Kenya yakumbwa na baa kubwa la njaa, tayari watu 150k wanahitaji msaada wa dharura

Madhara ya copy and paste kutoka kwa mabwana zao badala ya kuangalia njia zinazofaa na kuendana na hali ya nchi yako ndio haya sasa.
 
Mzee wa kajiado mnyuko wa njaa unaendeleaje hapo chini ya lockdown?
Kwani kuna sehemu yeyote nchini Kenya ambapo kuna lockdown? Hizo ndio pumba na propaganda ambazo mnatumia kujiliwaza huko kwenu Manzese kwenye vijiwe vyenu vya kahawa, kuhusu 'kaugonjwa kadogo ka corona'? Gatuzi tano tu Kenya kati ya 47, Mandera imeongezwa leo hii, ndio zipo chini ya 'travel restrictions' za kuingia na kutoka. Nairobi Metro, Kilifi, Mombasa na Kiambu. Tena hiyo haijawabana wale ambao wapo kwenye shughuli 'essential' za kiuchumi na huduma za kiserikali.
 
Hawa jamaa ni juzi tu wametuma tani kibao za matunda kwenda uingereza. Ifike muda waafrika tuanze kutumia akili asee!
 
Kiswahili kigumu mkuu. Mleta mada ni team lockdown hapo kwenye uzi anapigia debe lockdown
[emoji1][emoji1][emoji1] Umenikanganya Numbi, anyway tuache na hizi ligi zetu za kilofa humu. Sisteh, huu ni wakati wa kujiburudisha sio malumbano na stress za ovyo. Nitapitia pitia kule kwenye zile nyuzi zetu stress free za amani nione mapya mazuri uliyotuandalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…