudi kuipa Kenya kisomo dhidi ya ukabila

Kwa vipi?

Mkikuyu anadiriki kumlinganisha Nyerere na kenyatta ambaye amewauza watu wake utumwani. Wanaishi nchini mwao kama wakimbizi! Migogoro yote na jitihada zote wanazofanya ni kujaribu kusuluhisha, the so called Historical Injustice, ambayo ilisababishwa na kenyatta. Wale wataendelea na class struggle mpaka kiama. maana wanajua kwamba umasikini au matatizo yao yanatokana na wakikuyu. Hilo ni tatizo kubwa.
 
Ni kujihisi tu, mnatafuta sababu za malalamiko yasiyo na ulazim. Miaka ya Mkapa pale TRA kulikuwa na wakurugenzi nane wenye kutoka kabila moja la kaskazini.

Bosi mmoja akataja vigezo vya elimu vya hao waliokuwa na nafasi hizo. Vipi kama hao wanaopewa hizo nafasi awamu hii kama wanavyo vigezo vya kielimu, kuna ubaya gani wakapewa hizo kazi?.

Halafu kumbuka kuwa hilo kabila linalodaiwa kuwa ni la mheshimiwa Rais lina mikoa mitano, Simiyu, Geita, Mwanza, Shinyanga na Tabora, hao ni watu wengi sana na hilo ndilo kabila kubwa kuliko yote Tanzania, yaani wasipewe vyeo kwa sababu eti wakipewa Rais ataonekana anapendelea alipotoka!!.

Tuondokane na hizi mindsets nyepesi, tupo milioni 55 tunaelekea milioni 60, kila mwenye uwezo na elimu anahitajika mchango wake.
 
ukabila ndio uliowasaidia kenya kama sio ukabila wengekuwa wanakhanisiwa na Kanu kama ccm inavyowakhanisi wabongo
 
Kenya wana mabaya yao mengi sana yaliyojikita kwenye dhana ya ukabila... Bahati nzuri ni kuwa kule kwao ukabila ni jambo la wazi kabisa...!!
Ukija Tanzania... Hakika tumejitahidi...lakini ukweli tuuseme tu wazi... Ukabila upo maofisini, kwenye siasa, n.k.. Kama unabisha mwakani jaribu kuchukua fomu ukagombee ubunge huko ndani ndani kwenye Jimbo au jamii isiyo yako alafu utaletee majibu... Au jaribu kwenda huko ndani ndani ukaanzishe biashara au shughuli yoyote ya Maendeleo mfano kilimo!
Kwa mantiki hiyo ukabila upo..!!
Ila bado tuna moral authority ya "kuwakanya" ndugu zetu Wakenya juu ya ukabila nchini kwao...

Ukija kwenye tofauti za kiuchumi na mambo mengine mengi yanayogusa maslahi mapana ya jamii nadhani Tanzania nayo ina mengi ya kujifunza kutoka Kenya
Lakini je, tutaruhusu mtu wa nje (kutoka Kenya) aje atukaripikie kuhusu "maovu" yetu kama sisi tulivyofanya kwa Wakenya??
Eti, jamani Mkenya aje atuponde jinsi tunavyowadahalilisha wanafunzi kwa kisingizio Cha elimu bure?
Tunavyowakandamiza wanasiasa na wale wote wenye mawazo pinzani?
Aje aongelee jinsi tunavyowanyima wananchi fursa ya kufuatilia matukio ndani ya Bunge la nchi yao??
Tutamvumilia huyo mtu??!
 
Kabudi aliongea aliyoyaongea, jee hapa kwetu kuna nia njema ya kuepuka siasa za mpasuko wa kikabila na kimajimbo? Tuache kuwa lecture Wakenya kana kwamba sisi hatuna mengi ya kujifunza kutoka kwao.
 
Huyu mwandishi kaamua kwa makusudi kuikashifu Tanzania na viongozi wake wakuu hivyo apuuzwe maana haya ni maoni yake binafsi na sio ya Wakenya waliomualika Kabudi.

Sisi hatuangalii waliomuika Kabudi walikuwa wanataka nini, bali tunaangalia ukweli wa alichokisema huyu mkenya.
 
Ndio hivyo. Kwa maneno machache watu wanaambiwa "waache unafiki". Kwako moto unawaka halafu unajifanya kwenda kwa majirani kuwapa lecture uchwara ya namna ya kuishi pamoja. Huna hiyo moral authority, pimbi wewe.
 
Huyo Jamaa anatakiwa apuuzwe sababu anajifanya msemaji wa Wakenya wakati hawajamtuma kuandika hayo.

Yeye hahitaji kutumwa na mkenya yoyote, cha muhimu yeye ni mkenya na kuongea ukweli fullstop.
 
Kabudi aliongea aliyoyaongea, jee hapa kwetu kuna nia njema ya kuepuka siasa za mpasuko wa kikabila na kimajimbo? Tuache kuwa lecture Wakenya kana kwamba sisi hatuna mengi ya kujifunza kutoka kwao.
Kiongozi wetu mkuu anazo kauli kali na zenye kuogopesha, lakini bahati njema tunao wazee watatu, na siku zote nyumba yenye wazee huwa inaweza kuikwepa misukosuko.

Pamoja na hiyo misukosuko ya kisiasa sisi bado tunayo sauti yenye kuheshimika tunapoongea mbele ya wakenya.

Jiulize, ni kwanini katika tukio muhimu la kisiasa kwa majirani zetu hawakuona ni muhimu kuwaalika marais wa nchi kama Somalia, Sudan, Uganda na hata Rwanda.
 

Acha kupanic, mkenya kaongea ukweli wa wazi, hakuna mwanaccm anaweza kwenda kuwashauri wakenya kwa niaba ya watanzania. Yeye Kabudi aongee kwa niaba ya ccm na sio watanzania maana sio wote tunaaunga mkono madhalimu wanafiki.
 
He he heeeeee! Mwalimu wa Kiswahili, uwafundishaye jirani zetu lugha adhimu. Sio kwamba una vyeti feki mwalimu?

Ndugu mwalimu, neno sahihi la Kiswahili lenye kumaanisha versus ni DHIDI sio ZIDI.
Ndio. Na nilisema 'sikuhariri'. 'Dhidi' ninaifahamu vyema.
Basi furahi na hilo kosa.
 

Hana lugha ya kumuogopesha yoyote zaidi ya kauli za kinafiki na matendo ya kujenga chuki. Hakuna aliyemuita Kabudi, bali alikuwa huko Kenya kwenye mambo mengine, kwa bahati ndio hilo jambo likaweko hivyo Uhuru akamualika. Wakenya wanatujua na unafiki wetu wote na wanajua ni jinsi gani haturidhiki na mambo ila ni makondoo wa kiwango cha juu.
 

MM yangu nikua ukiwa kama Mkenya hukupaswa kutoa kasfa ulizo toa na matusi kama ulivyo tiririka pia Nyerere usinge mtaja kabisa,,Kabudi aliongea mengi sana ila ww uliona hayo tu,

nI HAYO TU
 
Uliloliandika hulijui zaidi ya kuongozwa na chuki binafsi kwa serikali ya awamu ya tano.
 
Wewe nae sijui unaongea nini yaani pamoja na figusu zote za serekali za mitaa huku liona hilo? Wapinzani wafanyeje?kama hakuna katiba ya warioba au uwepo wa tume huru usitegemee upinzani kukukomboa unapaswa uamke wewe, ukitaka mabadiliko inakubidi utoke uandamane maana nguvu ya umaa haijawahi kushindwa popote duniani na hii ipo kikatiba mkuu saa ya ukombozi ni sasa
 
Tena mwambie palamagamba ni kabila dogo sana liko katikati ya nchi tena mtanzania asilia wakafie mbali hawa jamaa siwapendi kama nini
 
Pumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…