Kenya yamuita balozi wa Tanzania akafafanue sakata la vifaranga na kupigwa mnada kwa ng'ombe

Kenya yamuita balozi wa Tanzania akafafanue sakata la vifaranga na kupigwa mnada kwa ng'ombe

Dah hata Mimi nashangaa mkuu
Kwa nini Watanzania huwa hatupendi kuheshimu mawazo ya watu wengine!? Na kusimama pamoja inapokuja katika masuala ya TAIFA kwa manufaa ya Watanzania wote kwa ujumla!? Inasikitisha sana.
 
Ila wakenya nao wanawashwawashwa sasa hao vifaranga si walishamuuzia mtanzania?

Wakulalamika ni mtanzania sababu yeye ndio aliewanunua na kuviingiza Tanzania kimagendo sasa Kenya kina kuwasha nini wakati pesa ulishalipwa?

Pilipili ale asha kuwashwa awashwe fulani
 
Hizi habari sio za kuaminika!sizani kama tunaweza kufika uko sababu ya Chicks! Labda kuna lingine Nyuma ya pazia exposed by political matter!
 
Ni vema kujadili watu wamepakati sehemu zote bara Africa wanamahusiano, maofisa wetu wakati mwingine wasifanye kazi bila kuzingatia busara, diplomasia ni uhusiano mwema, mipaka waliweka wakoloni ni vema tukajali zaidi undugu wetu, tutekeleze sheria kwa hekima.Si jambo jema kuchuma vifaranga kwa utaratibu ulitumika bila mamlaka husika kwa majirani kushirikishwa.
 
Ila wakenya nao wanawashwawashwa sasa hao vifaranga si walishamuuzia mtanzania?

Wakulalamika ni mtanzania sababu yeye ndio aliewanunua na kuviingiza Tanzania kimagendo sasa Kenya kina kuwasha nini wakati pesa ulishalipwa?

Pumbavu kabisa wewe
Ukiwapa majibu Stahiki kama haya utaambiwa una mipasho mkuu. Wapuuzi sana hawa jamaa!
 
Huyo aliyeleta aliokota? Bidhaa zinazotoka China zina vigezo gani na mbona punda wanachinjwa kila siku na hatuambiwi ni daktari gani kaenda kuwapima ili wasafirishwe kwenda China. One sided decision or double standard. Mimi naunga mkono haya yote mradi yangeenda kwenye uwazi na sheria na kuhusisha wahusika wa wizara zote.
Tatizo wewe unatanguliza udaku katika mazungumzo ya msingi, unaushahidi wowote ule juu ya kuchinjwa na kusafirishwa kwa punda zaidi ya udaku wa maneno ya kwenye mitandao? nchi haziongozwi kwa jinsi unavyopenda, zinaongozwa kwa kufuata sheria zilizotungwa na kuwekwa na wananchi wenyewe, kama unadhani kuna sheria imekiukwa, kila mtu anayo haki ya kwenda mahakamani kutafuta haki hiyo.
 
Unaongea pumba ww...Wa tz wengi tuna nufaika na huu urafiki wa kenya ..nenda sehem kama namanga uone biashara wanavyofanya Wa tz na wa kenya....haya mambo ni ya kukaa na kuyatatua kidiplomasia
Hawa wakenya wanaenda kupigiwa magoti

Ngoja tunyooshane kwanza ili tukikaa kwenye mijadala ya ki diplomasia basi tuwe tunaheshimiana mkuu.

Mkuu akaze tuu mpaka pale wakenya watakapoa acha dharau
 
Unaongea pumba ww...Wa tz wengi tuna nufaika na huu urafiki wa kenya ..nenda sehem kama namanga uone biashara wanavyofanya Wa tz na wa kenya....haya mambo ni ya kukaa na kuyatatua kidiplomasia

Sawa.Lakini kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo.Diplomasia nayo ina sheria na taratibu zake!
 
Kwa nini Watanzania huwa hatupendi kuheshimu mawazo ya watu wengine!? Na kusimama pamoja inapokuja katika masuala ya TAIFA kwa manufaa ya Watanzania wote kwa ujumla!? Inasikitisha sana.
Imefika kipindi mtu utakubali siasa zinatupeleka kubaya kwani kila kampeni tunategemea madhaifu ya tunaepambana nae
Hivyo anapoonesha uimara mtu huhisi kufirisika kisiasa
 
Wakulima wa tz walipokatazwa kuuza mazao kenya wakaanza kulia....
 
Kukiukwa kwa taratibu hizo hakutoi loophole ya kuteketeza viumbe husika Kama Hakuna outbreak ya Ugonjwa usiotibika.

Mbona wale ng'ombe hawajachomwa moto?
Tatizo lako wewe ni uwelewa mdogo unaokusumbua, mwisho utasema gari zikikamatwa zimeingia kiholela zichomwe moto, watu walioingia bila vibali pia wachomwe moto, tumia akili uliyopewa na mungu katika kufikiria mambo, kila jambo linapangiwa sheria kutokana na mazingira ya wakati uliopo, kipindi cha Ebola tahadhari iliyochukuliwa mipakani na sasa hivi ni tofauti kabisa, kukutokea ugonjwa wa foot and mounth disease au kimeta, na ikaonekana kuna hatari ya kuenea katika hizi nchi zetu, hata hizo ng'ombe pia zitawashwa moto
 
Tatizo wewe unatanguliza udaku katika mazungumzo ya msingi, unaushahidi wowote ule juu ya kuchinjwa na kusafirishwa kwa punda zaidi ya udaku wa maneno ya kwenye mitandao? nchi haziongozwi kwa jinsi unavyopenda, zinaongozwa kwa kufuata sheria zilizotungwa na kuwekwa na wananchi wenyewe, kama unadhani kuna sheria imekiukwa, kila mtu anayo haki ya kwenda mahakamani kutafuta haki hiyo.
Machinjio ya punda yapo tena wanayaoneshaga hadi kwenye habari za ITV hujawai ona?
 
Kwa mfano tukapata mgogoro tukawa hatuna mahusiano chanya nao wazan wataoumia ni kina nani.....serikali au wananchi
 
Back
Top Bottom