Kenya yavunja rekodi ya deni la Taifa mpaka kuvunja sheria, Tanzania tumejipangaje?

Kenya yavunja rekodi ya deni la Taifa mpaka kuvunja sheria, Tanzania tumejipangaje?

Mkuu Mimi sio mtaalum wa uchumi hivi kukuwa kwa uchumu si lazima kuwe na matokeo chanya kwa mtu moja mmoja au mimi ndo sielewi


Mtu mmoja mmoja mwenyewe sio mimi huku Kajunjumele au mtu wa Nanjilinji, ni wale ma-giants, kama mawaziri na wafanyabiashara.

Huko developed countries poor people, homeless, na jobless wapo pia.
 
Utawala wa William Ruto umeshutumiwa kutokana na mwenendo deni la Taifa nchini Kenya huku akiwa ndiye Rais aliekopa pesa nyingi zaidi ndani ya mwaka mmoja tangu Taifa la Kenya liumbwe.

Deni hilo limeongezeka kwa $ bilioni 10.8 kufikia $ bilioni 70.75 kulingana na takwimu zilizotolewa Jumanne huku ukuaji wa uchumi wa Kenya ukishuka mpaka 4.8% kutoka 7.6% huku mfumuko wa bei ukifika 7.3%

Kwa Tanzania, deni la Taifa liliongezeka kwa Tshs trilioni 21 ndani ya miezi 6 kufikia Disemba 2022 likiwa ndio ongezeko kubwa zaidi kuwahi kutoka katika historia ya Tanzania huku watawala wakiwatoa watanzania hofu juu ya uvumilivu wa deni hilo.

Kenya wana mwisho wa kiwango cha juu cha kukopa(Debt ceiling) kilichopitishwa kisheria ambacho ni Kshs trilioni 10 lakini deni hilo limefika trilioni 10.1 na moja ya hatua Kenya inayotarajiwa kuchukua ni kuacha kukopa huku Bunge likibadili sheria ya ukopaji.

Sidhani kama Tanzania tuna 'debt ceiling' na mipango ya kulipunguza spidi ya ukuaji deni la taifa maana deni kupungua imekuwa ni ndoto kwa nchi nyingi za dunia ya tatu. Nini kifanyike?
Hatari sana🙌🙌
 
Back
Top Bottom