Rais Uhuru popote alipo ajue tutamhukumu vibaya sana akitanguliza maslahi ya uchumi mbele ya afya zetu, hili la Watanzania asilegeze chochote, kila Mtanzania anayekuja hapa lazima apanue mdogo na kutumbukizwa kifaa kupima corona, haijalishi wazuie mindege watakavyo lakini msimamo wetu ubaki ule ule.
Museveni ameweka jeshi kabisa kuzuia Watanzania, Kagame kule naye naskia huwa mkali sana dhidi ya Watanzania, Zambia na majirani wote wa Tanzania wote wana misimamo mikali, sisi tusilegeze pia, tuhakikishe usalama wa afya yetu ni kipau mbele.
Hawa Watanzania walijichokea na kushindwa kwenye juhudi dhidi ya corona, kwao huko imekua gonjwa la aibu, ukiumwa inabidi uhangaike ndani kwa ndani na kuifanya siri majirani wasijue maana utanyanyapaliwa sana, tangu ile siku namba zao zilipandisha ghafla na kuwa 509 kisha rais akawa mkali, waliufyata wote.