Kenya yafanikiwa kurusha Satelite yake kwenye mzingo wa Dunia kwa kutumia Roketi, Tanzania kufanya hivyo mwaka 2025

Kuna matatizo mengi tulionao hapa (earth) sasa huko hiyo satellite itasaidia wapi?

Kama ni issue ya 'promotions' kwanini hiyo satellite warushe kutoka USA..
 
Kuna matatizo mengi tulionao hapa (earth) sasa huko hiyo satellite itasaidia wapi?

Kama ni issue ya 'promotions' kwanini hiyo satellite warushe kutoka USA..
Satelites zinasaidia kutatua matatizo ya dunia. Nchi nyingi zina satelites lakini warushaji satelites ni wachache ama US, au India, au Russia, au china au umoja wa Ulaya. So ukitengeneza satelite itabidi uende kwenye mataifa hayo uzuri US warushaji wengi kampuni binafsi so unaweza tafuta ikayokufaa
 
Wewe ulishaumaliza umaskini na njaa Tanzania? Mawazo ya mjinga. Miaka 60+ ya Uhuru unafikiri wenzenu watakalia tuu cheap politics za ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo. The world has to move on....despite challenges mbalimbali. Kila sekta ifanye kazi yake.
Kilimo kipunguze njaa
Teknolojia isonge mbele
 
Kuna matatizo mengi tulionao hapa (earth) sasa huko hiyo satellite itasaidia wapi?

Kama ni issue ya 'promotions' kwanini hiyo satellite warushe kutoka USA..
Fanya yako tuone utarushia wapi. Movie tu ya samia ilitengenezewa huko sembuse satellite.
 

Mkuu ngija nikuelimishe kidogo usipotoshe wengine Satellite kazi yake sio ku host ,

Hosting zinafanyika duniani maana servers zinahitaji eneo kubwa na miundombinu ya uhakika kama umeme na internet ya kasi pamoja na watu wa ku mantain hiyo kind of structure huwezi iweka kwenye orbit

Satellite zina kazi tofauti na kazi kubwa huwa ni kwa ajili ya mawasiliano kama unavyopata channel hapo nyumbani kwako kwa kutumia dish

Kazi nyingine nyingi ni kwa ajili ya uchunguzi hasa wa hali ya hewa na vitu vingine vya ki reserch hapa duniani

Zipo sattelite za kuchunguza anga la mbali na mifumo ya kiusalama za nchi tofauti tofauti

Na hapa majuzi Space X ime launch satellite zaidi ya elfu 2 kwenye orbit ya dunia kwa ajili ya internet inayoitwa Starlink hii ndio internet ya kwanza public inatotumia satellite

Satellite zinajengwa kwa material mepesi na kwa umbo dogo as possibile na inawekewa vifaa vinavyotumia umeme mdogo na battery za ku reserve umeme na solar panels kubwa maana source ya umeme huko angani ni jua tu
 
Tunaanza kupiga fix Starlink wana zaidi ya satellites 🛰 4,000 kwajili ya internet tu toka mwaka 2019 hii taarifa mnazipata wapi?
 
Nimeamini katika kila mafanikio ni lazima yawe na juhudi kubwa sana ambapo juhudi zenyewe hubebwa na vitendo ndani yake

Wenzetu wakenya wamefanikiwa sana kwenye masuala mbalimbali kutokana wamewekeza kuanzia chini kabisa wamewekeza kwa kutazama watu wa baadae au kizazi cha miaka 50 inayokuja ndio maana unaweza kukuta msingi wa kila kitu wanauanzia kwa watoto wadogo

Nfano mwingine Shirika la Nasa kwa kufahami hilo wameweka connection baina yao na Mashule na taasisi mbalimbali za elimu ili tu waweze kuanza kupata watu kutokea chini na wao baada waje wawaendeleze ili waje kuwatumikia katika taasisi yao

Mfano Ukichukulia Nasa jinsi wanavyotegemea Chuo cha California Jet Propulsion , hichi ni chuo cha kisayansi ya tekinolojia ambapo wenyewe wanashughulika na utengenezwaji wa vifaa vyote na vyombo vyote vya anga za mbali visivyobeba watu , Ukichukulia mfano wa vyombo kama vinavyotua mwezini na vile.vilivyowahi kwenda Mars na kwenye sayari nyengine

Utaweza kuona Nasa wanafahidika na kile kitu walichokiwekeza kwenye chuo hicho ambapo kimekuwa kikitoa wafanya kazi wengi wa NASA

Wenzetu wamefika mbali kwa kuwekeza katika maono yao ya baadae
 
Kwa kuongezea tu NASA ni kama wanamejipa jukumu la kuzipanga satellite kimehesabu ili zisigongane daima katika mizunguko yake nilitizama interview moja bbc swahili kuna dada wa kitanzania anafanya kazi nasa anasema yeye yupo kwenye kitengo icho cha kupanga satellite za ulimwengu ili zisigongane kamwe nilistaajabu kumbe kuna mtanzania anafanya kazi nasa tena anaongea kiswahili safi kbs na amesema anachokutana nacho nasa ni hesabu halisi alizokutana nazo darasani hivyo akawataka wanafunzi wanapo ambiwa watafute sijui mambo ya thamani ya x sijui kipeo kikuu cha shirika wasione tabu yey amekutana na izo hesabu kweny kazi yake
 
CHOMBO CHA JUICE CHAANZA SAFARI YAKE KUELEKEA SAYARI YA JUPITER

Siku ya jana umoja wa ulaya uliweza kurusha chombo anga za mbali ambacho kimepewa jina la Juice space craft kuelekea katika safari ya miaka 7 ya uchunguzi kwenye miezi mbalimbali ya sayari ya Jupiter

Mwanadamu amebaki na maswali mengi sana juu ya miezi kadhaa ya sayari ya Jupiter ambayo mengine ndani yake imejawa na barafu bila kusahau ule mwezi wa Ganymede wenye kiasi kikubwa cha maji kuliko maji yote yanayopatikana duniani

Chombo hicho kilibebwa katika rocke ya umoja wa ulaya inayojulikana kama Ariane 5 ambapo tutahitajika kusubiria kipindi cha miaka 7 kwa chombo hicho kuweza kufika katika miezo hiyo ya Jupiter

Kumbuka sayari ya Jupiter ni sayari namba 2 yenye miezi mingi zaidi katika mfumo wa nyota Jua huku namba moja ikishikwa na sayari ya Saturn

Mwanadamu bado anaendelea kutafuta alama ya maisha ya viumbe hai katika maeneo mbalimbali huku akiwa ana kiasi fulani cha uhakika huenda kwenye mwezi wa Ganymede kukawa na maisha ya viumbe wa majini
 
Mbona Tanzania kuna omba omba wengi tu mtaani??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…