Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Hoja wanazo. Kama huyu ametoa hoja. But pia unaweza ukapita tu sehemu mtu akakuona asikupende jinsi unavyotembea...wanampinga bila hoja za msingi ndio maana tunasema wanaongozwa na chuki.
1. Unatembea kibabe
2. Unatembea unajifanya kama mcha Mungu kumbe mnafiq
3. Unatembea kwa kujisikia
Watu waruhusiwe tu kumchukia kwa sababu walizo nazo. Tutamwonesha ni dhaifu ikiwa tutadhani anapopingwa anapingwa sababu ni Jinsia Ke.
Tutaonesha Dini ni dhaifu ikiwa tutatumia kama excuse kuzuia asipingwe kwa sababu safari hii huyu ni wa Dini yetu. Magufuli kuna ambao walikuwa wanamwona hana makosa. But alipingwa na Wakristo pia. Na hapo nlijifunza kuna watu si wanafiki.
Ila sasa huyu naona vigezo vya kumtetea asipingwe ni vingi
1. Dini
2. Jinsia
3. Asili yake
Watu wanatumia vigezo hivyo ili aimbiwe nyimbo za sifa/na mapambio. Si sahihi.
Mimi huwa nawaheshimu hata wanaonichukia bila sababu. Ni haki yao ya msingi.