Kenya wateta unafiki wa Profesa Kabudi kuipa Kenya kisomo dhidi ya ukabila

Sisi hatuangalii waliomuika Kabudi walikuwa wanataka nini, bali tunaangalia ukweli wa alichokisema huyu mkenya.
Haina ukenya wowote ni hawa hawa wa mitandaoni anatumia ujanja wa kitoto kujifanya mkenya ili apate kuongea aliyokusudia kuyaongea.
 
Chuki ya nini wewe pongo kuna mambo huhitaji ufundiswe ndiyo uyaelewe jiongez wewe popoma yaani taifa langu linaangamia kwa kukosa watu wenye maarifa ni wajinga tuu wanahamua wanaloamka lako kitandani sijui wanashauriwa na akina nani! vijana ndiyo mabadiliko ya mataifa yao hakuna cha chaguzi hapa ni maandamano tu ndiyo poa yetu. Vijana wamebakwa kifikra na wanasiasa wasiojua kesho yao.
Uliloliandika hulijui zaidi ya kuongozwa na chuki binafsi kwa serikali ya awamu ya tano.
 
Huyu mjinga gani ambaye hajiu Kiswahili na anaongea mambo asiyoyajua? Kenya kuna ukabila au hakuna?? Simple, kama upo, je umeleta madhara? Ndiyo. Kumbuka aftermath ya uchaguzi which claimed deaths of thousands. Huyu hajitambui. Somo hilo hata mtoto mdogo anaweza akawafundisha. Eti Nyerere nk. Anahusikaje na ukabila wenu?
 
Huenda walitaka tujifunze namna ya kukaa pamoja bila kujali tofauti zetu za kichama.
 
Wewe ndio popoma wa kiwango cha kimataifa. Mange aliitisha maandamano akiwa Marekani vijana wa rika lako walichofanya ni kujifungia ndani.
 
Huenda walitaka tujifunze namna ya kukaa pamoja bila kujali tofauti zetu za kichama.
Kukaa pamoja enzi za JK tulikaa pamoja mpaka watu wakanywa chai pamoja na pale ikulu, nini kilichofuatia.

Mbowe akasema Kikwete sio muaminifu wanaongea jambo moja anakwenda kutenda jingine. JPM kaona bora afunge vioo ajishughulishe na uboreshaji wa sekta ya afya na miundo mbinu ya kisasa ya mawasiliano.
 
Nchi zote ulizotaja ambazo hazikualikwa zimeshapitia misukosuko na upotevu wa maisha. Kwa hiyo si vibaya jirani yako akikukaribisha ili ujifunze umuhimu wa kukaa pamoja. Kumbuka baba wa taifa alituasa kuwa, Tanzania siyo kisiwa na tusijione tofauti. Amani yetu ni ya kulinda hata kwa kukaa pamoja na kunywa chai.
 
Hata kama mimi naishi kwa kuibia watu, hainizuii mimi kukuonya dhidi ya athari za wizi. Waweza sikia basi sikia, huwezi potezea endelea kuiba. Halafu uone siku ukikamatwa wewe kama nitafungwa mimi.
 
Very well said.
 
Wa kutufunza umuhimu wa kukaa pamoja sio Kenya mkuu Mansander. Alitufunza Mwalimu Nyerere miaka mingi iliyopita.

Sisi tulifuta uchifu baada tu ya uhuru mataifa mengi ya afrika yalishindwa. Kina Nigeria mpaka kesho wanatukuza uchifu matokeo yake utaifa wao ni dhaifu sana.

Magufuli mtazamo wake ni wa ukuzaji wa uchumi na anauonyesha kwa kuhakikisha nchi inafikika na kutokeka kwa urahisi.
 
Kenya haijakuwa kama Rwanda ambapo karibu watu milioni moja waliangamia katika mauaji ya halaiki ya 1984. Tukumbuke Rwanda ni ndogo na ilihusisha makabila mawili tu ya Hutu na Tutsi ilihali Kenya ina makabila takriban 43. Tanzania ina makabila zaidi ya 100. Twaweza kusema changamoto za kikabila ziko kila mahali lakini huzidi katika nchi yenye makabila machache ama moja lenye nguvu na watu wengi linalotaka kutawala makabila mengine.


Mchanganuo mzuri sana. Tanzania tunaanza kuano figisu figisu upendeleo upendeleo ,kabila kubwa- Wasukuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…