Very stupid question. Wewe kwa nini unataka apendwe na watu wote? Mitume tu hawakupendwa na watu wote. Itakuwa binadamu? Kila mtu ana haki ya kumpenda na kumchukia amtakaye usiwapangie watu. Na vigezo vya dini,jinsia, sijui nini ni vya kipumbavu. Magufuli alichukiwa na waislamu,wakristo na wasio na dini. Tegemea na mwingine naye atachukia na watu tofauti tofaut kwa sababu tofaut tofaut.
Kwa nini sisi wengine mtu akichukiwa tunakimbilia kwenye dini yake? Mbona walioongoza kumpinga magufuli walikuwepo maaskofu pia?
Tusiwe dhaifu kiasi hiki kujificha kwenye kichaka flani kila tunapokosolewa. Wasiwasi wangu utakuwa sasa akikosolewa kuna watakaosema ni sababu ni mwanamke. Kuna wapumbavuh wengine watasema sababu ni dini flani.
Wengine nao watakuja na akili za hovyo kwa sababu ya aliyetoka alikuwa hivi na vile ....
Acheni hisia na mihemko. Tumieni akili. Kila mtu anaruhusiwa kupenda na kuchukia aamuacho.